Siku ya jana katika kuadhimisha siku ya walimu Duniani, nimekutana na jumbe nyingi zinazoonyesha uelewa wa Watanzania juu ya kazi ya utekelezaji wa miradi katika Elimu inayofanywa kwa weledi chini ya Uongozi wa serikali ya awamu ya sita, tuangazie baadhi ya mambo;
1.Ujenzi wa Shule mpya za sekondari na shule ya msingi zipatazo 266.
2. Ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa ya shule za msingi, vituo shikizi, na shule za sekondari vipatavyo 18,219.
3. Ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi na sekondari vipatavyo 4,525.
4. Ukamilishaji ujenzi wa vyumba vya maabara vipatavyo 1,399.
5. Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari yapatayo 568.
6. Ujenzi wa mabweni kwa shule za msingi na sekondari yapatayo 170.
7. Ujenzi wa nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari zipatazo 42.
8. Kutolewa ajira za walimu wapatao 9800 wa kada tofauti tofauti.
9. Watumishi katika wizara ya Elimu kwa maana ya walimu, waratibu wa Elimu na Maafisa Elimu kulipwa malimbikizo na madai yao yote yaliyohakikiwa.
10. Kutolewa fedha za Mikopo ya Elimu ya juu na kuondolewa kwa tozo ya VRF kiasi cha asilimia 6 kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo.
Rais Samia Suluhu anachapa kazi na anastahili pongezi za dhati, kama mwananchi mwenye kujitambua nitaendelea kushiriki ujenzi wa Taifa langu kwa vitendo.