Mambo 10 niliyoyaona Simba vs Tabora

Mambo 10 niliyoyaona Simba vs Tabora

Kwavile kafunga, umesahau alivyoimbwa Jobe alivyoingia uwanjani mashabiki wa Simba hawakutaka kusubiria muda wakaanza kumsifia Jobe ni bonge la fundi halafu wakamsema Freddy kuwa ndio garasa.
Mangungu na Mwamedi wanataka mashabiki wa design hiyo
 
Awesu ndio anamalizia mpira wake ,

Mngemuona kipindi yupo Arusha anacheza ndondo 2010 mngesemaje?

Nashangaa Leo et ana miaka 28

Ina maana kipind kile anakichafua Sheikh Amri Abeid pale Arusha alikuwa ana miaka 14?
Hanatofauti na mchezaji chipukizi wa tff aka mzize, kakimbiza bodaboda miaka mi3 leo hii tunaambiwa kinda wa miaka 18
 
Awesu anaimbwa sana mtandaoni, nahitaji kumtizama zaidi na zaidi kuthibitisha hili.

Ni kweli ahoua anamfanya mukwala asiwe hatari.. Simba inahitaji playmaker lakini sidhani kama awesu ndio suluhu ya hili tatizo.
 
1.Awesu Awesu fundi wa mpira
2.Awesu Awesu Fundi wa mpira
3.Awesu Awesu Fundi wa mpira
4.Awesu Awesu fundi wa mpira
5.Jeans Charles Ahoua anamfanya Mukwala aonekane nyoka wa kibisa, nafasi yake asimame Awesu Awesu
6.Okajeph au Kagoma ndio mbadala wa Mzamiru, Mzamiru anachelewesha sana mipira
7.Abdulrazak Hamza mzawa halisi wa kibongo
8.Timu bado inacheza kwa slow iongeze spidi
9.Mukwala anaonekana mchovu kwa sababu ya Ahoua
10.Kiungo wa chini awe Okajepha, wa juu Debora kumi Awesu Awesu fundi wa boli, nna hakika ipo siku mtu anakula 8
😫😫😫
Bantu Lady wanatamba Huku 😪😪😪
 
Hongera Simba kwa ushindi japo walikuwa na uwezo wa kushinda goli nyingi zaidi ya hizo tatu. Na hili narudia tena aliye karibu na uongozi pamoja na benchi la ufundi awasanue bado mapema kuwa waachane na tabia ya kuridhika baada ya kufunga goli moja au mawili. Hili kosa naona Simba bado hawajifunza yaliyotokea msimu uliopita wanaenda tena kulirudia msimu huu.

Mwishoni mwa ligi mshindi anaweza kupatikana kwa tofauti ya magoli na kipindi cha kuvuna magoli ni mechi hizi za mwanzoni wakati timu hazijakaa vizuri. Sasa ukija kwa Simba mpira ukianza wanatafuta magoli kwa nguvu halafu wakipata goli moja au mawili ndio basi tena wakiona mpinzani ni dhaifu kidogo ujue mpira ndio umeishia hapo. Wataanza pasi zao fupi fupi kule nyuma wakati washambuliaji wanasubiri mipira kule mbele wafunge. Hii tabia mbovu ilikuwa msimu uliopita naona na baadhi ya wachezaji wapya nao wameshafundishwa na wenzao waliowakuta. Viongozi na benchi la ufundi walikemee hili jambo tena mapema hii tabia kwani msimu huu idadi ya magoli itakuwa na umuhimu mkubwa sana na ndio inaweza kuja kuamua ubingwa iwapo timu zitafungana kwa pointi.

Kwa haraka haraka nilichokiona kwenye mechi ya leo:-
1. Simba hii ya sasa imemzidi kasi Muzamiru. Asipobadilika haraka atapotea mazima. Asione aibu ajifunze kwa Mavambo mpira haukai mguuni kwake zaidi ya sekunde 30 labda kuwe na sababu ya msingi. Na kikubwa zaidi ageukie mbele sio kurudi rudi nyuma kila saa. Mwenzake Ngoma msimu uliopita alikuwa tegemeo la Simba pale kwenye dimba la kati lakini mechi hizi chache kapotea mazima na sidhani kama kama atakuwepo Simba baada ya dirisha dogo.
2. Ahoua kama anakuja halafu anapotea. Benchi la ufundi lisione aibu hiyo nafasi yake apewe Chasambi aanze kwani mpaka sasa Ahoua ameshindwa kuitendea haki hiyo nafasi. Ahoua amekuwa yupo "slow" sana na ana uchoyo kiasi anainyima Simba magoli kwa kutaka afunge mwenyewe hata kama hayupo kwenye nafasi nzuri na wenzake wapo kwenye nafasi nzuri. Benchi la ufundi kama linampenda sana Ahoua na ili asipotee kabisa basi liwe linampa dakika chache na kuziongeza taratibu mpaka aingie kwenye mfumo vinginevyo watampoteza mazima maana ukimwangalia usoni kama anaaza kuchanganyikiwa na kukata tamaa japo anaonekana ana uwezo mkubwa.
3. Aliye karibu na Mohamed Huseini amwambie mapema kuwa huko anakoelekea sio kuzuri. Sijui ndio ufaza au kaizoea sana Simba. Anakaa sana na mpira bila sababu, anapenda kurudisha mpira nyuma bila sababu na mbaya zaidi ni kile kitendo cha kufika kwenye kona ya adui washambuliaji wanasubiri krosi yeye anageuka nyuma anaanza pasi fupi. Kwenye mechi ya leo alipiga krosi mbili hatari moja ikaza goli na nyingine ilipita katikati ya goli ikakosa mmaliziaji. Kama tokea mwanzo angefanya hivyo Simba leo ilikuwa ipate magoli mengi. Na huyu ndio kinara wa kuridhika na matokeo. Simba ikiwa inaongoza tu goli moja aua mbili ndio huwa anaanzisha upuuzi wake wa kuoiga pasi fupi fupi kwa wenzake kule nyuma badala aipeleke timu mbele ipate magoli zaidi.
4. Mukwala nimpe pole yake. Aambiwe tu ukweli kuwa juhudi anayo lakini anakosa utulivu mbele ya goli. Ni vema akajulishwa wapenzi wa mpira hasa wa hizi timu kubwa hawana simile. Akichelewa kujitafuta asije kushangaa ule umati uliokuwa unamshangilia wakati anatambulishwa umati ule ule ukaanza kumzomea. Na hapo ndio atakapochanganyikiwa na kupootea kabisa.
5. Musa Camara ni golikipa mzuri sana lakini tabia yake ya kusogea sana mbele ya goli lake akumbushwe tu isiwe kila saa kwani ipo siku atakutana na wale waataalamu wenye kuweza kuuvusha mpira kutokea kwenye nusu yao hadi kwenye goli la mpinzani. Au ikitokea bahati mbaya mchezaji wa Simba akapoteza mpira halafu ukanaswa na mchezaji wa timu pinzani ajue hiyo itakuwa dhahama kwake kwani hawahawa mashabiki na wapenzi wa Simba wanaomsifia leo ndio hawahawa watakaomtukana hadharani hasa ikiwa amechomesha mechi muhimu.
6. Kwa mtizamo wangu Okejepha ndio kiungo sahihi wa jiko la chini lakini mpaka sasa sijajua kwanini benchi la ufundi halipendi kumwamini. Nimemwangalia mechi zote alizocheza amekuwa anaichangamsha sana timu kwa ujumla kiasi unaiona timu inapata kasi kuelekea kwenye lango la adui. N apia timu inakuwa na utulivu pale katikati. Anyway makocha ndio wapo naye mazoezini kila siku labda wana sababu za kiufundi wanazojua wao kwa nini hawamwamini Okejepha asianze mwanzo mwisho.
7. Mwisho nasubiri kwa hamu siku ambayo benchi la ufundi la SIMBA litakapokuwa limelewa halafu pale kwenye viungo wawili wa kati wakaanza na Okejepha na Kagoma halafu pale juu namba 10 akacheza Mavambo!

Ni mtizamo tu.
 
SIMBA BWANA, MABINGWA WA KUSIFIA WACHEZAJI WAO NA KUAMINISHA WATU. YAANI UNAWEZA KUOGOPA. SITASAHAU KIPINDI ONANA NA CHE MALON WAMESAJILIWA. NILIJUA ONANA NI LEVEL ZA NEYMAR
 
Back
Top Bottom