We usitake kutuboa chama nani kwenye Simba ya Sasa1. Kipa wetu Pin Pin Camara ndio usajili namba moja mzuri uliofanywa na viongozi wa Simba, ni kipa ambaye hata kama anafungwa huwa anafungwa kama wanavyofungwa makipa wengine duniani lakini haiondoi ukweli kuwa kipa huyu ni bora mno na Aishi Manula atafute changamoto timu nyingine.
2. Shomari Kapombe 100% Jesus amepambana sana leo na kama sio mvua angeweza zaidi kusaidia kupandisha mashambulizi kwani hirizi zote zilikuwa kwake leo.
3. Beki Tshabalala amepungua sana uwezo, amesumbuliwa sana na yule winga wa kushoto wa Al Masry, yaani kama sio bahati kuwa upande wetu leo tungekuwa tunaongea mengine, ni vyema kocha Fahdu akaanza kumuamini Valentine Nouma.
4. Chamou bado sio beki mzuri, ana nguvu lakini hana maarifa, sio difenda mzuri kabisa kabisa.Ana madhaifu mengi mno.
Soma Pia: FT: Simba SC 2-0 Al Masry SC | Robo Fainali CAF CC | Uwanja wa Mkapa | 09 Aprili 2025
5.Hamza ni beki mzuri lakini yuko slow sana, timu inatafuta matokeo yeye anaanzisha mpira nyuma akiwa slow mno, anapokuwa na mpira haangalii mbele yeye anaangalia kipa na beki wake Chamou, ajirekebishe aongeze spidi.
6.Kagoma amecheza vizuri sana, lakini amechoshwa sana na Fabrice Ngoma, Ngoma hana kasi na nadhani tunahitaji kuwa na kiungo mwingine mzuri zaidi ya Ngoma mithili ya Feitoto.
7. Kibu hakuwa na mchezo leo pengine alipania sana gemu lakini nguvu alizokuwa nazo zilisaidia sana kuwakabili waarabu wale ambao kama sio kujiangusha zaidi ya bao mbili zingekaa pale
8. Viongozi wa Simba, Jean Charles Ahoua sio level ya Simba, kama tunasema yeye ndio wa kutuvusha basi tunajidanganya, Ahoua hata faulo anazolazimisha kupiga hana uwezo mzuri wa kupiga faulo kama Clatous Chama.Kila faulo anataka kupiga yeye halafu anapoteza, mechi ijayo na Afrika Kusini ajirekebishe.
9. Mukwala amecheza vizuri lakini sio kwa level ya timu kubwa kama simba, yule striker Sowah wa Singida ni mtu hasa.
10. Elie Mpanzu Kibisawala, dhambi zake nimebeba mimi, tukiongea ile kisoka wachezaji wa kimataifa Simba ni wanne tu, Camara, Mpanzu, Nouma na Che Malone, kama wachezaji wa kigeni wangekuwa na uwezo kama ule wa Mpanzu, wala tusingekuwa na presha kama ilivyokuwa leo, Mpanzu, Camara ndio wachezaji bora kabisa waliosajiliwa Simba.
Mohamed hussein ni beki mzuri sana, but tuwe honest time does catch up to us eventualy, na nadhan umri umriHussein hata game ya kwanza alichemka sn plus Ateba,analysis ya kocha ilimsaidia kumtoa mapema.
Wasauzi niwepesi sana so Ateba ni game inayomfaa sana,Debora pia ingemfaa ingawa bado kocha atampa nafasi Ngoma,mbaya zaidi simba anamalizia round away hapa ndio pagumu kwake
Sio wepesi kiivo,nilidhani hivyo pia!Hussein hata game ya kwanza alichemka sn plus Ateba,analysis ya kocha ilimsaidia kumtoa mapema.
Wasauzi niwepesi sana so Ateba ni game inayomfaa sana,Debora pia ingemfaa ingawa bado kocha atampa nafasi Ngoma,mbaya zaidi simba anamalizia round away hapa ndio pagumu kwake
ππππππππ₯π₯π₯ SIMBA nguvu MojaNa ndio maana yupo hapo Simba sababu ya ubora wake.
Ndipo uwezo wake ulipoishia leo. Kumbuka ni wachezaji wote wamecheza uwanja uliolowana na mvua. Hata wengine bila hali ya mvua wangekuwa na ubora zaidi hivyo ingejibalansi. Uzuri Simba wamefikia malengo ya mechi.
M. Husein kacheza mechi nyingi sana bila kupumzika. Anachoka anahitaji mapumziko
Nani kakudanganya Fadlu hamwamini Nouma. Ni kwamba kwenye mipango yake anaona ubora wa Husein ni zaidi ya Nouma. Ndio maana Nouma yupo Simba vile anaaminiwa na kocha
Ila wewe jamaa, yaani Chamou sio beki mzuri KABISA KABISA. Basi Simba leo ingebugia 20. Tumrudishe Kenedy Wilson sasa na Inonga.
Unaelewa nini maana ya game plan?
Unajua kocha aliwaelekeza wacheze kwa namna gani?
Unajua builder up plan ya kocha ilikuwaje?
Kwahiyo Simba haijapata matokeo vile Hamza alikuwa slow sana. Hakuna cha kujirekebisha hapo. Tafuta timu yako wawe wanakurupuka kucheza haraka haraka.
Kwani kocha hajui uchezaji wa Ngoma. Vipi ikiwa kocha alimwambia acheze alivyocheza ili kutoa nafasi wengine kujipanga.
Basi fanya mpango umsajili Fei Toto.
Haujui kufuatilia mpira, Kibu anasaidia sana kuzuia na kupandisha mipira mbele
Chama yupo Yanga, mfuate.
Utakuwa na makengeza ya ubongo wewe jamaa. Yaani Ahoua huyu huyu ninaemjua na kila shabiki wa Simba anamjua. Haya masihara sasa.
Unataka uwezo gani?
ππππ
Hebu kachungulie dakika walizocheza NBC ligi na magoli waliyofunga kila mmoja kisha usome tena komenti yako. Ukiendelea kushikilia msimamo wako basi ukafanyiwe oparasheni ya ubongo.
Leo kila mchezaji wa Simba kacheza vizuri kulingana na uwezo na nafasi yake. Ndio maana hata waliotokea benchi ndani ya dakika 90 wamefanya vizuri. Hata kwenye penati kipa kafanya kazi nzuri na wapiga penati kazi nzuri, magoli ya kiufundi na utulivu wa hali ya juu. Wote wamefunga.
πππππAchana na wachambuzi uchwara. Yaani Ahoua hadi faulo hajui kupiga? Huyo mchambuzi akachambue mchele. Ni mwehu