Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
Ngoma mzito umri umeenda,Simba wapo slowly sana kuanzia beki mpaka namba sita yani walikua wana anza mpira pole pole.1. Kipa wetu Pin Pin Camara ndio usajili namba moja mzuri uliofanywa na viongozi wa Simba, ni kipa ambaye hata kama anafungwa huwa anafungwa kama wanavyofungwa makipa wengine duniani lakini haiondoi ukweli kuwa kipa huyu ni bora mno na Aishi Manula atafute changamoto timu nyingine.
2. Shomari Kapombe 100% Jesus amepambana sana leo na kama sio mvua angeweza zaidi kusaidia kupandisha mashambulizi kwani hirizi zote zilikuwa kwake leo.
3. Beki Tshabalala amepungua sana uwezo, amesumbuliwa sana na yule winga wa kushoto wa Al Masry, yaani kama sio bahati kuwa upande wetu leo tungekuwa tunaongea mengine, ni vyema kocha Fahdu akaanza kumuamini Valentine Nouma.
4. Chamou bado sio beki mzuri, ana nguvu lakini hana maarifa, sio difenda mzuri kabisa kabisa.Ana madhaifu mengi mno.
Soma Pia: FT: Simba SC 2-0 Al Masry SC | Robo Fainali CAF CC | Uwanja wa Mkapa | 09 Aprili 2025
5.Hamza ni beki mzuri lakini yuko slow sana, timu inatafuta matokeo yeye anaanzisha mpira nyuma akiwa slow mno, anapokuwa na mpira haangalii mbele yeye anaangalia kipa na beki wake Chamou, ajirekebishe aongeze spidi.
6.Kagoma amecheza vizuri sana, lakini amechoshwa sana na Fabrice Ngoma, Ngoma hana kasi na nadhani tunahitaji kuwa na kiungo mwingine mzuri zaidi ya Ngoma mithili ya Feitoto.
7. Kibu hakuwa na mchezo leo pengine alipania sana gemu lakini nguvu alizokuwa nazo zilisaidia sana kuwakabili waarabu wale ambao kama sio kujiangusha zaidi ya bao mbili zingekaa pale
8. Viongozi wa Simba, Jean Charles Ahoua sio level ya Simba, kama tunasema yeye ndio wa kutuvusha basi tunajidanganya, Ahoua hata faulo anazolazimisha kupiga hana uwezo mzuri wa kupiga faulo kama Clatous Chama.Kila faulo anataka kupiga yeye halafu anapoteza, mechi ijayo na Afrika Kusini ajirekebishe.
9. Mukwala amecheza vizuri lakini sio kwa level ya timu kubwa kama simba, yule striker Sowah wa Singida ni mtu hasa.
10. Elie Mpanzu Kibisawala, dhambi zake nimebeba mimi, tukiongea ile kisoka wachezaji wa kimataifa Simba ni wanne tu, Camara, Mpanzu, Nouma na Che Malone, kama wachezaji wa kigeni wangekuwa na uwezo kama ule wa Mpanzu, wala tusingekuwa na presha kama ilivyokuwa leo, Mpanzu, Camara ndio wachezaji bora kabisa waliosajiliwa Simba.
Achana na wachambuzi uchwara. Yaani Ahoua hadi faulo hajui kupiga? Huyo mchambuzi akachambue mchele. Ni mwehuAchana na Ahouaaa....achana na Hamza....
Na hakuna wa kumtoa hapo ahouaa...mkae kwa kutulia...acheni ujuaji
Vipi ikiwa anacheza kwa kufuata maelekezo ya kocha wake na ndio maana anampangaHussein hata game ya kwanza alichemka sn plus Ateba,analysis ya kocha ilimsaidia kumtoa mapema.
Wasauzi niwepesi sana so Ateba ni game inayomfaa sana,Debora pia ingemfaa ingawa bado kocha atampa nafasi Ngoma,mbaya zaidi simba anamalizia round away hapa ndio pagumu kwake
Ngoma mzito umri umeenda,Simba wapo slowly sana kuanzia beki mpaka namba sita yani walikua wana anza mpira pole pole.
Kwa uzoefu jamaa yupo nao sana ilakwa team inayojua kumiliki mpira game itakua ngumu sana kwangu mm Debora ni mziri sana kuliko NgomaVipi ikiwa anacheza kwa kufuata maelekezo ya kocha wake na ndio maana anampanga
Hapana umeona dakika za mwisho wanachelewa kuanzisha mpira na kufata mpira wanachelewa kuanzisha na wanaona dakika zina kipimbia na wanatakiwa wapate goli la ushindi, wao Waarabu walishakata tamaa wakawa wana subiri bahati ya kufuzu kwa kutegemea penatiVipi ikiwa wanachezq slow kufuata maelekezo ya kocha wao
Viungo wa Simba hawana kasi, Wachezaji wenye kasi ni Mpanzu na kibu kidogo, Kagoma na Ngoma wazito na wanacheza pole poleVipi ikiwa wanachezq slow kufuata maelekezo ya kocha wao
Na ndio maana yupo hapo Simba sababu ya ubora wake.Kipa wetu Pin Pin Camara ndio usajili namba moja mzuri uliofanywa na viongozi wa Simba, ni kipa ambaye hata kama anafungwa huwa anafungwa kama wanavyofungwa makipa wengine duniani lakini haiondoi ukweli kuwa kipa huyu ni bora mno na Aishi Manula atafute changamoto timu nyingine.
Ndipo uwezo wake ulipoishia leo. Kumbuka ni wachezaji wote wamecheza uwanja uliolowana na mvua. Hata wengine bila hali ya mvua wangekuwa na ubora zaidi hivyo ingejibalansi. Uzuri Simba wamefikia malengo ya mechi.Shomari Kapombe 100% Jesus amepambana sana leo na kama sio mvua angeweza zaidi kusaidia kupandisha mashambulizi kwani hirizi zote zilikuwa kwake leo.
M. Husein kacheza mechi nyingi sana bila kupumzika. Anachoka anahitaji mapumzikoBeki Tshabalala amepungua sana uwezo, amesumbuliwa sana na yule winga wa kushoto wa Al Masry, yaani kama sio bahati kuwa upande wetu leo tungekuwa tunaongea mengine, ni vyema kocha Fahdu akaanza kumuamini Valentine Nouma.
Ila wewe jamaa, yaani Chamou sio beki mzuri KABISA KABISA. Basi Simba leo ingebugia 20. Tumrudishe Kenedy Wilson sasa na Inonga.Chamou bado sio beki mzuri, ana nguvu lakini hana maarifa, sio difenda mzuri kabisa kabisa.Ana madhaifu mengi mno.
Unaelewa nini maana ya game plan?5.Hamza ni beki mzuri lakini yuko slow sana, timu inatafuta matokeo yeye anaanzisha mpira nyuma akiwa slow mno, anapokuwa na mpira haangalii mbele yeye anaangalia kipa na beki wake Chamou, ajirekebishe aongeze spidi.
Kwani kocha hajui uchezaji wa Ngoma. Vipi ikiwa kocha alimwambia acheze alivyocheza ili kutoa nafasi wengine kujipanga.6.Kagoma amecheza vizuri sana, lakini amechoshwa sana na Fabrice Ngoma, Ngoma hana kasi na nadhani tunahitaji kuwa na kiungo mwingine mzuri zaidi ya Ngoma mithili ya Feitoto.
Haujui kufuatilia mpira, Kibu anasaidia sana kuzuia na kupandisha mipira mbeleKibu hakuwa na mchezo leo pengine alipania sana gemu lakini nguvu alizokuwa nazo zilisaidia sana kuwakabili waarabu wale ambao kama sio kujiangusha zaidi ya bao mbili zingekaa pale
Chama yupo Yanga, mfuate.Viongozi wa Simba, Jean Charles Ahoua sio level ya Simba, kama tunasema yeye ndio wa kutuvusha basi tunajidanganya, Ahoua hata faulo anazolazimisha kupiga hana uwezo mzuri wa kupiga faulo kama Clatous Chama.Kila faulo anataka kupiga yeye halafu anapoteza, mechi ijayo na Afrika Kusini ajirekebishe.
ππππMukwala amecheza vizuri lakini sio kwa level ya timu kubwa kama simba, yule striker Sowah wa Singida ni mtu hasa.
Leo kila mchezaji wa Simba kacheza vizuri kulingana na uwezo na nafasi yake. Ndio maana hata waliotokea benchi ndani ya dakika 90 wamefanya vizuri. Hata kwenye penati kipa kafanya kazi nzuri na wapiga penati kazi nzuri, magoli ya kiufundi na utulivu wa hali ya juu. Wote wamefunga.Elie Mpanzu Kibisawala, dhambi zake nimebeba mimi, tukiongea ile kisoka wachezaji wa kimataifa Simba ni wanne tu, Camara, Mpanzu, Nouma na Che Malone, kama wachezaji wa kigeni wangekuwa na uwezo kama ule wa Mpanzu, wala tusingekuwa na presha kama ilivyokuwa leo, Mpanzu, Camara ndio wachezaji bora kabisa waliosajiliwa Simba.
Vipi ikiwa kocha ndio kawaelekeza wacheze hivyo. Basi tukukabidhi benchi la ufundi uwaelekeze kucheza kwa kasiViungo wa Simba hawana kasi, Wachezaji wenye kasi ni Mpanzu na kibu kidogo, Kagoma na Ngoma wazito na wanacheza pole pole
Bila shaka Debora ni mzuri kwako, ila kwa Fadlu Ngoma ni bora zaidi ya Debora.Kwa uzoefu jamaa yupo nao sana ilakwa team inayojua kumiliki mpira game itakua ngumu sana kwangu mm Debora ni mziri sana kuliko Ngoma