Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Ndugu mama Samia.
Umetufungia JF tusiiaccess ndani ya Tanzania, lakini tutakueleza ukweli na utakufikia.
Iko hivi mama yangu, ndani ya nchi yetu kuna vilio kila kona, watu hawaridhiki na nchi inavyokwenda.
Mimi nitakueleza ukweli tu, ukitaka chukua ukitaka achana nao. Kuna hali ngumu ya maisha, huduma za kijamii ziko hovyo, uhuru wa habari serikali yako inautia kitanzi kila kukicha, Kuna vilio kila kona vya utekaji, Rushwa na upigaji umekithiri, Hata fursa ya watu kutoa dukuduku kupitia chaguzi utawala wako umeifungilia mbali, eti unagombea mwenyewe na Salum Mwalimu wa chama cha mchongo. Aibu gani hii!.
Leo nilikuwa nasoma kwa Dada wa Taifa (Da Mange) kuwa hata watu wa vyombo nao wameanza kuguna, na kujihisi kusapoti maandamano yanayotangazwa.
Sasa ndugu Samia, Stuka, usizibe pamba masikioni. Chukua hatua, fanya reforms kutuliza hii nchi. Usipouanika usije ukashangaa unautwanga mbichi!
Usiweke imani sana kwa vyombo ukadhani kuwa wataweza kuziba ombwe la kisiasa. Hivi vyombo Madam dunia nzima huwa havitabiriki, ndiyo maana wenzio huwa wanavitumia kama last resort kunusuru hali badala ya kuwa kama strategic ya kisiasa ya kuwashinda wenzio kisiasa.
Madam, nchi imevimba hii, usidhani kuwa uwekeze kwanza kwenye uchaguzi, ushinde, utangazwe, halafu eti uanze kutibu madonda na majeraha kwa kuitisha mchakato feki wa mabadiliko ya katiba ukidhani kuwa hilo litautuliza umma!. Hilo halitatokea kwa sababu zifuatazo.
1. Umma hauamini kama wewe unaweza kuleta reforms wanazozitaka. Maana ulikuwa na fursa ya kuleta reconciliation nchini, ukavurugavuruga zile 4R zako. Sasa waprove wrong NOW. Ukiweza hili, pengine utapata uungwaji mkono!
2. Hali ya maisha ya wananchi ni ngumu mno, mambo hayaendi, umma hauwezi kukubali kudanganywa kwa kuwapa fupa la mchakato wa mabadiliko ya katiba, wakati wanasoma mitandaoni kuwa wateule wako wanamiliki ma Rolls Royce, Mabuggati, Lamboghini na watoto wao wanapigwa video wanakumbatia mabulungutu ya dola.
3. Hutaweza kuwapa watu hope ya kubadili maisha yao, wakati umeshakuwa kwenye power kwa miaka 10, nusu kama makamu na nusu kama rais, Je una lipi jipya?
Kwa hiyo madam president, cha kufanya sasa ni kukubali ukweli kuwa ipo haja ya kufanya reforms kabla ya uchaguzi ili Taifa liwe moja, turudishe imani katika process ya uchaguzi. La Sivyo, ukishupaza Shingo madam, ni kweli utatangazwa kushinda hapo november, lakini utajikuta nchi nzima imekususa. Utatawala kwa shida mno madam. Chukua hatua now!