Hammer11
JF-Expert Member
- Feb 18, 2024
- 1,518
- 2,174
Wadau, mnakumbuka nilileta uzi kuhusu binti aliyekwenda nchi za Kiarabu kufanya kazi? Sasa hivi, kuna jambo limetokea na nipo njia panda.
Kwa kifupi, mimi kwao sijulikani vizuri, wazazi wake wanaamini mimi ni bwana wa mtoto wao, lakini ndugu zake wanajua ukweli. Juzi tarehe 11, binti alinipa kama shilingi laki 3 hivi na kuniambia nione simu nzuri nipeleke nyumbani kwa mama yake. Aliniambia kwamba ile simu itanigharimu kama 250,000 na hiyo 50,000 iliyobaki niichukue kama zawadi.
Baada ya kununua simu hiyo kwa 250,000, alinielekeza niseme kuwa simu hiyo nimenunua online, na kwamba alinipa kazi ya kuifikisha nyumbani. Nilifanya kama alivyosema; nilipeleka simu na kutoa maelezo kwa mama yake kama alivyonielekeza, kisha nikaondoka zangu.
Sasa, shida ni kwamba mama yake aliporudi nyumbani na kuambiwa kuhusu simu, alimkasirikia sana binti yake na kumpigia simu akamfokea. Mama huyo amesema hataki kabisa kuniona mpaka mtoto wake aje mwenyewe na kunitambulisha rasmi. Cha zaidi, mtoto wake anarudi baada ya miaka miwili! Mama huyo ameenda mbali zaidi na kusema hata hataki kutumia ile simu, na tayari mimi nishaigharamia.
Sasa hapa ndipo njia panda inapoanza. Nimemwambia binti kuhusu hali hiyo, na yeye ananiambia nisiwe na wasiwasi kwa sababu ananipenda sana. Sasa, najiuliza:

- Nimshawishi huyu binti tujenge maisha kwetu wenyewe bila kushirikisha sana mama yake?
- Ama nimpotezee kabisa huyu binti na niendelee na mambo yangu?