Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
1. Simba ifanye tathmini upya kipindi hiki cha dirisha dogo kuhusu uwezo wa wachezaji wake wa kigeni kama kweli wanaweza kuitetea bendera na heshima ya Simba.Hadi sasa dirisha dogo linafunguliwa leo wachezaji wa kigeni wameshindwa kujitoa na kufikia hata nusu ya Kibu Dennis.
2. Tusione haya kutafuta kocha mwingine kutafuta mbadala wa Fahdu, huyu Simba imemzidi sana.Kwanza upangaji wa kikosi kwake ni changamoto, pili wachezaji wa kucheza aina ya mechi kulingana na ugumu hajui, tatu anamtenga sana kocha msaidizi Seleman Matola na kuwaamini wasaidizi wake wengine ambao hawamsaidii, viwango vya wachezaji vimeshuka sana.
3. Simba tangu mchezo na Bravos kiwango hakibadiliki, timu haijulikani inacheza formation gani ali mradi waganga wanatusaidia kupata matokeo tunaona tuna timu.
4. Niliwahi kutabiri juu ya tabia ya Che Malone kujiamini kupita kiasi, mara anafanya tackling ndani ya penalty box, leo ameingia kwenye timing
5.Wakati umefika sasa Valentine Nouma kuanza ndani ya kikosi chetu, huyu ni silaha ya mwisho ya kocha wetu pale mambo yanapokuwa magumu na kweli ameisaidia sana timu yetu mwanaume huyu wa shoka.
6.Hamza ni beki mmoja anayecheza mpira kwa kupoozesha sana, ndio maana mpira umemshinda Afrika Kusini.Ukimpa mpira tu hana maamuzi ya haraka, anakaa nao weee hadi apigiwe makelele na washabiki nje ndio anatoa pasi.
7.Che Malone anacheza slow, Hamza yuko slow, Ngoma yuko slow, Mavambo yuko slow unaweza kupata matokeo haraka
8.Joshua Mutale awe mchezaji wa kwanza kutupiwa virago dirisha dogo, wa pili ni Mukwara.
9.Sikuona sababu kabisa ya kumtoa Leonel Ateba, Ateba alikuwa anahangaika huku na kule lakini kocha akamtoa kafara kwenda kumuingiza yule kichaa Mukwala.
10.Ni ngumu sana kubeba ubingwa wa Tanzania na huu wa Losers kwa perfomance hii, Ahoua, Mukwara, Ayoub, Ngoma, Mutale, Mavambo watafutieni utaratibu mwingine mpira umeshawashinda vinginevyo muda c mrefu lawama zitawaendea viongozi.
11. Uwanja wa Taifa umekuwa mgumu sana kwetu siku hizi, viongozi angalieni jambo hili kwanini ushindi unapatikana kwa taabu mle wakati uwanja ni wetu.
12. Hakuna mchezaji Simba anayejitoa zaidi ya Kibu, tulikuwa tunalalamika sana kocha kumtoa mwanaume huyu kwa sababu tulikuwa tunaamini ni mtu ambaye anytime anaweza kukufanya ulie na umvamie refa bila sababu kama ilivyo leo.
13.Simba muongezeni yule Gerad Gwalala wa Coastak Union akacheze kiungo ya chini pale kusaidiana na Kagoma, hawa wachezaji wa kigeni wako slow sana na hawana maajabu yoyote.
14.Hata Elie Mpanzu ambaye ni kungo fundi sana anaweza asionekana mzuri kutokana na aina ya uchezaji na ufundishaji wa kocha Fahdu.
15.Tuombe Mungu Constantine ashinde leo huko Angola maana kwa uwezo wa kocha wetu kule Tunisia tunaenda kufungwa, kule Angola tunaenda kufungwa, huwezi kuwa bingwa kwa kushinda nyumbani tu huku ugenini unaliwa utamu.
Soma Pia: Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024
Badilisheni kocha, tusiogope kuchekwa na Yanga kwa sababu tu eti tuliwacheka.Kocha wetu hawezi kutufikisha popote pale.