Mama yako na Mke wako nani anastahili kukaa siti ya mbele ya Gari yako mnapotoka wote kwa pamoja?

Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Mwanaume aweza kuwa na wake wengi ila mama ni mmoja tu. That's one. Pili, siti zinatofautiana hadhi?

Hoja hizo zikusaidie kufikia maamuzi.
 
Yupi anayestahili ulinzi zaidi ya mwingine, mke au mama?

Swali tuliulizwa zamani hilo,... 'mtumbwi unataka kuzama, nani hapo utakayeanza kumuokoa, mama au mkeo?'.
Kwangu mama yangu ndio anastahaili ulinzi zaidi kuliko mke wangu, hapo lazima nimuokoe mama, mke wangu atasubiri kama kutakuwa na nafasi ya kumuokoa mtu mwingine ataokolewa kama haipo basi itakuwa ni Mungu ametoa na sasa ametwaa.
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
ni muhimu sana,
wote wakae huko nyuma, mbele kuna mambo mengi kwenye kuendesha gari 🐒
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Kwani hilo gari ni lazima uendeshe wewe. Si anaweza kuendesha mkeo?
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
We dereva kuwa wa kwanza kuingia kwenye gari humfungulii mtu mlango atakaye wahi seat unasepa nao ivo ivo mama akiwa mbele barid wife poa tu ukianza kuwaza hayo ni kujiletea complications
 
Binafsi sipendi kukaa mbele,nitakaa tu kama naendesha mimi lakini kama dereva ni mwingine huwa mimi nakaa nyuma.
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Familia nzima hamtakiwi kupanda gari moja hivyo.

Ikitokea ajali msiba usiwaondoe wote kwa mpigo.
 
Mimi Na Wanangu Tunakaa Nyuma Huku Nikiendelea Kunyonya Mvinyo Taratiibu,,Mke Dereva,,Mama Amevunja Kishoka Pembeni Ya Mkwe Wake.
 
Wakuu naomba ufafanuzi katika hili.

Je Mke anapaswa kumuachia Mama siti ya mbele akae na mwanae na yeye akae siti ya nyuma.

Au Mama ndiye anayepaswa kukaa siti ya nyuma.

Naona kama hili suala ni mtambuka, naomba kujuzwa.
Hakuna Mama anayejitambua atakayekaa siti ya mbele na mwanae halafu mkwewe akae siti ya nyuma. Ukiona mama yako anang'ang'ania kukaa siti ya mbele wakati mnasafiri na mkeo ujue kuna tatizo kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…