Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
1. Kipa wetu Pin Pin Camara ndio usajili namba moja mzuri uliofanywa na viongozi wa Simba, ni kipa ambaye hata kama anafungwa huwa anafungwa kama wanavyofungwa makipa wengine duniani lakini haiondoi ukweli kuwa kipa huyu ni bora mno na Aishi Manula atafute changamoto timu nyingine.
2. Shomari Kapombe 100% Jesus amepambana sana leo na kama sio mvua angeweza zaidi kusaidia kupandisha mashambulizi kwani hirizi zote zilikuwa kwake leo.
3. Beki Tshabalala amepungua sana uwezo, amesumbuliwa sana na yule winga wa kushoto wa Al Masry, yaani kama sio bahati kuwa upande wetu leo tungekuwa tunaongea mengine, ni vyema kocha Fahdu akaanza kumuamini Valentine Nouma.
4. Chamou bado sio beki mzuri, ana nguvu lakini hana maarifa, sio difenda mzuri kabisa kabisa.Ana madhaifu mengi mno.
Soma Pia: FT: Simba SC 2-0 Al Masry SC | Robo Fainali CAF CC | Uwanja wa Mkapa | 09 Aprili 2025
5.Hamza ni beki mzuri lakini yuko slow sana, timu inatafuta matokeo yeye anaanzisha mpira nyuma akiwa slow mno, anapokuwa na mpira haangalii mbele yeye anaangalia kipa na beki wake Chamou, ajirekebishe aongeze spidi.
6.Kagoma amecheza vizuri sana, lakini amechoshwa sana na Fabrice Ngoma, Ngoma hana kasi na nadhani tunahitaji kuwa na kiungo mwingine mzuri zaidi ya Ngoma mithili ya Feitoto.
7. Kibu hakuwa na mchezo leo pengine alipania sana gemu lakini nguvu alizokuwa nazo zilisaidia sana kuwakabili waarabu wale ambao kama sio kujiangusha zaidi ya bao mbili zingekaa pale
8. Viongozi wa Simba, Jean Charles Ahoua sio level ya Simba, kama tunasema yeye ndio wa kutuvusha basi tunajidanganya, Ahoua hata faulo anazolazimisha kupiga hana uwezo mzuri wa kupiga faulo kama Clatous Chama.Kila faulo anataka kupiga yeye halafu anapoteza, mechi ijayo na Afrika Kusini ajirekebishe.
9. Mukwala amecheza vizuri lakini sio kwa level ya timu kubwa kama simba, yule striker Sowah wa Singida ni mtu hasa.
10. Elie Mpanzu Kibisawala, dhambi zake nimebeba mimi, tukiongea ile kisoka wachezaji wa kimataifa Simba ni wanne tu, Camara, Mpanzu, Nouma na Che Malone, kama wachezaji wa kigeni wangekuwa na uwezo kama ule wa Mpanzu, wala tusingekuwa na presha kama ilivyokuwa leo, Mpanzu, Camara ndio wachezaji bora kabisa waliosajiliwa Simba.