Mambo 10 niliyoyaona leo Simba ikitinga Nusu Fainali na Kuivaa Stellenbosch ya Afrika Kusini

Mambo 10 niliyoyaona leo Simba ikitinga Nusu Fainali na Kuivaa Stellenbosch ya Afrika Kusini

Tatizo watu wakisema mapungufu mnaona sijui ni mamluki ni ushabiki maandazi kukaa unasifia kila kitu kwamba ndo ushabiki ni wehu

Hamkuona kwamba Jana simba intensity aliyocheza nayo kipindi cha kwanza kipindi cha pili alipooza akaanza kumtafuta kwa nguvu dk za nyongeza ndo ilikua gameplan ya fadlu si ndio ???

Yani upo dk ya 70 bado unacheza back passes huyo ahoua mnaesema ndo anasabisha mpanzu awe hivi mi nashidwa kuelewa sijui make hata ukiangalia goli za mpanzu halikutoka kwa ahoua ahoua huyo mnayemsifia kuna wakati golikipa wao alichoma akapata mpira mnakumbuka alichokifanya

Sio hivyo tu kuna krosi mukwala alifinya mabeki akapiga v pasi ikamkuta ahoua mnayemsifia yuko ye na goli mnakumbuka alichokifanya na mengine mengi ukianza kuchambua moja kati ya wachezaji waliopoteza mipira mingi ni pamoja na ahoua

Ko tumsifie kwa lipi kupiga faulo na kugongesha mwamba wakati timu inahitaji matokeo au hivi mnafikiria kweli yani jana kibu na ahoua ni moja kati ya wachezaji waliocheza hovyo

Simba Jana ingekua na no 10 walau mwenye asilimia 70vYa chama al masry walikua wanakufa zaidi ya goli 3

Tushukuru tu performance ya camara na mpanzu ila simba hasa kipindi cha pili walicheza hovyo dk za nyongeza ndo wakaanza kukamia unakamia dk za nyongeza ilihali ulikua na uwezo wa kufanya hivyo kabla

FADLU mwenyewe kasema anahitaji no 10 kutoka ndani Ina maana hajui au kwanini hajasema anataka no 6 au winga

Ahoua mchezaji wa kipumbavu sana kitete mguuni,hawezi kufungua wapinzani mbele yani Dah kila kitu mnasifia mnasahau kuna wakati tutacheza na timu ngumu ambayo kupata nafasi 1 ni golden chance ambayo ndo hiyo unatakiwa umalize gemu

Kazi kwakweli??
 
1. Kipa wetu Pin Pin Camara ndio usajili namba moja mzuri uliofanywa na viongozi wa Simba, ni kipa ambaye hata kama anafungwa huwa anafungwa kama wanavyofungwa makipa wengine duniani lakini haiondoi ukweli kuwa kipa huyu ni bora mno na Aishi Manula atafute changamoto timu nyingine.

2. Shomari Kapombe 100% Jesus amepambana sana leo na kama sio mvua angeweza zaidi kusaidia kupandisha mashambulizi kwani hirizi zote zilikuwa kwake leo.

3. Beki Tshabalala amepungua sana uwezo, amesumbuliwa sana na yule winga wa kushoto wa Al Masry, yaani kama sio bahati kuwa upande wetu leo tungekuwa tunaongea mengine, ni vyema kocha Fahdu akaanza kumuamini Valentine Nouma.

4. Chamou bado sio beki mzuri, ana nguvu lakini hana maarifa, sio difenda mzuri kabisa kabisa.Ana madhaifu mengi mno.

Soma Pia: FT: Simba SC 2-0 Al Masry SC | Robo Fainali CAF CC | Uwanja wa Mkapa | 09 Aprili 2025

5.Hamza ni beki mzuri lakini yuko slow sana, timu inatafuta matokeo yeye anaanzisha mpira nyuma akiwa slow mno, anapokuwa na mpira haangalii mbele yeye anaangalia kipa na beki wake Chamou, ajirekebishe aongeze spidi.

6.Kagoma amecheza vizuri sana, lakini amechoshwa sana na Fabrice Ngoma, Ngoma hana kasi na nadhani tunahitaji kuwa na kiungo mwingine mzuri zaidi ya Ngoma mithili ya Feitoto.

7. Kibu hakuwa na mchezo leo pengine alipania sana gemu lakini nguvu alizokuwa nazo zilisaidia sana kuwakabili waarabu wale ambao kama sio kujiangusha zaidi ya bao mbili zingekaa pale

8. Viongozi wa Simba, Jean Charles Ahoua sio level ya Simba, kama tunasema yeye ndio wa kutuvusha basi tunajidanganya, Ahoua hata faulo anazolazimisha kupiga hana uwezo mzuri wa kupiga faulo kama Clatous Chama.Kila faulo anataka kupiga yeye halafu anapoteza, mechi ijayo na Afrika Kusini ajirekebishe.

9. Mukwala amecheza vizuri lakini sio kwa level ya timu kubwa kama simba, yule striker Sowah wa Singida ni mtu hasa.

10. Elie Mpanzu Kibisawala, dhambi zake nimebeba mimi, tukiongea ile kisoka wachezaji wa kimataifa Simba ni wanne tu, Camara, Mpanzu, Nouma na Che Malone, kama wachezaji wa kigeni wangekuwa na uwezo kama ule wa Mpanzu, wala tusingekuwa na presha kama ilivyokuwa leo, Mpanzu, Camara ndio wachezaji bora kabisa waliosajiliwa Simba.
We usitake kutuboa chama nani kwenye Simba ya Sasa
 
Hussein hata game ya kwanza alichemka sn plus Ateba,analysis ya kocha ilimsaidia kumtoa mapema.
Wasauzi niwepesi sana so Ateba ni game inayomfaa sana,Debora pia ingemfaa ingawa bado kocha atampa nafasi Ngoma,mbaya zaidi simba anamalizia round away hapa ndio pagumu kwake
Mohamed hussein ni beki mzuri sana, but tuwe honest time does catch up to us eventualy, na nadhan umri umri
 
Hussein hata game ya kwanza alichemka sn plus Ateba,analysis ya kocha ilimsaidia kumtoa mapema.
Wasauzi niwepesi sana so Ateba ni game inayomfaa sana,Debora pia ingemfaa ingawa bado kocha atampa nafasi Ngoma,mbaya zaidi simba anamalizia round away hapa ndio pagumu kwake
Sio wepesi kiivo,nilidhani hivyo pia!
Sifa yao kubwa ni kucheza kitimu zaidi na intensity yao iko juu mud mwingi, hadi amefika hapa,sio wa kupuuza kabisa!
 
Na ndio maana yupo hapo Simba sababu ya ubora wake.

Ndipo uwezo wake ulipoishia leo. Kumbuka ni wachezaji wote wamecheza uwanja uliolowana na mvua. Hata wengine bila hali ya mvua wangekuwa na ubora zaidi hivyo ingejibalansi. Uzuri Simba wamefikia malengo ya mechi.

M. Husein kacheza mechi nyingi sana bila kupumzika. Anachoka anahitaji mapumziko

Nani kakudanganya Fadlu hamwamini Nouma. Ni kwamba kwenye mipango yake anaona ubora wa Husein ni zaidi ya Nouma. Ndio maana Nouma yupo Simba vile anaaminiwa na kocha

Ila wewe jamaa, yaani Chamou sio beki mzuri KABISA KABISA. Basi Simba leo ingebugia 20. Tumrudishe Kenedy Wilson sasa na Inonga.

Unaelewa nini maana ya game plan?
Unajua kocha aliwaelekeza wacheze kwa namna gani?
Unajua builder up plan ya kocha ilikuwaje?

Kwahiyo Simba haijapata matokeo vile Hamza alikuwa slow sana. Hakuna cha kujirekebisha hapo. Tafuta timu yako wawe wanakurupuka kucheza haraka haraka.
Kwani kocha hajui uchezaji wa Ngoma. Vipi ikiwa kocha alimwambia acheze alivyocheza ili kutoa nafasi wengine kujipanga.

Basi fanya mpango umsajili Fei Toto.

Haujui kufuatilia mpira, Kibu anasaidia sana kuzuia na kupandisha mipira mbele

Chama yupo Yanga, mfuate.

Utakuwa na makengeza ya ubongo wewe jamaa. Yaani Ahoua huyu huyu ninaemjua na kila shabiki wa Simba anamjua. Haya masihara sasa.

Unataka uwezo gani?
😂😂😂😂
Hebu kachungulie dakika walizocheza NBC ligi na magoli waliyofunga kila mmoja kisha usome tena komenti yako. Ukiendelea kushikilia msimamo wako basi ukafanyiwe oparasheni ya ubongo.

Leo kila mchezaji wa Simba kacheza vizuri kulingana na uwezo na nafasi yake. Ndio maana hata waliotokea benchi ndani ya dakika 90 wamefanya vizuri. Hata kwenye penati kipa kafanya kazi nzuri na wapiga penati kazi nzuri, magoli ya kiufundi na utulivu wa hali ya juu. Wote wamefunga.
👍👍👍👍👍👍👍🔥🔥🔥 SIMBA nguvu Moja
 
Hivi wanatumia vigezo gani timu hii kuanzia nyumbani na kumalizia ugenini hatua ya nusu fainali?
 
Back
Top Bottom