Mamba asingewekwa kwenye kundi la Super Predator hastaili kabisa

Mamba asingewekwa kwenye kundi la Super Predator hastaili kabisa

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka wanajamvi!

Mamba hakidhi vigezo vya kuitwa au kuwa Super Predator. Kwa mtazamo wangu hastaili kuwa kabisa kwenye Hilo kundi la Super predator.

Wanyama wengine ambao wako kwenye Hilo kundi Simba, Chui, Duma, Mbwa mwitu na Fisi wanastahili sifa zote na wanakidhi vigezo.

Licha ya uhodari wa Mamba, nguvu, kuogopwa, ukubwa wa mwili ushupavu na nguvu zote anazo anavyowinda na kutwaa windo Bado tu ni mchumbaaa kwasababu ANATAGA.
 
Mazingira anayoishi Jaguar hakuna Mamba. Wale unaoona akiwakamata kwenye maji wanaitwa Caiman ambao uzito wao maximum ni 40kgs. Ingekuwa Nile crocodile Jaguar asingewezana naye lile monster linafika hadi kilo 500 uzito
Hivyo vyenye kilo 40 vikiwa kwenye maji vinakuwa na pulling ya nguvu kuliko hata volkswagen amarok
 
Kuna mwamba anaitwa jaguar, anafuta mamba kumayi na kumburuta
Huwa wanatafuna vile vi-cayman au alligators vya America na Asia. Ila sio African crocodile. Huyu kiumbe ni habari nyingine!

Kila kiumbe kinachoishi Africa kimevurugwa. Kuna documentary moja niliona simba aliingia mtoni kwa kiburi chake akajua jamaa hawamuwezi. Alinusurika ila akabaki taya linaning'inia, akaenda kufia mbele huko!
 
Upo sahihi, viumbe vya Africa vyote vimevurugwa, kuna kuku ana vifaranga Leo kanirukia aniparue bila kosa lolote.
 
Huwa wanatafuna vile vi-cayman au alligators vya America na Asia. Ila sio African crocodile. Huyu kiumbe ni habari nyingine!

Kila kiumbe kinachoishi Africa kimevurugwa. Kuna documentary moja niliona simba aliingia mtoni kwa kiburi chake akajua jamaa hawamuwezi. Alinusurika ila akabaki taya linaning'inia, akaenda kufia mbele huko!
Bado Simba alionyesha umwamba tu kutoka hai
 
Hakuna mamba anayetolewa kumayi na Jaguar. Hao unaowasema ni jamii ya mamba. Si mamba Crocodile. Mamba ana ndugu zake wengi tu watoto wa mjomba na shangazi ila yeye kama yeye mwambie yoyote amfate kumtoa Kumayi... Hakuna
Mamba hana cha kumfanya Simba labda amuotee sana.
Yani Simba anambonda ndugu Mamba home and away
 
Back
Top Bottom