KWELI Mamba (Gustave) anakadiriwa kuua watu takribani 300 Ziwa Tangayika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
 
Tunachokijua
Mamba ni reptilia wakubwa wenye ngozi ngumu wanaoishi kando na ndani ya mito, mabwawa na maziwa na wanatofautiana urefu na uzito kati ya aina moja na nyingine lakini inakadiriwa wanaweza kuishi hadi miaka 75 huku wakifikisha urefu wa futi 20.

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa Mamba Gustave ambaye ni mamba aina ya Nile ameandikwa katika machapisho mbalimbali ikiwemo hapa, hapa na hapa akielezewa kuwa ni miongoni mwa mamba wakubwa kuwahi kutokea barani Afrika huku akihusishwa na ulaji wa binadamu takribani 300 wakazi Burundi upande wa kaskazini mwa ziwa Tanganyika na mto Rusizi/Ruzizi. kwa mujibu wa National geographic (2009) inaaminika kuwa mamba Gustave alianza kuua watu kuanzia mwaka 1987.

Tovuti ya Dinoanimals wanaeleza kuwa kuna madai kwamba Gustave alikuwa anaua watu si kwa ajili ya chakula tu bali pia kwa ajili ya kujifurahisha na baada ya kufanya hivyo hupotea kwa takribani miezi kadhaa kabla ya kuibukia sehemu nyingine. Dinoanimals wanaeleza pia kuwa Gustave alikuwa na makovu tofauti tofauti ikiwemo ya risasi yaliyosababishwa na waliokuwa wakimuwinda ingawa majaribio yote yalishindwa kufanikiwa kumuua. Mamba Gustave anakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilogram 900 na urefu wa kati ya futi 20 na futi 24, anatajwa kuwa na ukubwa mara tatu zaidi ya Mamba wa kawaida nchini Burundi.

Gustave alitambuliwa na kupewa jina hilo na Patrice Faye ambaye ni mtaalamu wa Amphibia na Reptilia, tovuti ya Dinoanimals inaeleza kuwa Gustave aliwindwa na watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kumuua lakini Faye pekee ndiye aliyehitaji kumpata Gustave akiwa mzima ili akamuhifadhi sehemu ambayo hatoleta athari kwa binadamu ili awe mbegu kwa mamba wengine wa aina yake. Faye alianza kufanya utafiti kuhusu Gustave kuanzia miaka ya 1990 na mwaka 2004 akatoa makala ya video kumuhusu Gustave iliyojulikana kwa jina la Capturing the killer croc.

Tovuti mbalimbali ikiwemo Rapusia zinaonesha kuwa Gustave alionekana kwa mara ya mwisho kati ya 2015 na 2016 akidhaniwa kuwa na miaka 75 huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama ameshafariki ama yupo eneo lingine. Ingawa inakadiriwa kuwa mamba Gustave ameua watu 300 lakini hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuwa mamba huyo aliua idadi hiyo ya watu.

Kwa kuwa ziwa Tanganyika linapatikana pia nchini Tanzania JamiiCheck imewasilia na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia kwa afisa habari wao Beatus Maganja ambaye amesema kwa Tanzania hakuna tukio lilirekodiwa kufanywa na mamba Gustave na kama matukio haya yangekuwepo basi mamba huyo angedhibitiwa

“Taarifa za huyo mamba mimi sizijui na bado hatujapata taarifa za tukio la mamba wa aina hiyo’’
Hivi kama hawajamkamata wamewezaje kumpima vipimo vyote hivyo hadi kujua uzito wake in details kabisa tena in decimal places?

By the way, kwanini umeamua kusema ni Tanzania wakati citing yako mwenyewe inataja Burundi? Ndio uzalendo uliobobea kuipenda nchi yako au?
 
Wikipedia inasema ni Burundi badala ya Tanzania
 
Itakuwa Ziwa Tanga yika limepanuka na kufika Burundi yaani🤔

Halafu Kigoma Jina Gustav halina maana yoyote, labda Mwami!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…