Mambo 15 niliyoyaona leo Simba ikiivua ubingwa Wydad kwa Mkapa

Saidoo afurushweee, lina nuksi, mikosi na gundu lile zee, khaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamani acheni kumbeza mchezaji namna hii...ana mchango wake..mwacheni mwalimu ndo anaejua..kumtamkia mchezaji maneno kama haya wkt anaipambania timu yetu si uungwana hata kidogo..kila mtu ana ups an downs zake...

Sijapenta Cocaa.. 😊
 
Kuna watu mna Siri!! Wydad alichukua ubingwa kimya kimya na Leo kavuliwa?
Nimeishia kusoma kichwa cha habari tu, nilipoona ameandika kumvua ubingwa nikaacha kusoma content nikaenda kwenye comments za watu.
Hata kama ingekuwa Wydad ndio bingwa mtetezi, huwezi kusema Wydad kavuliwa ubingwa wakati kuna mechi mbili zimebaki ambazo ni sawa na alama 6 kwa kila timu. Hadi sasa timu zote tatu ( Wydad, Galaxy na Simba) yeyote anaweza kuungana na Asec kwenye kufuzu. Wydad akishinda mechi inayofuata dhidi ya Galaxy halafu Simba ikafungwa mechi inayofuata dhidi ya Asec, basi asilimia ya Simba kufuzu itakuwa ni chache sana. Kwasababu Wydad atamaliza mechi yake nyumbani dhidi ya Asec mwenye uhakika wa kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na point 13 zisizoweza fikiwa na yeyote ile. Hivyo kutokana na Wydad kuwa nyumbani na Asec ku relax, Wydad anaweza kumfunga Asec kule Morocco na safari ikaishia hapo.

Hatima ya hili group litakuwa kwenye mzunguko wa tano.
 
7.Simba imeshinda kwa sababu mpira umechezwa sana nje otherwis wasingekuga wale wamanga.


11.Saido Ntibazonkiza bado anahitajika sana kikosini, leo angekuwepp lazima angeweka kambani.
Sentensi zinazojicontradict. Kwamba Simba imeshinda kwa kuwa mpira umechezwa sana nje, halafu unakuja kusema Saido Ntibazonkiza angekuwepp lazima angeweka kambani. Ina maana Saido angecheza ndio mpira usingekuwa umechezwa nje?
 
10.Mwamba wa Lusaka sijui nini kimemkuta, uwezo umepungua sana.

11.Saido Ntibazonkiza bado anahitajika sana kikosini, leo angekuwepp lazima angeweka kambani.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa lakini naomba nitofautiane na wewe kidogo hapo kwenye namba 10 na 11.

Kwanza kabla ya kumsifu Onana naomba kwa nia nzuri tu urudi " youtube" uangalie mara mbili mbili uone goli zote mbili zimeanzia kwa nani kama sio kazi kubwa liiyofanywa kwanza na Chama. Chama aliyeisha ni bora zaidi mara mbili ya Saidoo aliye "fit" . Na leo Saidoo angekuwepo Simba wasingepata hata goli moja kwa sababu Saidoo ana juhudi sana bila akili na utlivu na hicho ndio kinachomtofautisha yeye na Chama.
 
1. Taja timu inayoongoza kuifunga magoli mengi sana Mbumbumbu SC duniani.

2. Taja timu inayoongoza kuifunga Mbumbumbu SC mechi nyingi sana duniani.

3. Mara ngapi Makolokolo waligoma kurudi uwanjani dhidi ya Yanga SC baada ya kichapo kizito cha half time kumaliza dakika 90 za mpira?

Makolokolo mnajitutumua tu kwa Mabingwa wenu Yanga SC, bila Mbeleko Simba ni mwepesi sana [emoji4]
 
Naamini Benchika atakuwa amejufunza kitu leo kwa kumchezesha Chama katikati badala ya Saidoo. Chama akili kubwa, utulivu na "team work" lakini Sidoo ubinafsi, papara na juhudi bila akili hata ili "one two" ya goli la pili angekuwa Saidoo haki ya Mungu angefumua shuti ili afunge asifiwe yeye hata timu ikikosa ushindi yeye hajali ilimradi yeye kapata sifa.
 
Mwaka 1938 hapakuwepo timu inaitwa simba katika ardhi ya Tanganyika
 
Sawa Keyboard Coach. Tumekuelewa.
 
Namba 4 na namba 10 hapo umechambua kimuhemko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…