Mambo 10 niliyoyaona jana Yanga vs CRB ya Algeria

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
1. Yanga wamecheza mchezo mzuri sana lakini mpira ni matokeo

2.Ligi Kuu ya soka hapa bongo ilimpa kiburi Gamondi na kujiona kuwa anaweza kumvamia yeyote hapa duniani, hakujua kuwa ligi yetu ni kivyetu vyetu.

3.Huwezi kwenda kushiriki michuano mikubwa kama hii kwa ngazi ya afrika ukawa na mabeki aina ya Ibrahim Job na Ibrahim Bacca, au Mwamnyeto never on earth

4. Kwa kiwango cha jana cha Yanga kiukwel wakiendelea vile hapa Tanzania na afrika mashariki hakuna wa kuwazuia

5.Pacome na Mzengeli wabadilike, waache kuwa wachezaji machachari badala ya wacheza bora

6.Fowadi Yanga hakuna, Clement Mzize is too young to play against CRB

7.CRB watapata taabu sana mechi ya marudiano hapa nyumbani kwani they are not good to that extent

8.Mechi za ugenini hasa unapocheza na mwarabu kwao lazima uwe na adabu, otherwise yatakutokea kama ya jana.

9.Ligi ya mabingwa sio kama kombe la Loser, Gamondi japo ni mgeni atahadharishwe

10.Kipa Metacha Mnata sio kaliba ya Diarra, hajaacha mchezo wake wa kitoto wa kujifanya kaumia
 
Simple tu jana CRB wameonyesha mpira ni mipango sio pasi..
 
Wachezaji toka kwenye timu za Taifa walikuwa hoi kwa kukosa mapumziko ya kutosha.

Zengeli, Aziz Ki, Lomalisa hata Job hawakuwa kwenye ubora wao haswa.

Lini Mamelodi Sundowns walipaki basi ugenini?

Makolokolo SC fans pambaneni na mechi yenu ya leo kwanza maana Mwenzio akinyolewa tilia maji zako.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
NO.5 Wana mikimbio kama kenge
 

Haisaidii kitu, muhimu point 3
 
Yanga akichezewa pira kiberenge mwanzo mwisho hajawahi kutoboa!
 
Nilichokiona ni kwamba timu moja ilikuwa na wavulana wa soka na nyingine ilikuwa na wanaume wa soka!! Wavulana wa soka hulenga kuonekana lakini wanaume wa soka hulenga kupata matokeo!! Kingine nilichokiona ni kuwa mechi ya jana imethibitisha kuwa ubora kwenye mashindano ya kombe la losers haufui dafu kwenye mashindano ya kombe la mabingwa!!
 
Gamindi sio mgeni wa Champions league kacheza fainali hizo ujue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…