KWELI Mamba (Gustave) anakadiriwa kuua watu takribani 300 Ziwa Tangayika

KWELI Mamba (Gustave) anakadiriwa kuua watu takribani 300 Ziwa Tangayika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
FB_IMG_17281825575769347.jpg

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
 
Tunachokijua
Mamba ni reptilia wakubwa wenye ngozi ngumu wanaoishi kando na ndani ya mito, mabwawa na maziwa na wanatofautiana urefu na uzito kati ya aina moja na nyingine lakini inakadiriwa wanaweza kuishi hadi miaka 75 huku wakifikisha urefu wa futi 20.

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa Mamba Gustave ambaye ni mamba aina ya Nile ameandikwa katika machapisho mbalimbali ikiwemo hapa, hapa na hapa akielezewa kuwa ni miongoni mwa mamba wakubwa kuwahi kutokea barani Afrika huku akihusishwa na ulaji wa binadamu takribani 300 wakazi Burundi upande wa kaskazini mwa ziwa Tanganyika na mto Rusizi/Ruzizi. kwa mujibu wa National geographic (2009) inaaminika kuwa mamba Gustave alianza kuua watu kuanzia mwaka 1987.

Tovuti ya Dinoanimals wanaeleza kuwa kuna madai kwamba Gustave alikuwa anaua watu si kwa ajili ya chakula tu bali pia kwa ajili ya kujifurahisha na baada ya kufanya hivyo hupotea kwa takribani miezi kadhaa kabla ya kuibukia sehemu nyingine. Dinoanimals wanaeleza pia kuwa Gustave alikuwa na makovu tofauti tofauti ikiwemo ya risasi yaliyosababishwa na waliokuwa wakimuwinda ingawa majaribio yote yalishindwa kufanikiwa kumuua. Mamba Gustave anakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilogram 900 na urefu wa kati ya futi 20 na futi 24, anatajwa kuwa na ukubwa mara tatu zaidi ya Mamba wa kawaida nchini Burundi.

Gustave alitambuliwa na kupewa jina hilo na Patrice Faye ambaye ni mtaalamu wa Amphibia na Reptilia, tovuti ya Dinoanimals inaeleza kuwa Gustave aliwindwa na watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji kumuua lakini Faye pekee ndiye aliyehitaji kumpata Gustave akiwa mzima ili akamuhifadhi sehemu ambayo hatoleta athari kwa binadamu ili awe mbegu kwa mamba wengine wa aina yake. Faye alianza kufanya utafiti kuhusu Gustave kuanzia miaka ya 1990 na mwaka 2004 akatoa makala ya video kumuhusu Gustave iliyojulikana kwa jina la Capturing the killer croc.

Tovuti mbalimbali ikiwemo Rapusia zinaonesha kuwa Gustave alionekana kwa mara ya mwisho kati ya 2015 na 2016 akidhaniwa kuwa na miaka 75 huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama ameshafariki ama yupo eneo lingine. Ingawa inakadiriwa kuwa mamba Gustave ameua watu 300 lakini hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuwa mamba huyo aliua idadi hiyo ya watu.

Kwa kuwa ziwa Tanganyika linapatikana pia nchini Tanzania JamiiCheck imewasilia na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) kupitia kwa afisa habari wao Beatus Maganja ambaye amesema kwa Tanzania hakuna tukio lilirekodiwa kufanywa na mamba Gustave na kama matukio haya yangekuwepo basi mamba huyo angedhibitiwa

“Taarifa za huyo mamba mimi sizijui na bado hatujapata taarifa za tukio la mamba wa aina hiyo’’
Basi nimeshaelewa kwanini Uhamiaji wanawakazia sana wanapotaka kupatiwa passport
Naona wazee wa zamani walitokea Kigoma ya Burundi wwlipokuja huku wakasema tumetokea Kigoma basi na hii ya kwetu ndio ikazaliwa kwa jina hili
Nimewaza tu labda yule mzee wa Historia anaweza kutusaidia
Ila kila kitu kinawezekana maana dunia ilikuwa moja ikakatwa katwa tu kwa ramani
 
Unamaanisha watu wa Kigoma ni watu kutoka Burundi si ndio?
 
Unamaanisha watu wa Kigoma ni watu kutoka Burundi si ndio?
We lianzishe tu maana kwa ubishi hawajambo
Nilipanda treni kutoka Kgm mpaka Tbr walibishana mpaka safari inaisha kuhusu dagaa wa wapi watamu kigoma au mwanza
Sasa mimi sina ubavu wa kubishana
 
We lianzishe tu maana kwa ubishi hawajambo
Nilipanda treni kutoka Kgm mpaka Tbr walibishana mpaka safari inaisha kuhusu dagaa wa wapi watamu kigoma au mwanza
Sasa mimi sina ubavu wa kubishana
Watu wa Kigoma ni wa Burundi?
 
Kama mnania ya kumuua semeni dawazipo anaitwa anajitokeza akiwa na hasira zote , anatulizwa kwa maneno anapigwa risasi ..semeni mnataka iwaje
 
Mamba ana mita 6 yaani zaidi ya futi 15?
HAIWEZEKANI KABISA.
 
Wanaohoji vipimo vya huyo mamba wa kufikirika, huwa mnaangalia Natgeo wild kweli?. Mbona kupitia zile picha, huwa wanawapima wanyama kwa vipimo mbalimbali hadi speed zao wakiwa wanakipimbia.
 
Wabongo hatujui vitu vingi sana ambavyo vipo tu.

Huyo mamba ameua watu wengi zaidi Burundi kuliko Tz. Inaaminiwa amekua akitegemea zaidi kuwinda binadamu kwakua alipata jeraha linalomfanya ashindwe winda natural preys.

Mara ya kwanza najua kuhusu Gustav nilitazama filamu inaitwa Primeval
 
Nakumbuka kuna kiboko alisumbua sana mtoni miaka ya 90 kijijini kwetu huko ,usiku anatoka mtoni anaenda kwenye mashamba ya viazi ni kutifua shamba zima , baadae akaua watu wawili hawa walikua walevi inasemekana walipomuona walijua ni ndama😅😅

Basi alikuja mzee mmoja mtaalam akafanya mambo yake kisha akatupia unga unga fulani humo mtoni ,

Baada ya kama nusu saa dubwana likaibuka lina hasira balaa mzee akalitupia maji fulani hivi likapoa kama nguruwe kaona miwa hapo hapo wandewa wakalishindilia masasi ya kutosha na ndio siku ya kwanza kula kiboko choma🤣
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
Atakua na vinasaba vya CCM huyu
 
Hivi kama hawajamkamata wamewezaje kumpima vipimo vyote hivyo hadi kujua uzito wake in details kabisa tena in decimal places?

By the way, kwanini umeamua kusema ni Tanzania wakati citing yako mwenyewe inataja Burundi? Ndio uzalendo uliobobea kuipenda nchi yako au?
Unaishi dunia ipi? Tech sikuhizi kama unaamini wachimba gas wakisema wamegundua ujazo wa gas ardhini trillion kadhaa na wakawekeza miaka kibao gas hauishi na ikiisha hesabu zao unakuta ni kweli.. tech ipo juu kuna vitu tu ikitizama inapima inajua hata kama umekula mihogo inajua uzito wako ukishaenda choo
 
View attachment 3116460

Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio.

Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu na tayari leo October 5 wamechapisha katika mtandao wa Wikipedia.

Picha ya Gustave imepigwa na 'Martin Best' wa National Geographic Society.
Unaweza kusoma tukio hili kwa urefu zaidi: Gustave (crocodile) - Wikipedia
Maajabu ya Lake Tanganyika.

Kwa hisani ya Kigoma Region Tanzania
Nani kampa hilo jina la gustav
 
Back
Top Bottom