Mama mtu mzima ,umri miaka 40 anatafuta kazi ya usafi wa nyumba za kulala wageni ,au kazi yoyote halalI ajipatie kipato,.
MahalI popote pale hata kijijini.yupo tayari
Mkuu; vipi umeamua kuanzisha uzi wa dizaini hii? Uzi huu kwa kupitia hizo komenti za wadau na majibu uliyotoa, ninashawishika kuchangia hivi:
1. Huyo mwanamke mtu mzima unayemsemea, huyo ni mtu HEWA i.e. HAYUPO KABISA ni Mtu wa kuchonga ni FAKE.
2. Wewe
katika Fiction au igizo hili umejipa nafasi ya UDALALI halafu unawa-enjoy watu kwa kuona jinsi wanavyotiririka. (Hili halina shida)
3. Tangazo lako hili lina mapungufu mengi mno e.g.
(a)Mtu gani anatafuta au anatafutiwa kazi halafu hakuna/haweki wajihi (sifa zake i.e. CV yake basi walau hata useme anajua kusoma na kuandika, hana matatizo ya kiafya/akili/viungo n.k. n.k.
(b) Wapo wadau wametaka mawasiliano naye lakini ww unasema hana simu i.e. hana hata majirani wenye simu? kweli? Na ww haukuonesha wala nia au ridhaa kumsaidia kupitia simu yako!!! Ina mana mhusika hajui kinachendelea kumhusu yeye mwenyewe.i.e. Yupo gizani na hiyo shida yake.
(c) Umewaeleza wadau kwamba yupo Moshi. Lakini hukutaja ni Moshi mjini, vijijini au wapi e.g. Kata, Kitongoji etc. kana kwamba huyo mama hana ndugu, majirani, haishi ndani ya Jamii ila wewe ndo umejitolea kumsaidia kumtafutia kazi. Kwani huko Moshi imeshindikana
Locally kupata kibarua/kazi mpaka umeileta shida yake huku jamvini? Mbona Moshi kazi ni nyingi mno ila baadhi ya watu wanachagua kazi i.e. Wanaringa.
(d) Vipi ; huyo mama hana hata mtu mmoja wa kuzaliwa naye i.e. hana kaka, dada au wadogo zake? Hakuwahi kuolewa?
MWISHO:
Naomba uniwie radhi kama nimekukwaza kwa hii komenti yangu.
Ila ni ruksa kutoa povu bila matusi.