Hii dunia usipokua na roho ngumu kila jambo litakutoa machozi.
Kaza moyo ndugu yangu, mimi nakaza moyo na sikuwahi kua tayari kushindwa tangu nikiwa shule mpaka leo, neno kufeli sitakikulisikia, kubaliana hali kwamba huna mama pambana, jitahidi ulinde damu yako ili usiwache wanao mapema wakapata shida, na jitahidi sasa uwe na familia kidogo utapata faraja.
kua na familia mimi imenisaidia kiasi flani, japo kuna wakati nakua stressed sana tena nikimkumbuka mama yangu, hata ndugu kama dada, kaka, mama mdogo, mama mkubwa, mjomba wote hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kunitafuta wanapokua wanataka pesa zangu na wanapokua wamekwama wanahitaji mawazo yangu na hasa hasa pesa.