Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Katika mambo ambayo huwa siyasahau ni hili.
Mama yangu ndugu zake kadhaa wamesomea udaktari. Na hata jina alilonipatia mimi nila baba yake ambaye mpaka sasa ni daktari. Lakini pia mara mimi baada ya kuzaliwa na kupatiwa jina hilo la huyo baba yake, nilianza kuitwa jina la utani Dokta, Dokta.
Nilisoma sana kwa bidii ili na mimi nije kuwa daktari. Mara baada ya kuhitimu kidato cha sita na kufanikiwa kufaulu vizuri.
Nilimwendea mama yangu na kumwambia mama mimi nataka kuwa daktari. Aliniambia kwa upole kabisa mwanangu mimi sipendi wewe uwe daktari hivyo achana na mambo ya udaktari somea mambo mengine. Basi tangia siku hiyo siupendi udaktari kabisa.
Lakini maswali mengi bado najiulizaga kwanini mama hakupenda nisomee udaktari, mpaka leo sijawai pata majibu.