Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.

Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.

Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.

Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.


Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.


Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.


Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.

Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.

Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.


NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Yupo na addiction ya mikopo yaani hapo hana tofauti na mcheza kamali..
Hapo kazi unayo ni kumuomba Mungu tu.. ila ata wakiuza nyumba bado ataendelea kukopa hukohuko kijijini anapokimbilia..

Mimi nakushauri fanya maisha yako hesabu una hasara kwa mzazi basi..
 
Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao , wakisikia mikopo wanajifunga vibwebwe mbio kwenye mikopo

Kwanini mikopo Iko milangoni kwasababu wakopeshaji ni matapeli wamegundua watu wengi hawajishughulishi wanao kopesha wanafurahia zaidi kuwakopesha wanawake

Mikopo kausha damu:
Hii mikopo inageuka mikopo kausha damu endapo maingizo yako ya Kila siku ama kwa mwezi hayawezi kuresha mikopo kwa muda husika

Mimi nimelifuatilia hili la mikopo kwa kina na Nina andiko lake nilidhani ni fursa y kuelimisha jamii elimu ya ujasiriamali, hiyo fursa haipo mifumo hairuhusu matapeli na wajuaji ni wengi
Liko wapi hilo andiko mkuu kama hutajali?
 
Mchukue uishi naye boss

Wanawake jinsi wanavyokua uwezo wao wa kufikiri hupungua kwa kasi

Inawezekana kuna mwamba amemteka mama anamtuma akope
Una point.

Huyu ni mtu kama sio wapili ni watatu nasikia analalamika mama yake kuzidiwa na mikopo. Kuna jamaa mmoja nafahamiana nae alinieleza kesi karibu kama hii hii kuhusu mama ake anakopa sana na anachofanya hakijulikani. Sema huyo jamaa yeye ana ka uwezo kwahiyo hua anamlipia lakini inachosha sana.

Kuna mwingine alinisimulia mama mkwe wake amekamatika kwa wauza madawa haya ya kienyeji kila siku anapigiwa simu atume hela akiuliza za nini anaambiwa za deni la dawa. Akidadisi zaidi mama anakua mkali inabidi atume tuu.

Ni changamoto hawa wamama.
 
Ni mama wa pekee na ni mtoto wa pekee, Lazima nguvu ya upendo iwepo kila upande, lipa madeni na ishi nae, then kuwa nae karibu kama biashara yako.
 
Vijana wengine sijui mmerogwa?? Baba yako ashafariki, nyumba, mashamba n.k vipo. Mama yako yupo mwenyewe na hana chochote cha maana anachofanya. Hakuna ndugu yeyote wa kukaa nyumbani na kulinda mali za familia. Wewe badala ya kurudi ukakaa nyumbani uongoze na kusimamia familia na vitega uchumi vilivyopo unakimbilia mjini kuuza genge, kupanga nyumba na kuishi kwa tabu. Tatizo ni wewe na si mama yako. Rudi kijijini simamia mji. Unatakiwa kujua wazazi wakikua wanahitaji kusimamiwa na sisi watoto wao.
 
Una point.

Huyu ni mtu kama sio wapili ni watatu nasikia analalamika mama yake kuzidiwa na mikopo. Kuna jamaa mmoja nafahamiana nae alinieleza kesi karibu kama hii hii kuhusu mama ake anakopa sana na anachofanya hakijulikani. Sema huyo jamaa yeye ana ka uwezo kwahiyo hua anamlipia lakini inachosha sana.

Kuna mwingine alinisimulia mama mkwe wake amekamatika kwa wauza madawa haya ya kienyeji kila siku anapigiwa simu atume hela akiuliza za nini anaambiwa za deni la dawa. Akidadisi zaidi mama anakua mkali inabidi atume tuu.

Ni changamoto hawa wamama.
Ndio boss mwanamke anahitaji mtu wa kumuongoza

Uwezo wao wa kufanya maamuzi hupungua kwa kasi Sana akikosa mume au watoto wa kumuongoza anapotea totally
 
Nimesoma maoni ya wadau wengi ni kama vile hawavai viatu vya uhusika wa jambo hili ndiyo maana wanaliparaza, wanashauri bila kuuvaa uhusika.

Maneno yafuatayo yanafikirisha sana: 'mwache', 'hasaidiki', 'nyumba iuzwe' nk nk.
Maneno ya namna hiyo yanafikirisha zaidi ya kushauri namna ya kupambana na changamoto iliyo mbele ya mleta mada.

Nadhani aanze tafakari kwa kutumia mfano ulio nje ya mfano wa mada hii.

Je leo hii angelisikia mama yake kalazwa kwa gonjwa kubwa linalohitaji matibabu nje ya nchi angelifanyaje na yeye hana kitu?

Je kwa kuwa hana kitu hawezi kumsaidia mama yake hata kwa kuwasiliana na kuwahusisha watu wengine ili kumsaidia mzazi wake?

Nimetolea mfano huu kurahisisha wananzengo kuuvaa uhusika ili kila mmoja aone kama tatizo la mtoa mada ni la kwake na si la mtu mwingine .

Mleta mada, tafuta nauli nenda kakutane na mama yako ana kwa ana uongee naye akueleze historia ya jambo hili, ili wewe utathimini ukubwa wake na namna ya kuanza nalo.

Ukiwa mbali bila kufika na kuonana naye, jambo hili litakusumbua, hautapata njia sahihi ya kudeal nalo.

Maana jambo linalomhusu mzazi wako nawe linakuhusu pia moja kwa moja, asiwe ni mzazi wako wa raha tu na inapopatikana shida ama matatizo unamkimbia.

Suala la kumuacha alimalize tatizo hili kubwa peke yake ambapo yeye limemshinda, ni sawa na kumtelekeza katika dhiki.

Kuuza nyumba liwe jambo la mwisho kabisa katika tafakari yenu ya kupata gharama za kulipa deni, kwa sababu, nyumba hiyo yaweza kuwa ni kitovu pekee kilichoshikilia uhai wako na wa mama yako, leo iuzwe wewe kwenu itakuwa ni wapi!

Lazima nikwambie, utakapokaa naye na kuongea naye kwa lugha ya unyenyekevu utakayoitumia, itafikia katika maelezo yake utagundua mbinu zozote zitakazo kusaidia angalau kupata pa kushika.

Vaa ujasiri wa kusaidia mzazi wako hata kwa mawazo na pia kushirikisha watu wengine utafanikiwa.

Natumaini Mungu atakutangulia, muhimu funga safari kwenda kuonana na mzazi wako ana kwa ana.
 
Yupo na addiction ya mikopo yaani hapo hana tofauti na mcheza kamali..
Hapo kazi unayo ni kumuomba Mungu tu.. ila ata wakiuza nyumba bado ataendelea kukopa hukohuko kijijini anapokimbilia..

Mimi nakushauri fanya maisha yako hesabu una hasara kwa mzazi basi..
Shida roho inaniuma sana naona kama atapata presha atafariki nachanganyikiwa mm
 
Liko wapi hilo andiko mkuu kama hutajali?
Ninalo cha ajabu fursa za mikopo zinakuja wakati uchaguzi unakaribia baada ya uchaguzi unaachwa uteseke hata hivyo hiyo mikopo imekaa kimitego mitego tu ni wachache tu wanaofaidika, wanaishi kwa matumaini Hadi uchaguzi unapita
 
Badili line acha kumtafuta kwa muda wa miezi sita. Ukizembea mkuu utakufa kwa msongo wa mawazo.
Yeye sindoatakufa maan nyumbn kakimbia anaishi mashambani uko anakula nn sasa anaish vip kupata magonjwa ya moyo
 
Vijana wengine sijui mmerogwa?? Baba yako ashafariki, nyumba, mashamba n.k vipo. Mama yako yupo mwenyewe na hana chochote cha maana anachofanya. Hakuna ndugu yeyote wa kukaa nyumbani na kulinda mali za familia. Wewe badala ya kurudi ukakaa nyumbani uongoze na kusimamia familia na vitega uchumi vilivyopo unakimbilia mjini kuuza genge, kupanga nyumba na kuishi kwa tabu. Tatizo ni wewe na si mama yako. Rudi kijijini simamia mji. Unatakiwa kujua wazazi wakikua wanahitaji kusimamiwa na sisi watoto wao.
Ata uyu mama alikuwa uku mjini pi alikopa ndo kakimbilia kijijin naiyo nyumba utaishi vip bila kuhangaika kutafuta riziki
 
Duh sina kazi mkuu kwann nijifiche mm nibinti napamban nikipt kazi pia nafanya
 
Back
Top Bottom