Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi

Dah inasikitisha sana sometime wazazi wanakera badala ya kuwa mfano mzuri kwa watoto wanakuwa mwiba mchungu!

Njia nzuri ya kukabili tatizo ni kulitatua fanya namna ulipe madeni yote hata kama ni kwa kuuza vitu au rehani. Madeni yaishe akirudia acha apambane mwenyewe.
Icho chakuuza kufika milioni ndo sina namimi binti najitafuta mamilioni kuyalipa siwezi labda Namimi niingie kwenye mikopo
 
Kasimamie uuzwaji wa hiyo nyumba mlipe madeni yote muanze upya ,akirudia tena muache tu apambane mwenyewe,ukimuendekeza hutopiga hatua kabisa
 
Ndio hivyo kaka maarifa muhimu mambo kama haya yanatokea hapa tunajifunza kuyatatua.
Dunia inaenda kasi sana tunahitaji maarifa kila siku changamoto kama hizi ningum sana hasa linapomhusisha mzazi
 
Icho chakuuza kufika milioni ndo sina namimi binti najitafuta mamilioni kuyalipa siwezi labda Namimi niingie kwenye mikopo
anha kumbe we binti, Pole sana dadaetu kiukweli ni changamoto, chakufanya mhimize mama aache hio tabia hata kama ukimwambia ananuna inabidi umwambie.

Kama kawakopa watu binafsi inabidi mkae na mama umwambie muwaite wadeni wenu, uwaombe wakupe muda ulipe polepole kuwa muwazi kwamba hali ni ngumu wakupe muda. Waite kando waambie wasimkopeshe mama tena kama inawezekana.
 
Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.

Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.

Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.

Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.


Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.


Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.


Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.

Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.

Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.


NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Pole sana mkuu. Kama mtu hajapitia hii hali, hawezi kukuelewa.
Pole sana. Ushauri, mwache aishi maisha anayoona yanamfaa. Sana sana utapata stress na utaendelea kuwa maskini, usiyeweza kujisaidia au kusaidia wengine.
 
Acha kujipa stress zisizo na kichwa wala miguu boss. Watu wanalia na wazazi wanaumwa magonjwa yasiyopona kila siku kuna bili za hospitali wewe unawehuka na mama anayekopesheka? Pambania maisha yako, mama akimaliza collateral zote ataacha kukopa.
 
Msijikute smart sana, watu wako kwenye matatizo unataka waanze kutafuta italic na times new roman? Pumbaf
Na wewe hebu ondoa ujinga wako... Babaako aliuza ng'ombe kisha akakupeleka ng'ombe wewe shule
 
Wanajamii, sijui nianze na kulia...
Natamani nipige ukunga watu wanisikie, wajue mpaka ndani mwangu navyoumia. Natamani nipate wa kumweleza huu uchungu wangu ninavyojisikia kwa sasa, lakini watanicheka. Sina dada, sina kaka, sina mdogo — nimezaliwa peke yangu.

Story ni hii...
Mama yangu ni mtu wa mikopo sana. Baada ya kufariki baba, hali imekuwa mbaya zaidi. Hata alipokuwa na baba, walishawahi kufilisiwa, lakini mzee alilipa. Sasa hana kipato wala biashara. Nilijaribu kulipa mikopo yake nikiwa Dar es Salaam wakati nasoma chuo, nikitumia boom na vibishara vidogo vidogo. Mpaka inafika muda mtaji unakata.

Alipozidiwa na mikopo, alikimbilia kijijini. Kumbe huko nako alianza kukopa. Haniambii, lakini utasikia leo, “naumwa,” sijui “nitumie kiasi fulani.” Mimi natuma kama ninayo.

Hali yangu kwa sasa...
Sina kazi. Mjini nina kigenge kidogo ndiyo napambana nacho. Lakini hakikui mpaka leo. Aliyeniona mwaka jana na mwaka huu, niko vilevile. Siwezi kunywa hata soda.


Kitu kinachoniumiza zaidi leo ni hiki...
Wanajamii, naomba hata ushauri. Huu mkopo mpya aliouchukua mwezi wa kumi na mbili (Desemba) kutoka kampuni mbili tofauti: mmoja ni Black — milioni 1 na laki 4, mwingine ni milioni moja. Kila wiki anatakiwa kurejesha. Na sijui amefanyia nini hizo pesa. Nyumbani kwetu kijijini hakuna kitu zaidi ya kitanda na godoro tu.


Watu wa mikopo wamekuja nyumbani kutaka kuuza nyumba aliyoweka rehani. Yeye amekimbia — siku ya tatu sasa hapatikani. Inavyosemekana, hayupo kijijini, amekimbilia mashambani. Jana alinipigia kwa namba nyingine, kuniambia anaumwa sana miguu, hawezi kutembea. Nikatuma elfu 20 aende hospitali — kumbe alinipiga kizinga.


Hali yangu ni mbaya...
Sina maisha. Najitafuta tu. Nimepanga. Niko peke yangu. Sina hata wa kumweleza au kushauriana naye. Ningekuwa na hata kaka, tungepigiana simu.

Wanajamii, naombeni tu mawazo yenu:
Nifanyeje ili aache hii tabia ya mikopo na kulipa haya madeni?
Uwezo sina. Napambana na maisha ya mjini lakini siendelei. Niliyoumizwa moyoni. Naomba sana kwa Mungu, lakini sijui kwa nini habadiliki.

Nishaurini nifanye nini. Akili imefika mwisho sasa.
Ningekuwa na pakulilia, ningeenda nilie uchungu uishe — ila sina.
Hata rafiki sina, naogopa kumwambia — hii ni aibu sana.


NB: Ukimuuliza kuhusu mikopo yake, anakasirika, mnagombana, na simu hapigi tena.
Naombeni msaada — hata wa mawazo. Nifanye nini? Sina amani tena toka nipigiwe simu kupewa hizi habari.
Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao , wakisikia mikopo wanajifunga vibwebwe mbio kwenye mikopo

Kwanini mikopo Iko milangoni kwasababu wakopeshaji ni matapeli wamegundua watu wengi hawajishughulishi wanao kopesha wanafurahia zaidi kuwakopesha wanawake, kumbe wanawake ni rahisi kupata pesa za marejesho sitakii kuzama sana kwenye hili

Mikopo kausha damu:
Hii mikopo inageuka mikopo kausha damu endapo maingizo yako ya Kila siku ama kwa mwezi hayawezeshi kuresha mikopo kwa muda husika

Mimi nimelifuatilia hili la mikopo kwa kina na Nina andiko lake nilidhani ni fursa y kuelimisha jamii elimu ya ujasiriamali, hiyo fursa haipo mifumo hairuhusu matapeli na wajuaji ni wengi, (unworking government machineries)

Mikopo hudumaza akili watu wengi wanajihusisha na mikopo kwasababu ya uoga wa kukabiliana na wanao wadai pia watanzania ni masikini hawana miradi inayo wezesha kumudu maisha, (to afford life) la mwisho tamaa

Mikopo huwezesha kutatua matatizo kwa haraka, kama una biashara yenye mtiririko unaweza kopa, kumbe mikopo huwafanya watu wawe na nidhamu ya matumizi ya pesa, mikopo inaongeza uwezo wa kufikiri na kipato

Hitimisho tukope endapo mtiririko wa pesa mifukoni mwetu uko vizuri, mikopo hukimbiza watu kwenye familia zao wengi wamezikimbia familia zao kwasababu ya mikopo
 
Umenikumbusha nilimwambia mama wakati huo mimi sitaweza kumsaidia ngoja nijaribu kupambana ili mbele yasafari akikosa nguvu zakujipambania nimsaidie bahati mbaya mpaka leo bado sijatoboa mkuu achana nae ukiendelea huyo mama mwisho utakata tamaa yakuishi
Inahuzunisha sana mama angu sijui anashida gani ananiweka kundi gani binti yake roho inaniuma saana
 
Pole kwa chnagmoto unayopitia.

Nimepangialia andiko lako, ili kuwarahisishia wadau wengine:

---
Hali Yangu ya Sasa na Uchungu Moyoni

Wanajamii, sijui hata nianze vipi, natamani kulia na kupiga ukunga ili wote mjue jinsi ninavyoumia ndani kwa ndani. Uchungu nilionao ni mkubwa na ninatamani kupata mtu wa kumueleza, lakini nahofia kuchekwa. Sina kaka, dada, wala mdogo; nimezaliwa peke yangu. Hii hali imeninyima amani kabisa, nina maumivu makali moyoni na nahisi aibu kubwa hata kuwaeleza marafiki. Kama kungekuwa mahali pa kulilia, ningekwenda ili huu uchungu uishe.

Tatizo Sugu la Mikopo ya Mama

Kiini cha haya yote ni mama yangu kuwa na tabia ya kukopa kupita kiasi. Hali hii ilizidi baada ya baba kufariki, ingawa hata awali aliwahi kufilisiwa na baba akalazimika kulipa madeni yake. Alipoelemewa na madeni Dar es Salaam, alikimbilia kijijini, lakini kumbe na huko aliendelea na tabia hiyo ya kukopa bila hata kunijulisha. Mara nyingi huniambia anaumwa ili nimtumie pesa, nami kama ninayo huwa natuma.

Mkopo Mpya na Tishio la Kupoteza Nyumba

Kilichonisukuma kuwaandikia leo ni kuhusu mikopo mipya aliyoichukua Desemba kutoka kampuni mbili tofauti: moja ya Shilingi milioni 1.4 na nyingine ya Shilingi milioni 1, ambazo anatakiwa kurejesha kila wiki. Pesa hizi sijui hata alizifanyia nini maana nyumbani kijijini hakuna chochote cha maana zaidi ya kitanda na godoro. Watu wa mikopo walifika nyumbani wakitaka kuiuza nyumba aliyoiweka rehani. Kutokana na hilo, mama amekimbia (leo ni siku ya tatu) na hapatikani kwenye simu yake; inasemekana amekimbilia mashambani. Jana alifanikiwa kunipigia kwa namba ngeni akidai anaumwa sana miguu hawezi kutembea, nikamtumia Shilingi 20,000 kwa ajili ya matibabu, kumbe ilikuwa ni njia yake ya kunipiga kizinga tu.

Changamoto Zangu Binafsi za Kimaisha na Kipato

Mimi mwenyewe hali yangu si nzuri. Nilijitahidi kulipa baadhi ya madeni yake nikiwa chuo kwa kutumia pesa ya 'boom' na faida ya vibiashara vidogo nilivyokuwa nafanya, lakini mtaji uliisha. Kwa sasa sina kazi rasmi, nina kigenge kidogo tu ambacho napambana nacho lakini hakikui; hali yangu ni ileile kila mwaka, hata kunywa soda ni anasa. Ninaishi peke yangu katika chumba cha kupanga, napambana na ugumu wa maisha ya mjini lakini sioni maendeleo. Uwezo wa kulipa haya madeni mapya sina kabisa.

Changamoto ya Mawasiliano na Mama Kuhusu Madeni

Pia, kuna changamoto kubwa ya mawasiliano. Nikijaribu kumuuliza kuhusu mikopo yake, huwa mkali sana, tunaishia kugombana na anaweza kukata mawasiliano kabisa kwa kutokupiga simu.

Ombi la Ushauri: Nifanye Nini?

Wanajamii wapendwa, nimefika mwisho wa akili. Naomba sana msaada wenu wa mawazo: Nifanye nini ili kumsaidia mama aache hii tabia ya mikopo? Na nitawezaje kukabiliana na haya madeni mapya wakati uwezo wangu ni mdogo? Nimekuwa nikimuombea sana abadilike, lakini hali bado ni ileile. Nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya. Tafadhali nishaurini.
Shukrani
 
Duu pole sana hili tatizo siyo la mama yk peke Yako ni janga la kitaifa la akina mama wengi wa kitanzania wameathirika na mikopo, hii mikopo ipo milangoni mwao

Kwanini mikopo Iko milangoni kwasababu wakopeshaji ni matapeli wamegundua watu wengi yajishughulishi wanao kopesha wanafurahia zaidi kuwakopesha wanawake
Yah ni kweli kabisa usemacho,kuna wa baba wengi wamekubwa na mfadhaiko wa akili sababu ya madeni ya wake zao yasiyoisha.
 
Inaumiza sana mkuu pole sana nasikitika kukwambia mama yako kashakuwa mraibu wa mikopo.

Huwezi kufukia shimo kwa kuendelea kulichimba, anachokifanya mama yako ni kutaka kufukia shimo wakati bado yupo ndani anaendelea kuchimba mwishowe itashindikana kabisa kutoka shimoni. Acha nyumba iuzwe ajifunze japo mtu kama huyo ni wakuwa nae makini sana.
 
Mchukue uishi naye boss

Wanawake jinsi wanavyokua uwezo wao wa kufikiri hupungua kwa kasi

Inawezekana kuna mwamba amemteka mama anamtuma akope
 
Huu mwandiko sio wa muuza genge,wewe ni msomi na una kazi nzuri tu,kuwa wazi hatukurogi
 
Pole mkuu
Ni ngumu kuuchukua ushauri mgumu wa kumkacha maza mimi naona cha kufanya ni wewe kufatilia hayo madeni makubwa yamefikia wapi, pata details zote.

Kama mama huwa anakutafuta kwa uficho basi siku akikutafuta, tenga nae muda ujue yeye kajipanga vipi kuilipa hiyo mikopo na kama yupo tayari kuruhusu nyumba iuzwe.

Mueleze hali yako halisi kiuchumi kua hutoweza kumudu kumlipia/kupata hela za vizinga vyake.
 
Back
Top Bottom