Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
1. Mechi ilikuwa nzuri mno na ya ushindani kuliko hata ile na Simba, kilichowaharibia Singida ni udhamini wake kwa GSM.Ukikubali kuvaa jezi yenye nembo hiyo hata ucheze namna gani lazima ufungwe tu.Wamecheza mpira mzuri na wengi tumeshangaa inakuwaje wanasajili wachezaji wazuri kuliko wa Simba?
2.Singida wana watu na sijui nani anayesajili wachezaji wake halafu sisi tunaletewa Mutale, Ahoua, Chamou, Nouma, Mukwala.Wale watu Bada, Kofi, Damaro, Likeyekeye, Chukwu, Tchakei wale ni levo ya Simba kabisa na hao akina Ahoua ndio wanatakiwa waende Singida.
3.Kocha Hemed Morocco amuite mara moja winga Edmund John, yule dogo sio wa kucheza hapa bongo sema ndio hivyo tena.Hakuna kiungo wa pembeni kwa sasa hapa nchini kumshinda Edmund John, hata Often Chikola bado sana.
4. Pacome 'Zuzu' ni mchezaji mzuri lakini leo amedhihirirsha kuwa akikutana na wachezaji wanaojua anakuwa wa kawaida tu, hakuna lolote la maana alilolifanya uwanjani.
5.Yule kiungo Mohamed Damaro jamani, jamani, jamani, yaani yule acheze Singida kweli halafu Ngoma, Kagoma ndio wacheze Simba? Kweli mashabiki wana haki ya kutaka kuachiwa timu yao.
6.Yanga wameshinda lakini sio timu ya kubeba ubingwa wa Afrika, wa kawaida sana.Leo Singida wameonyesha magepu mengi ndani ya kikosi hicho, kama sio kuleta udugu ngoma ilikuwa ngumu sana.
7.Kama Ligi itakuwa na timu zenye wachezaji wenye ubora kama Singida ingawa wamefungwa kwa mambo ya nje ya uwanja basi ligi yetu itakuwa ngumu sana.
8.Kuna mambo yanawasaidia sana Yanga kupitia kamati zao za mashindano, wako vizuri sana kwenye mambo ya ufundi vinginevyo leo hawakuwa na timu ya kuifunga Singida.
9.Narudia tena hakuna haja ya kwenda nje kutafuta kiungo wa chini zaidi ya Mohamed Damaro wa Singida Big Star.
10.Narudia hakuna kiungo wa juu wa kumzidi Arthur Bada, huna sababu ya kuhangaika kumuibia Mo hela zake kwenda kumtafuta Ahoua.Jonathan Sowah hana akili ingawa ni mchezaji hatari.