Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Ningekuwa na uwezo nisingekuj kulalamik uku jingejua tu chance yakupata fedha ipo ila ndo ivyo ...naningelipa it's ningewahaidi kulipa sta kidogo kidogo
Huku utapata wafariji na mawzo lakini hawawezi kukupa pesa Kwa maana kila mtu anapambana na hali yake huko duniani kuna watu wana matatizo wewe ni cha mtoto
 
Pole mkuu
Ni ngumu kuuchukua ushauri mgumu wa kumkacha maza mimi naona cha kufanya ni wewe kufatilia hayo madeni makubwa yamefikia wapi, pata details zote.

Kama mama huwa anakutafuta kwa uficho basi siku akikutafuta, tenga nae muda ujue yeye kajipanga vipi kuilipa hiyo mikopo na kama yupo tayari kuruhusu nyumba iuzwe.

Mueleze hali yako halisi kiuchumi kua hutoweza kumudu kumlipia/kupata hela za vizinga vyake.
Amenitafuta nimenweleza kasema atalipa anafanya vibarua apate ela alipe ayupo tayar nyumba kuuzwa nikamwambia mm sina chakusema pambana na mm sina ela unajua hsli yangu
 
Hauko peke yako mkuu
Hii ni tatizo la wanawake wengi sana hapa 255
👇👇👇👇👇👇
Hii ni kampuni ya BRAC (Sio black kama ulivyoandika), nilidhamini mshangaz mmoja huko sasa ameshindwa kulipa marejesho, amekimbia msala kaniachia.


Screenshot_20250417-064204.jpg
 
Mama ni mama ila akiwa vampire sio mama uyo , izo pesa zote ana peleka wapi au ni mlevi angekua ana ku support kupitia izo pesa sawa aila kama amna mpotezee ni ngumu kwako ila ukweli ndo uo mama ako ni katiri sanaaa
 
Hatari
Pole kwa chnagmoto unayopitia.

Nimepangialia andiko lako, ili kuwarahisishia wadau wengine:

---
Hali Yangu ya Sasa na Uchungu Moyoni

Wanajamii, sijui hata nianze vipi, natamani kulia na kupiga ukunga ili wote mjue jinsi ninavyoumia ndani kwa ndani. Uchungu nilionao ni mkubwa na ninatamani kupata mtu wa kumueleza, lakini nahofia kuchekwa. Sina kaka, dada, wala mdogo; nimezaliwa peke yangu. Hii hali imeninyima amani kabisa, nina maumivu makali moyoni na nahisi aibu kubwa hata kuwaeleza marafiki. Kama kungekuwa mahali pa kulilia, ningekwenda ili huu uchungu uishe.

Tatizo Sugu la Mikopo ya Mama

Kiini cha haya yote ni mama yangu kuwa na tabia ya kukopa kupita kiasi. Hali hii ilizidi baada ya baba kufariki, ingawa hata awali aliwahi kufilisiwa na baba akalazimika kulipa madeni yake. Alipoelemewa na madeni Dar es Salaam, alikimbilia kijijini, lakini kumbe na huko aliendelea na tabia hiyo ya kukopa bila hata kunijulisha. Mara nyingi huniambia anaumwa ili nimtumie pesa, nami kama ninayo huwa natuma.

Mkopo Mpya na Tishio la Kupoteza Nyumba

Kilichonisukuma kuwaandikia leo ni kuhusu mikopo mipya aliyoichukua Desemba kutoka kampuni mbili tofauti: moja ya Shilingi milioni 1.4 na nyingine ya Shilingi milioni 1, ambazo anatakiwa kurejesha kila wiki. Pesa hizi sijui hata alizifanyia nini maana nyumbani kijijini hakuna chochote cha maana zaidi ya kitanda na godoro. Watu wa mikopo walifika nyumbani wakitaka kuiuza nyumba aliyoiweka rehani. Kutokana na hilo, mama amekimbia (leo ni siku ya tatu) na hapatikani kwenye simu yake; inasemekana amekimbilia mashambani. Jana alifanikiwa kunipigia kwa namba ngeni akidai anaumwa sana miguu hawezi kutembea, nikamtumia Shilingi 20,000 kwa ajili ya matibabu, kumbe ilikuwa ni njia yake ya kunipiga kizinga tu.

Changamoto Zangu Binafsi za Kimaisha na Kipato

Mimi mwenyewe hali yangu si nzuri. Nilijitahidi kulipa baadhi ya madeni yake nikiwa chuo kwa kutumia pesa ya 'boom' na faida ya vibiashara vidogo nilivyokuwa nafanya, lakini mtaji uliisha. Kwa sasa sina kazi rasmi, nina kigenge kidogo tu ambacho napambana nacho lakini hakikui; hali yangu ni ileile kila mwaka, hata kunywa soda ni anasa. Ninaishi peke yangu katika chumba cha kupanga, napambana na ugumu wa maisha ya mjini lakini sioni maendeleo. Uwezo wa kulipa haya madeni mapya sina kabisa.

Changamoto ya Mawasiliano na Mama Kuhusu Madeni

Pia, kuna changamoto kubwa ya mawasiliano. Nikijaribu kumuuliza kuhusu mikopo yake, huwa mkali sana, tunaishia kugombana na anaweza kukata mawasiliano kabisa kwa kutokupiga simu.

Ombi la Ushauri: Nifanye Nini?

Wanajamii wapendwa, nimefika mwisho wa akili. Naomba sana msaada wenu wa mawazo: Nifanye nini ili kumsaidia mama aache hii tabia ya mikopo? Na nitawezaje kukabiliana na haya madeni mapya wakati uwezo wangu ni mdogo? Nimekuwa nikimuombea sana abadilike, lakini hali bado ni ileile. Nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya. Tafadhali nishaurini.
 
Inaumiza sana mkuu pole sana nasikitika kukwambia mama yako kashakuwa mraibu wa mikopo.

Huwezi kufukia shimo kwa kuendelea kulichimba, anachokifanya mama yako ni kutaka kufukia shimo wakati bado yupo ndani anaendelea kuchimba mwishowe itashindikana kabisa kutoka shimoni. Acha nyumba iuzwe ajifunze japo mtu kama huyo ni wakuwa nae makini sana.
Ukiendekeza hii mikopo ya riba ina uraibu mkubwa sana.
 
Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.

Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.

Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.

Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.


Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.


Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.


Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.

Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.

Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.


NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Hiyo ni tabia yake huwezi kubadili mara moja,. Hata mzee wako ameshindwa kurekebisha. Jaribu kushirikishisha ndg na jamaa mkae chini mumueleze. Hata iyo nyumba ikiuzwa basi alipe mikopo na aanze upya ila mikopo aachane nayo kabisa. Pole sana
 
Inaweza kuonekana kama sio kweli lakini kwa kiasi fulani mama yako alichangia kifo cha mzee wako kwa namna moja au nyingine. Vile vile nawe utakumbwa na fate iliyomkuta mzee wako mbaya zaidi wewe bado uko katika umri mdogo sana.
 
Vijana wengine sijui mmerogwa?? Baba yako ashafariki, nyumba, mashamba n.k vipo. Mama yako yupo mwenyewe na hana chochote cha maana anachofanya. Hakuna ndugu yeyote wa kukaa nyumbani na kulinda mali za familia. Wewe badala ya kurudi ukakaa nyumbani uongoze na kusimamia familia na vitega uchumi vilivyopo unakimbilia mjini kuuza genge, kupanga nyumba na kuishi kwa tabu. Tatizo ni wewe na si mama yako. Rudi kijijini simamia mji. Unatakiwa kujua wazazi wakikua wanahitaji kusimamiwa na sisi watoto wao.
Wajinga wanadanganywa eti kuishi kwao hawatopata mafanikio ...Mtu anaacha kwao kuna kila kitu anaenda kuzunguka mikoa ya watu .
 
Ukiendekeza hii mikopo ya riba ina uraibu mkubwa sana.
Sana mkuu ila wengi atujui hilo, mikopo hasa hii midogo midogo inazorotesha sana. Na wengi wanachukua mikopo wanaenda kuitumia kwa lengo tofauti kabisa na lililowafanya wachukue mkopo.
 
Inaweza kuonekana kama sio kweli lakini kwa kiasi fulani mama yako alichangia kifo cha mzee wako kwa namna moja au nyingine. Vile vile nawe utakumbwa na fate iliyomkuta mzee wako mbaya zaidi wewe bado uko katika umri mdogo sana.
Kwamba?!

Emotional Intelligence- 0
 
Vijana wengine sijui mmerogwa?? Baba yako ashafariki, nyumba, mashamba n.k vipo. Mama yako yupo mwenyewe na hana chochote cha maana anachofanya. Hakuna ndugu yeyote wa kukaa nyumbani na kulinda mali za familia. Wewe badala ya kurudi ukakaa nyumbani uongoze na kusimamia familia na vitega uchumi vilivyopo unakimbilia mjini kuuza genge, kupanga nyumba na kuishi kwa tabu. Tatizo ni wewe na si mama yako. Rudi kijijini simamia mji. Unatakiwa kujua wazazi wakikua wanahitaji kusimamiwa na sisi watoto wao.
Thread closed!🤝
 
Back
Top Bottom