Mamba waonekana Bwawa la Chemka

Acha kuongea ujinga wewe kampuni ya African Queen mgeni wake alishashambuliwa na mambo hapo,hata Tanzania Specialist….

Hao wanaosema hakuna wanafaidika na hiyo sehemu lakin ukweli ni kwamba Mamba Chemka wapo..
Inasikitisha sana mkuu


Lini matukio haya yalitokea
 
Apo nishaogelea nipatamu Sana na nilikuwa nataman niende siku moja na beby wangu lakin duh.
 
Chemka hotspring
Nisaideni nikiwa Moshi Arusha highway unaingilia wapi kueleka huko? Na ni kilomita ngapi kutoka barabara kuu kufika huko? Je njia ya kufika huko inapitika kwa mwaka mzima kwa gari ndogo amabayo haina fourwheel? Nataka kufanya utalii wa ndani huko baadaye mwaka huu.
 
Ukifika Bomang'ombe uliza hata mtoto wa shule barabara ya kwenda Chemka utaoneshwa.
Nadhani around 15KM one way.
Karibu sana uogelee maji huku ukipata free massage ya samaki wadogo.
NB: Uje na nguo za kuogelea sio dela kwa mkeo/mpenzi.
 
Ukifika Bomang'ombe uliza hata mtoto wa shule barabara ya kwenda Chemka utaoneshwa.
Nadhani around 15KM one way.
Karibu sana uogelee maji huku ukipata free massage ya samaki wadogo.
NB: Uje na nguo za kuogelea sio dela kwa mkeo/mpenzi.
Ubarikiwe. Vipi barabara ni lami, changarawe au vumbi na je inapitika kwa gari ndogo muda wote wa mwaka?
 
Ubarikiwe. Vipi barabara ni lami, changarawe au vumbi na je inapitika kwa gari ndogo muda wote wa mwaka?
Changarawe,inapitika mwaka mzima ila kipindi hiki cha mvua ni changamoto kwa baadhi ya maeneo.
Unaweza kwenda hata na Bajaji.
Kila la heri.
 
Najiepusha na mabishano na mtu wa sampuli yako, mabadiliko yakitokea ni kukubaliana nayo. Wewe kabembee na ile kamba oga kwa starehe sio lazima uliwe leo, sikio la kufa.....
Mamba pale wanakuja wakitokea mto Mbuguni, 2006 kuna mzungu alishambuliwa na mamba akafa akiwa anatibiwa nje. Meno ya mamba yana sumu kali sana
 
Ndugu haufahamu vizuri tabia za mamba. Hilo dude la hovyo sana likiwa na njaa halina aibu wala nini. Likizidiwa na njaa linakamata binadamu hata nje ya maji japo nje ya maji ni mara chache sana na linakuwa halina nguvu sana kama linapokuwa ndani ya maji. Kama kweli mamba ameonekana wajulisheni askari wanyamapori wao ndio wanajua jinsi ya kuwawinda na kuwamaliza ili watu waendelee na shughuli za kibinadamu hapo kwenye hilo bwawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…