Mama wa John Heche aenda police central. "Mrudisheni Mtoto wangu”

Mama wa John Heche aenda police central. "Mrudisheni Mtoto wangu”

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mama Mzazi wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Weisiko Heche, jioni ya leo amefika katika Kituo cha Polisi Kati Jijini Dar es salaam ili kuomba kuelezwa alipo Mtoto wake huyo ambaye alikamatwa na Polisi jana October 22 2025 akiwa anaingia Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Dar es salaam.

Weisiko akiongea na Waandishi wa Habari nje ya Kituo cha Polisi Central amesema baada ya kufika katika Kituo hicho cha Polisi alimpigia Kamanda Muliro lakini hakupokea kisha baadae akapiga simu kwa Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Camilius Wambura ambaye alimwambia asubiri atapewa majibu “baadae nikapiga simu tena kule Dodoma nikaambiwa naweza nikaondoka maana hapo wamekataa kabisa kwamba hawajamuona hapo, ombi langu mimi ni kwmaba warudishe Mtoto wangu”

 
Wasivyo na mishipa ya aibu wakiambiwa wao ndiyo watekaji, wanabisha! Sasa ile jana wamemteka mahakamani, na kila mtu aliona! Usiku niliona kwenye chombo kimoja cha habari wakiwa wamempakia kwenye Double cabin nyeupe mpya waliyonunuliwa na Bosi wao!!

Hivi ujasiri wa kusema hawahusiki na kumkamata, watautoa wapi!
 
Hapo target yao ni kumuachia baada ya uchafuzi tarehe 29, sirikali ya kimaku sana hii!.
Hv jeshi letu la wananchi linakwama wapi kupindua meza, haiwezekani kutawaliwa tena na hawa wahuni!.
 
Daaah . Ndiyo inaanza hivi hivi siku ,wiki ,mwezi ,miezi,mwaka ,miaka . Na ndiyo inakuwa basiii tena ... Mungu wewe ndiye mtetezi wetu basi
 
Write your reply...kumbe limama lake nalo lihalifu na pia linatibiwa india inatakiwa lingetandikwa viboko nalo
 
Leo Ijumaa hadi j4 tutegemee Wanasiasa na wanaharakat weng kukamatwa na kuwekwa kizuiani had tar 29 ipite.

Heche yuko Salama . Next week watamfungulia kesi. Upepelez utakuwa haujakamilika na wiki ile kuanzia Jumatatu ya tar 3 Nov watamuachia kwa dhamana.

Lissu yeye atasubiri DPP mpya atakayechaguliwa na Samia . Ndio atasema hana haja ya kuendelea na kesi.

Kwahiyo Lissu ni katikat ya mwez Nov.
 
Mama Mzazi wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Weisiko Heche, jioni ya leo amefika katika Kituo cha Polisi Kati Jijini Dar es salaam ili kuomba kuelezwa alipo Mtoto wake huyo ambaye alikamatwa na Polisi jana October 22 2025 akiwa anaingia Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Dar es salaam.

Weisiko akiongea na Waandishi wa Habari nje ya Kituo cha Polisi Central amesema baada ya kufika katika Kituo hicho cha Polisi alimpigia Kamanda Muliro lakini hakupokea kisha baadae akapiga simu kwa Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Camilius Wambura ambaye alimwambia asubiri atapewa majibu “baadae nikapiga simu tena kule Dodoma nikaambiwa naweza nikaondoka maana hapo wamekataa kabisa kwamba hawajamuona hapo, ombi langu mimi ni kwmaba warudishe Mtoto wangu”


Mama Samia hivi hawaoni wanawake wenzake wanavyopata shida kwa WATOTO wao kutekwa bila sababu za msingi ....!!?

Haya yote huwa hata hataki kuyagusia kwenye hotuba zake za Tanzania ni PEPO .....!!
 
Back
Top Bottom