Mama wakati wewe haupo, mengi yametokea

Mama wakati wewe haupo, mengi yametokea

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Zitto katuambia kumbe zile korosho mlizimwaga baharini, watu wana siri sana.

Mama Kikwete anataka eti na yeye alipwe kiinua mgongo cha mmewe.

Kingine mama wakati wewe uko royo tua msajili amekipiga kufuli chama cha Umoja kutumia picha ya mtangulizi wako eti yeye sio mwanachama wake.

Naye balozi mstaafu wa Swideni katukataza kuijadili ripoti ya CAG, hivi mama sawa hiyo.

Wakili msomi Peter Madeleka alipotea polisi wakasema wao waliye naye ni Peter lkn sio Madeleka, kelele zilipozidi wakamwachia.

Zitto tena katuambia tunaompenda Magufuli eti tukazikwe pembeni mwa kaburi lake, naye Kibajaji akamwambia akazikwe pembeni mwa kaburi la mama yake. Uhuru ulizidi sana.

Rais wa nchi ya jirani ya Muungano wetu katuambia ukweli usiouma kwao kuwa aridhi ni ya wazanzibari tu wengine kumiliki ardhi mwisho Nungwi eti mama ya kweli hayo.

Msekwa naye katuambia asiyeupenda muungano ajinyonge.....

Naye spika aliyestaafishwa kaibukia bungeni watu eti alipotea mambo yalikuwa mengi sana mama.

Mwisho usio mwisho sana leo ukimaliza kuzindua Royo Tua hapo karibu na mlima Kilimanjaro nakushauri upumzike kidogo.

Karibu tena nyumbani Kazi iendelee.
 
Umeamua kumwaga mchele kwa mama siyo !!

hii nchi ina SIRI nyingi sana, ukiwa mfukunyuzi unaweza kuchizika kama ukizifahamu..ni za kuacha tu kama zilivyo... cha msingi kunakucha dunia haisimami.
 
Watoto wa kambo tunapata nao shida sana.

Hivi msukuma alisemaje vile.

Halafu boss wa huku alisema nini vile,

Ukiwa mmbeya uwe na kumbukumbu
 
Umeamua kumwaga mchele kwa mama siyo !!

hii nchi ina SIRI nyingi sana, ukiwa mfukunyuzi unaweza kuchizika kama ukizifahamu..ni za kuacha tu kama zilivyo... cha msingi kunakucha dunia haisimami.
Kuna kufuru huwa zinafanyika huko ndani acha kabisa.
 
Watoto wa kambo tunapata nao shida sana.

Hivi msukuma alisemaje vile.

Halafu boss wa huku alisema nini vile,

Ukiwa mmbeya uwe na kumbukumbu
Kwamba wanaomponda Magufuli baada ya kufa ni wanafiki kasoro Nyalandu
 
Back
Top Bottom