Mambo 10 niliyoyaona Simba ikiikaanga Al Ahly Tripoli ya Libya

Mambo 10 niliyoyaona Simba ikiikaanga Al Ahly Tripoli ya Libya

Camara saves of the match,maana pale kama lingeingia mechi ilikiwa imeshia pale.
Watu wameenda kwa 3, unasema lingeingia match imeisha, ina maana 3 kwa 2 hao waarabu koko wangeenda makundi?

Nina dawa ya maumivu uyasikiayo, hata usipate tabu, poleee.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ile ni offside, hata mimi nilishangaa goli kukataliwa ila baada ya mechi Azam waliirudia lile tukio. Unaona mshika kibendera alinyoosha kibendera mapema kabisa baada ya mchezaji aliyepo kwenye offside position kuuingilia mchezo. Refa wa kati ndiye aliyechelewa kuona.
Watuu wakachoma la 3, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Vipi nalo Off side? Mtasemaa yotee leoo.
 
Ilo ndio pira Irizi, timu haijulikani inacheza Nini lakini Magoli yanapatikana[emoji2][emoji2]
Dawa ya maumivu uliyonayo leo, ninayo wahii upate tibaaa.
Poleee wee, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Zilikutana pipa na mfuniko timu zote 2, Hawa waarabu wangekutana na yanga hakika wangechapika kuanzia kule kule kwao na uku wangeondoka na aibu ya mwaka, Simba imeingia group stage lakini timu bado sana tunawaambia, kama Hawa waarabu tu weupe hivi wanakupa tabu vipi ukikutana na timu inayojielewa itakuwaje?
Kwa sasa ndiyo mumehamia huku?
 
Kwa kifupi simba imecheza vizuri sana, narudia imecheza vizuri sana
 
Timu zinazojielewa ni zipi embu zitaje tuone kama.unajua kweli mpira , na ukitaja timu taja na mifumo wanayocheza na ulinganishe na simba na uelezee kwa kirefu kwanini mfumo wa hio timu utaushinda mfumo wa simba..
Fanya haraka tupe.jibu
Labda anamaanisha CBE mkuu
 
1. Mchezo ulikuwa mzuri lkn ulitaka kuwa mgumu baada ya Mabululu kututanguliza na waarabu kuweka viungo wengi kati kuliko sisi ambao tulimtegemea sana Kagoma na Fernandez

2. Che Malone ameanza kutupanda kichwani, yeye na Hamza uchezaji wao uko slow sana na kama tungecheza na timu kubwa kama zile za Champions leo kufuzu ingekuw ngumu

3. Timu aliishika sana Kibbu Denis leo, nilitukana na kulaani sana alipotolewa kabla ya Joshua Mutale. Kumtoa Kibbu kungeweza kutugharimu sana

4. Kweli nimeamini refa alipewa gemu kujaribiwa, unawezaje kukataa clear goal namna ile

5. Ukweli ni kuwa viungo wetu wa pembeni bado wana kazi kama tunahitaji mafanikio, afadhali nimemuona jukwaani Elie Mpanzu

6 Lionel Ateba ni mtu hatari sana kwa usalama wa Taifa

7. Jean Charles Ahoua bado hajaniridhisha kabisa kiwango chake alipaswa kukaa benchi kitambo t

8 Mussa Camara na Kibbu Denis ndio Nyota wa mchezo leo

9 Fahdu aambiwe tumeshinda leo lkn bado Simba haichezi mpira mzuri na hata sub pia zinamshinda

10 Mabululu anaipenda Sana na mshambuliaji aliyekamilika 100%, Simba inaweza kumuacha Mukwala ikambeba Mabululu

Nimefurahi sanaaaaaa leo

Soma Pia: FT: Simba SC 3-1 Al Ahly Tripoli | CAFCC | 2nd Leg | Benjamin Mkapa Stadium | 22-09-2024
kuna dogo wenu mmoja anaitwa shabalala, hata kama mnamtukana kuwa amezeeka, ni mtu mbadi sana yule, kijana yule hata timu ya taifa kama ataendelea hivyo atacheza hata akiwa na miaka 40. ana uwezo mkubwa na siku zote huwa anawasaidia sana.
 
Zilikutana pipa na mfuniko timu zote 2, Hawa waarabu wangekutana na yanga hakika wangechapika kuanzia kule kwao na wangeondoka na aibu ya mwaka, Simba imeingia group stage lakini timu bado tunawaambia, kama Hawa waarabu tu weupe hivi wanakupa tabu ukikutana na timu inayojielewa. itakuwaje?
Kama wale makarani wa fedha, mmewafunga Sita tu, mgeigunga mengi timu iliyowekeza ksma ile.
 
1. Waliompa jina Camara kuwa ni "spiderman" hawakukosea. Lile shuti la Mabululu wakati Camara anarudi upande mwingine ni makipa wachache sana wanaweza kufanya ile "save". Na kwa muda ule lingekuwa goli basi mechi ingeishia pale pale.
2. Che Malone anajiamini kupita kiasi huku anafanya makosa ya wazi kabisa wakati yeye ni mtu wa mwisho. Asipojirekebisha ipo siku ataichomesha Simba.
3. Benchi la ufundi Simba ni kweli lilichemsha mno na kuifanya ngumu baada ya kumuacha Mutale muda mrefu uwanjani wakati mechi ilishamshinda. Na mbaya zaidi unamtoa Kibu unamuacha Mutale anazurura uwanjani akipata mpira badala atoe pasi anakaa nao muda mrefu mpaka anayang'anywa.
4. Nilipongeze benchi la ufundi la Simba kwa kuanza kufanyia kazi " counter attack".
5. Magori na kamati yake wajulishwe kuwa bado Simba inahitaji namba 10 mwingine wa kumuongezewa Ahoua nguvu. Anatakiwa namba 10 hasa wa kulainisha mambo pale mbele.
6. Watu wengi wanalaumu mabeki wa kati kwenye goli alilofungwa Simba. Lakini mimi nawakumbusha tu mchezaji wa timu pinzani alipiga "free header" kuingiza mpira kati. Hayo makosa mara nyingi sana Kapombe na Mohamed Hussein wanayarudia sana wanashindwa ku screen mchezaji wa mwisho wakati faulu inapigwa.
7.Kwa Ateba walau Simba wamepata mtu. Kadri anavyocheza anaonyesha kuimarika akiendelea hivi atakuwa msaada sana kwa Simba.

Ni mtizamo tu
No 6 uko sahihi, shabalala anapenda kuingia Kat na kuacha pembeni pawe wazi.
 
Kwa simba hii mdebwedo furaha ni ya muda mfupi tu!! Kupiga timu mbovu si kipimo cha ubora!!
 
.

✍🏻Kipindi cha kwanza kwenye build up ya Simba SC kulikuwa na tatizo la kimuundo :

1: Distance kubwa kutoka mstari wa walinzi wa kati kwenda viungo na mstari wa mwisho wa ushambuliaji kiais kwamba Malone na Hamza walikuwa wanalazimika kupiga sana mipira mirefu

2: Tripoli walichofanya ni kuzuia kwa 4-4-1-1 namba kumi wao anakuwa anasimama na Fernandes maana ya anawanyima options mabeki wawili kupasia fupi kwa Fernandes ( ambaye ndio progressor mkuu )

✍🏻Ni sawa pia Tripoli ambao game plan yao inaonekana ni kumeza mashambulizi na kucheza kwa counter attacks lakini haikuwa na ufanisi kwanini ?

1: Hawana wingers wenye spidi sana ambao wa kum support Mabululu

2: Distance kubwa baina ya Mabululu na viungo washambuliaji kiasi kwamba second balls zote zilikuwa kwa Fernandes na Kagoma

✍🏻Kipindi cha pili Simba SC walikuwa better , vitu ambavyo hawakufanya kipindi cha kwanza , cha pili walifanya vizuri

1: Distance ndogo baina ya mistari yote mitatu maana yake inarahisisha kusogea na mpira mbele kutoka nyuma

2: Muundo mzuri wa ulinzi pale ambapo wana mpira ( si chini ya wachezaji wanne nyuma ) maana yake hata mpira ukipotea wapo salama dhidi ya transition

3: Movements sahihi hasa kwa wale ambao hawana mpira , kipindi cha kwanza kuna nyakati walikuwa wanaenda sana sehemu moja , cha pili tofauti .

4: Decision making hasa kwenye counter attacks ( idadi ya wachezaji wanaoenda mbele , spidi , passing , finishing )

5: Work rate , hakukuwa na abiria uwanjani .

NOTE

1: Reaction ya wachezaji kurudi mchezoni kipindi hiko hiko cha kwanza ilikuwa nzuri . Fanya ufanyavyo ufunge goli kwa namna yoyote ile ( mpira uliokufa , makosa ya mpinzani , uwezo binafsi etc etc )

2: Nafasi mbili kwa Mabululu moja kambani moja save ya Camara

3: Kila nikifikira ile offside imetokea wapi ? 🤔

4: Ahoua kipindi cha pili aliwaka sana , anaficha mali , decision making .

5: Kibu D spidi na power 🔥

6: Balua kauwa mechi , Camara kashinda mechi na ile Save

7: Beki wa kushoto wa Tripoli anajua boli

8: Ateba : Nguvu , Spidi , anatunza mali goli akilipa mgongo la mpinzani , kazi ya lone striker 🔥

FT: Simba SC 3-1 Tripoli C/P
 
Zilikutana pipa na mfuniko timu zote 2, Hawa waarabu wangekutana na yanga hakika wangechapika kuanzia kule kule kwao na uku wangeondoka na aibu ya mwaka, Simba imeingia group stage lakini timu bado sana tunawaambia, kama Hawa waarabu tu weupe hivi wanakupa tabu vipi ukikutana na timu inayojielewa itakuwaje?
Shetani upo kwenye ubora wako na utanena sana kwa lugha....
 
Shetani upo kwenye ubora wako na utanena sana kwa lugha....
Mashetani wamebaki upande wenu maana wanaokoka na kuusema ukweli kama mwanachama wenu mtiifu bwana Kaduguda kwamba mpo kwenye kombe la wakinamama, na mmekutana wote ni sanda na maiti akukuwepo na mwenye nafuu!
 
Back
Top Bottom