Mamba waonekana Bwawa la Chemka

Mamba waonekana Bwawa la Chemka

Acha kuongea ujinga wewe kampuni ya African Queen mgeni wake alishashambuliwa na mambo hapo,hata Tanzania Specialist….

Hao wanaosema hakuna wanafaidika na hiyo sehemu lakin ukweli ni kwamba Mamba Chemka wapo..
Inasikitisha sana mkuu

Lini matukio haya yalitokea
 
JF team nimekutana na hii habari kwenye whatsap, naomba kwa mtu aliye karibu na maeneo ya huko Chemka atuambie kama ni kweli au ni uzushi? Naambatanisha na video na huo ujumbe unaozunguka

Kinga ni bora kuliko tiba. Hapa ni Chemka kule boma ng’ombe. Sehemu pendwa kwa kuogelea na natural Massage. Tahadhari imetolewa, Bwawa limeingia ruba. Mashuhuda wanasema Mamba wameonekana. Inaaminika Mamba hao wametokea mto Pangani.

Sababu zilizowawezesha Mamba hao kusafiri umbali mrefu inaaminika ni mvua zilizofululiza muda mrefu na mafuriko yaliyoanza Novemba mwaka jana yakaungana na mvua za masika za mwaka huu.

View attachment 2966676
Apo nishaogelea nipatamu Sana na nilikuwa nataman niende siku moja na beby wangu lakin duh.
 
Chemka hotspring
Nisaideni nikiwa Moshi Arusha highway unaingilia wapi kueleka huko? Na ni kilomita ngapi kutoka barabara kuu kufika huko? Je njia ya kufika huko inapitika kwa mwaka mzima kwa gari ndogo amabayo haina fourwheel? Nataka kufanya utalii wa ndani huko baadaye mwaka huu.
 
Ukifika Bomang'ombe uliza hata mtoto wa shule barabara ya kwenda Chemka utaoneshwa.
Nadhani around 15KM one way.
Karibu sana uogelee maji huku ukipata free massage ya samaki wadogo.
NB: Uje na nguo za kuogelea sio dela kwa mkeo/mpenzi.
 
Ubarikiwe. Vipi barabara ni lami, changarawe au vumbi na je inapitika kwa gari ndogo muda wote wa mwaka?
 
Ubarikiwe. Vipi barabara ni lami, changarawe au vumbi na je inapitika kwa gari ndogo muda wote wa mwaka?
Changarawe,inapitika mwaka mzima ila kipindi hiki cha mvua ni changamoto kwa baadhi ya maeneo.
Unaweza kwenda hata na Bajaji.
Kila la heri.
 
Najiepusha na mabishano na mtu wa sampuli yako, mabadiliko yakitokea ni kukubaliana nayo. Wewe kabembee na ile kamba oga kwa starehe sio lazima uliwe leo, sikio la kufa.....
Mamba pale wanakuja wakitokea mto Mbuguni, 2006 kuna mzungu alishambuliwa na mamba akafa akiwa anatibiwa nje. Meno ya mamba yana sumu kali sana
 
mamba wapo, ni issue inayofahamika vizuri tu sema huwa wanakuja usiku. Mchana kukiwa na vurugu vurugu na mishemishe za watu wakiogelea huwa wanaenda mbali hawawezi kusogea, ndyo hali inayosababisha kuonekana kama hawapo, lakini usiku kunapokuwa kumetulia wanarudi na ni risk sana kuogelea mwenyewe usiku.
Ndugu haufahamu vizuri tabia za mamba. Hilo dude la hovyo sana likiwa na njaa halina aibu wala nini. Likizidiwa na njaa linakamata binadamu hata nje ya maji japo nje ya maji ni mara chache sana na linakuwa halina nguvu sana kama linapokuwa ndani ya maji. Kama kweli mamba ameonekana wajulisheni askari wanyamapori wao ndio wanajua jinsi ya kuwawinda na kuwamaliza ili watu waendelee na shughuli za kibinadamu hapo kwenye hilo bwawa.
 
Back
Top Bottom