KWELI Mamba (Gustave) anakadiriwa kuua watu takribani 300 Ziwa Tangayika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
FB_IMG_17281825575769347.jpg

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
 
Tunachokijua
Mamba ni reptilia wakubwa wenye ngozi ngumu wanaoishi kando na ndani ya mito, mabwawa na maziwa na wanatofautiana urefu na uzito kati ya aina moja na nyingine lakini inakadiriwa wanaweza kuishi hadi miaka 75 huku wakifikisha urefu wa futi 20.

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa Mamba Gustave ambaye ni mamba aina ya Nile ameandikwa katika machapisho mbalimbali ikiwemo hapa, hapa na hapa akielezewa kuwa ni miongoni mwa mamba wakubwa kuwahi kutokea barani Afrika huku akihusishwa na ulaji wa binadamu takribani 300 wakazi Burundi upande wa kaskazini mwa ziwa Tanganyika na mto Rusizi/Ruzizi. kwa mujibu wa National geographic (2009) inaaminika kuwa mamba Gustave alianza kuua watu kuanzia mwaka 1987.

Tovuti ya Dinoanimals wanaeleza kuwa kuna madai kwamba Gustave alikuwa anaua watu si kwa ajili ya chakula tu bali pia kwa ajili ya kujifurahisha na baada ya kufanya hivyo hupotea kwa takribani miezi kadhaa kabla ya kuibukia sehemu nyingine. Dinoanimals wanaeleza pia kuwa Gustave alikuwa na makovu tofauti tofauti ikiwemo ya risasi yaliyosababishwa na waliokuwa wakimuwinda ingawa majaribio yote yalishindwa kufanikiwa kumuua. Mamba Gustave anakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilogram 900 na urefu wa kati ya futi 20 na futi 24, anatajwa kuwa na ukubwa mara tatu zaidi ya Mamba wa kawaida nchini Burundi.

Gustave alitambuliwa na kupewa jina hilo na Patrice Faye ambaye ni mtaalamu wa Amphibia na Reptilia, tovuti ya Dinoanimals inaeleza kuwa Gustave aliwindwa na watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kumuua lakini Faye pekee ndiye aliyehitaji kumpata Gustave akiwa mzima ili akamuhifadhi sehemu ambayo hatoleta athari kwa binadamu ili awe mbegu kwa mamba wengine wa aina yake. Faye alianza kufanya utafiti kuhusu Gustave kuanzia miaka ya 1990 na mwaka 2004 akatoa makala ya video kumuhusu Gustave iliyojulikana kwa jina la Capturing the killer croc.

Tovuti mbalimbali ikiwemo Rapusia zinaonesha kuwa Gustave alionekana kwa mara ya mwisho kati ya 2015 na 2016 akidhaniwa kuwa na miaka 75 huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama ameshafariki ama yupo eneo lingine. Ingawa inakadiriwa kuwa mamba Gustave ameua watu 300 lakini hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuwa mamba huyo aliua idadi hiyo ya watu.

Kwa kuwa ziwa Tanganyika linapatikana pia nchini Tanzania JamiiCheck imewasilia na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia kwa afisa habari wao Beatus Maganja ambaye amesema kwa Tanzania hakuna tukio lilirekodiwa kufanywa na mamba Gustave na kama matukio haya yangekuwepo basi mamba huyo angedhibitiwa

“Taarifa za huyo mamba mimi sizijui na bado hatujapata taarifa za tukio la mamba wa aina hiyo’’
amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.
Huyo aliyekwenda kumpima urefu na uzito alishindwa nini kwenda na bunduki akamuua
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
Mamba kumkamata tembo???!!

☕🍵
 
Hilo jina la huyo mamba GUSTAVE ni mamba aliye sumbua nchin Burundi miaka 90s na sio Tz.Lakn pia matukio ya mamba kuua watu mkoa wa kigoma yako vijij vya kusin mwa mji wa kigoma kuanzia Ilagala na maeneo jirani,sunuka,Lubengera,kapara mpaka huko Lukoma,katumbi mpakan na Hifadhi ya Milima mahale.Tena maeneo hayo huathiriwa saana kwakuw mamba huvinjari ktk mito mikubwa inayo mwaga maji ziwa Tanganyika huo upande wa huo wa kusin kama vile mto Lwiche na Malagarasi.
Kwa upande wa kaskzin mwa mji wa Kigoma (uelekeo wa burund) kuna misim michache saana ambayo vboko na mamba wanaotoka burund huwa wanafka mpaka maeneo ya hifadhi ya taifa Gombe(km 24 kutoka kgoma mjini) hata hivyo ni nadra saana kuwa na matukio ya watu kushambuliw na mamba au vboko.Vijij viilvyoko within 24 km yaaan kati Hifadh ya Gombe na Kigoma mjin ambavyo ni Mtanga,kagongo migazin/ziwan na Kigarye hiv huwez ckia taarfa za kuonekana kwa hao viumbe.Na ikitokea ujue JW huwa wanakula nao sahan moja coz ktk orodha ya wanyama walioko hifadh ya Gombe mamba hawamo kbsaa,kwahyo wanapo onekana maeneo huleta taharuki mno coz sio ktu kilicho zoeleka ktk hayo maeneo.
HITIMISHO:
Hizo taarfa za Gustave na mkoa wa kigoma ni mpya kwangu labda kama ni huko kijij cha KAGUNGA ambacho kiko mpakan kbsaa na Burund,amabacho najua JW wangekuw washa mshusha ktambo maana cna hakika kama wanaeza subiria TANAPA ukzngatia hao viumbe wanatokea nchi jirani.
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Huu utambuzi wa uzito wa kilo 907 umepatikanaje!!?
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.
wamejuaje kuwa watu hao wote wameuawa na huyo Mamba mmoja?
Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika.
Kama hawajawahi kumkamata wamewezaje kumpima?
Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k.
Tembo?? Kiboko??? Una maanisha watoto wa Tembo na Viboko?
Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Kama wameweza kumpiga picha, wakaweza kumpima urefu na uzito maana yake hawajashindwa kumuua.
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania

Hadi urefu na uzito akapimwa ila imeshindikana kumpata ....
 
Back
Top Bottom