Mambo 10 kuelekea mwaka 1 wa kumkumbuka ya Hayati Magufuli

Mambo 10 kuelekea mwaka 1 wa kumkumbuka ya Hayati Magufuli

Sijui kwanini watu wanaona kuwa Magufuli alitenda mema sana wakati ndiye rais aliyefanya maovu mengi na kuwaumiza hata kuwaua watu wengi tu, kaharibu utengamano wa taifa kwa ukabila, kufanya matumizi mabaya ya fedha za umma kama CAG anavyoonesha, kuuwa makampuni mengi na kufanya upendeleo mkubwa kijijini kwake. Lazima uwe mtu mjinga kumwona Magufuli mtu wa kulilia.
Samahani Mkuu naomba nielezee kwanza ukabila wa mwendazake
 
Wajinga kama nyie hamuishi kwenu maendeleo hamuna Kwa elimu na mali za wizi utaka awafanyie nn kaangalue nyie mlivyokuwa wabaguzi kwanza
 
unaandika majungu tu hapa,ubaya aliofanya mtu haujifichi ni kanuni ya kawaida kabisa ya maisha.

magu angekuwa mwovu isingechukua wewe mwaka mzima kuwaeleza watu.
 
unaandika majungu tu hapa,ubaya aliofanya mtu haujifichi ni kanuni ya kawaida kabisa ya maisha.

magu angekuwa mwovu isingechukua wewe mwaka mzima kuwaeleza watu.
Unatetea mauaji? Wapi nimechukua mwaka mzima kusema haya. Kuna mtu asiyejua uovu wa awamu ya 5? Ndio maana mama anarekebisha sasa.
 
Wajinga kama nyie hamuishi kwenu maendeleo hamuna Kwa elimu na mali za wizi utaka awafanyie nn kaangalue nyie mlivyokuwa wabaguzi kwanza
Mlikula chini ya meza ya Magufuli hata nyama za watu sasa bado mnazililia!
 
Samahani Mkuu naomba nielezee kwanza ukabila wa mwendazake
Sijui nani asiyefahamu upendeleo mkubwa wa kuwajaza wasukuma serilalini na hata kampeni za kilugha na upendeleo wa miradi kanda ya ziwa. Maneno ya akina Gwajima na Makonda yalionesha ushenzi wa hali ya juu ni afadhali Mungu aliingilia kati watu wangeteseka sana kwa utawala ule.
 
Unatetea mauaji? Wapi nimechukua mwaka mzima kusema haya. Kuna mtu asiyejua uovu wa awamu ya 5? Ndio maana mama anarekebisha sasa.
mama anarekebisha mauaji unadhani anayeua ni mama???
 
Sijui nani asiyefahamu upendeleo mkubwa wa kuwajaza wasukuma serilalini na hata kampeni za kilugha na upendeleo wa miradi kanda ya ziwa. Maneno ya akina Gwajima na Makonda yalionesha ushenzi wa hali ya juu ni afadhali Mungu aliingilia kati watu wangeteseka sana kwa utawala ule.
Mkuu,
Kwahiyo saizi wasukuma hawapo serikalini?

Eleza kwa takwimu za upendeleo wa wasukuma serikalini wakati wa mwendazake?

Kwa kigezo ulichotumia basi Samia ana udini sababu kawachagua waislamu baadhi katika sekta tofaut tofaut? Maana wasukuma wachache walihalalisha kigezo chako cha ukabila

Kampeni zote alizofanya mwendazake alikua anaongea kilugha kulingana na eneo alilopo mfano akiwa kwa wagogo basi atasalimia kigogo, Je hilo nalo ni ukabila?
Au mtu akiongea tu kilugha basi ni ukabila, Kwa maana hiyo basi mwendazake hakuwa na ukabila bali alikua na makabila sababu aliongea lugha zaidi ya moja lakini tu kwenye eneo husika.

Unaweza kuanisha kwa mifano hapa ushenzi ulioongelewa na Makonda pamoja na Gwajima? basi tuwekee hapa wana JF tupate ushahidi huo.
 
Inajulikana wazi jinsi Gwajima alivyokuwa anawahamasisha wasukuma kilugha kupitia mtandao wamuunge mkono Magufuli kwani ni mtu wao. Salamu za kilugha hazina shida ila alihutubia kilugha huko mwanza na kanda ya ziwa. Ni mengi tu ya Ki ubaguzi na ubadhirifu mkubwa wa mali za umma yamefanywa. Pia watu wengi wameteswa na hata kuuwawa.
 
Mambo 10 kuelekea mwaka mmoja bila jpm/ bulldozer.

JASIRI
Hayati Magufuli alikuwa ni kiongozi jasiri ambaye aliamini kwenye kuamua hata kama mawazo yake hayaungwi mkono na walio wengi. Ujasiri wake ndio ulisaidia kutekeleza miradi Mingi na mikubwa ambayo haikuwahi kufikiriwa kuwa ingetekelezwa kwa muda mfupi.

Alikuwa kiongozi mahiri, shupavu na mwenye maono. Hivyo hakutaka kukwamishwa.

MZALENDO
Magufuli alikuwa mwana mwema wa Tanzania na Afrika. Alikuwa mzalendo wa kweli ambaye aliamini ipo siku Tanzania itakuwa ni donar Country. Alihamasisha watu kufanya kazi Kwa bidii na maarifa yote, huku akisistiza kuwa asiye fanya kazi na asile.

Alifanya haya ili kusmsha ali ya kufanya kazi. Na mtu yeyote aliyekuwa mvuvi hakuwa rafiki wa Dkt Magufuli. Hakuogopa kumfukuza mtu hadharani anapohisi anamkwamisha. Mdomoni mwake kila aliposimama aliizungumza Tanzania. Uzalendo wake na uchapa kazi wake uliweza kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati.

MWANAMAPINDUZI
Hayati Maguguli alikuwa ni mwanamapinduzi wa fikra. Alikuwa ni kiongozi ambaye aliamini kuwa Tanzania inakila kitu ila kwa muda mrefu ilikosa ujasiri wa kuamua. Miaka mingi hatukuzoe kusikia kiongozi yeyote Afrika anawavimbia Wazungu. Magufuli alikuwa na uwezo wa kuwasema Wazungu hadharani.

Aliamini kuwa Tanzania inaweza kujikomboa kutoka fikira tulizopandikizwa za kutegemea misaada na tukajitegemea. Alipoanza kujenga bwawa la Umeme la Nyerere Mataifa makubwa yalipiga kelele kuwa uhalibifu wa mazingira lakini JPM hakuwasikiliza Kwa kuwa aliamini mapinduzi ya Viwanda yanahitaji zaidi umeme.

Lakini pia alijua Umeme ni bidhaa inayouzika na inaweza kuitengenezea Tanzania fedha nyingi. Hivyo JPM alikuwa Mwanamapinduzi na mwanaharakati wa maendeleo.

MCHAPA KAZI
Uchapakazi wa JPM haukuwa na mawaa. Kuna wakati kitanda chake kilionekana kujaa faili. Sina uhakika kama alikuwa akipata muda wa kupumzika. Alikuwa siku nyingi yupo barabarani kusikiliza na kutatua kero za Wananchi. Aliwachukia watumishi waongo, wavivu na wanaopika data. Uchapa kazi wake ulimfanya kuwa na taarifa nyingi za kila mahali.

Kuna mahali ulikuwa unaweza kudhani ana faili za Watanzania wote. Uchapa kazi wake ndani ya kipindi kifupi Cha uongozi wake alifanikiwa kununua ndege, kununua meli, kujenga barabara, viwanja vya ndege, shule, vituo vya afya na hospital n.k

MTETEZI WA WANYONGE
Magufuli ilikuwa sauti ya Wantonge. Hakutaka kuona chozi la wanyonge linatoka. Hakusubiri kufanya utafiti kama hayo machozi ni ya kweli au si kweli maadam ameambiwa chanzo Cha chozi hili ni mtu flani alifanya maamzi. Aliamini kwenye kutumbua. Kama alidanganywa alikuwa ni mtu wa kuja hadharani kuwa nilidanganywa na kumrudisha mtu kazini.

Ukweli ni kuwa tumbua tumbua ilisaidia sana kuleta nidhamu maofisini. Kila mtu alifanya kazi kwa kumhofia mwenzake. Maofisini hatukuaminiana Kwa kuwa Kila mtu alikuwa usalama wa mwenzake. Tabia ya unanijua Mimi? JPM hakutaka kuisikia. Hii ilisaidia Sana kuwaweka wanyonge mstali mmoja na wale wa unanijua Mimi ni nani?

MKWELI ASIYE YUMBA,
Hayati JPM alikuwa mkweli asiyeyumba.Hakujua kulemba. Hakuchagua wa kumfokea anapokesea. Hata uwe kiongozi mkubwa alikuwa anakusema hadharani ukikosea. Aliwahi kumfokea Waziri wa ujenzi hadharani wakati wa mafuliko ya Morogoro, baadaye yeye mwenyewe JPM alijifuta chozi. Alikuwa na uchungu mkubwa anapoona mambo hayaendi.

Hakutaka mzaha! Wakati wa vurugu za Mtwara na Lindi aliwahi kusema kuwa........hata kama ni shangazi zao. Ukweli huu wa JPM ulimtengenezea maadui hasa wakwapuaji wa Mali za umma, na ulimtengenezea marafiki wengi hasa wa tabaka la chini.

Mwaka 2020 vijana wengi walikuwa wanasema sisi tunaenda kumpigia kura JPM, Wabunge na Madiwani hatuna shida nao. Huyu ndiye JPM ambaye kesho tr 17/3/2022 anatimiza mwaka mmoja tangu afariki.

SHUJAA NA HODARI,
Hayati Magufuli alikuwa Shujaa na hodari. Ushujaa na Uhodali ulikuwa unajidhihilisha kwenye maamzi. Hakutishika wala kuteteleka hata kama anavunja Sheria. Aliamini kuwa wakati mwingine Sheria zinachelewesha.

Alikuwa askari wa mstari wa mbele kutetea Utanzania kuliko mtu yeyote. Hakuogopa rangi ya mtu wala Taifa la mtu. Hakuogopa kusema Hapana au ndiyo. Umahiri wake na Uhodari wake alikuwa anapigiwa mfano kila mahali. Kwa mara ya kwanza alipoenda Afrika kusini kwenye uapisho wa Rais Kila mtu alitamani amuone huyu Simba wa Afrika.

HAKUWA MUUMINI MKUBWA WA DEMOKRASIA,
Hayati Magufuli alikuwa haamini katika demokrasia kubwa. Alikuwa anaamini demokrasia inachelewesha maendeleo. Alikuwa anasema mataifa makubwa yalianza kujenga demokrasia baada ya kujiimalisha kiuchimi. Kwa mtazamo wa hayati JPM ingekuwa ni ridhaa yake ninaamini angefuta mfumo wa vyama vingi.

Hapa ndipo alipojenga uhasama na Wanasiasa wengi. JPM hakupenda kuona mtu anamzuia mbele anapotaka kufanya jambo ndiyo maana hata watu walipohoji kuhusu ndege bado aliendelea kununua tena Kwa cash. Huu nao ni upekee mkubwa aliokuwa nao JPM. Watu kama hawa huzaliwa mara chache sana duniani.

ALIWAAMINI SANA VIJANA, JPM aliwaamini sana vijana kwenye uongozi wake. Aliwaamini vijana bila kujali itikadi ya vyama vyao. Aliamini kuwa Taifa hili litakuwa chini ya vijana Kwa muda mrefu, hivyo aliamini kuwapa vijana nafasi Kwa kuwa wananguvu nyingi. Wote aliowaamini aliwaambia fanyeni maamzi. Alisistiza bora kufanya maamzi ukakosea kuliko kutofanya maamzi.

ALIKUWA ANACHUKIA RUSHWA,
JPM alikuwa anachukia rushwa Kwa vitendo. Ili kutokomeza hili aliamua kuanzisha mahakama ya Rushwa ambayo ipo Mawasiliano Dar es salaam.

HUYU NDIYE JPM, MWANA MWEMA WA AFRIKA, MTETEZI WA WANYONGE NA SHUJAA. VITA ALIVIPIGANA, MWENDO ALIUMALIZA. R.I.P
makini sana
 
Uonevu na ukatili umekoma!
mauaji yameisha!
Ukabila na ukanda sasa unapotea!
Ukatili nao umekufa!
Uporaji na unyanganyi umefariki pia.
 
Back
Top Bottom