Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.

Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.

Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.

Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.


Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.


Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.


Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.

Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.

Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.


NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Pole sana! Umeshamjua, usimtumie pesa, zingatia maisha yako na kujiendeleza. Hakikisha hata wanaomdai wakija kwako, waambie hamna mkataba wa kumlipia madeni yake, hayakuhusu!
 
Back
Top Bottom