Pole mleta mada, hilo wazo lako sisemi kwamba ni baya ila mimi binafsi sikushauri kufanya hivyo.
Watu wa siku hizi wamegeuka kua nusu wanyama, unaweza kutafuta mtu kua mama yako wa hiari lakini matokeo yake ukawa umetafuta balaa.
Mkuu be strong, mimi nilifiwa na wazazi wangu nikiwa darasa la 5, baba yangu alifariki sijaingia hata shule ya msingi then mama akafariki nikiwa std 4, siwezi kukusimulia ni kiasi gani nimeteseka kwa kuishi na ndugu, nimenyanyasika mno, nimeishi na kaka zangu wakati nasoma, wake zao wamenifanyia mambo ya ajabu sitakuja kusahau mpaka nakufa.
Mpaka hapa nilipofika sijisifu ila namshukuru Mungu, nimetoboa shule kwa shida mno tena mno, watu wengine wote niliosoma nao primary waliishia Form 4, niliosoma nao form 4 wengi waliishia hapo form 4, Mungu mkubwa niliweza kutoboa mpaka chuo kwa mbinde mnooo.
Baada ya kufaulu form 5 ndio atleast shemeji zangu wakaanza kuhisi mimi ni binadamu.
Naishia hapa, kuna wakati nammiss sana mama, kuna wakati natamani niwe na mama yangu ili nikipata hata shilingi elfu moja nimpelekee, yaani nikipata likizo kazini hua natamani nikienda home nimkute mama yangu, nimbebee mazagazaga kibao.
Hua nikiwaza mambo ya mama siku yangu inaweza kuishi hovyo sana.
Nakomaa, sasa nina familia, nina watoto, nina mke, nina kazi, uhakika wa ugali na mambo madogo madogo upo. Namshukuru Mungu sana, ila mke wangu bado hawezi kuziba nafasi ya mama yangu hata kwa 0.5%.
Komaa na maisha, jikaze kiume.