Passion Lady
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 8,694
- 4,646
Haya haya badon ila sio sana bana....asante in advance Passion Lady
Natumai ulishalala na sasa umeamka
Wale wamefulia Arifu, hawana jipya.... Niaje Aloo?
Mkurugenzi mwenzangu TANMO mbona gazeti letu pendwa linakufa na wewe upo?
Btw: Elizabeth Dominic ameingiavrasmi kwenye bodi ya wakurugenzi.
Poa kaka nipo tu ndani ya jiji la baridi!Wale wamefulia Arifu, hawana jipya.... Niaje Aloo?
Poa Mkuu, wape hi wakezo FP na Preta.......Poa kaka nipo tu ndani ya jiji la baridi!
Ok pouwa kijanaPoa Mkuu, wape hi wakezo FP na Preta.......
Hujambo mdada wangu wa ukweli?Mi naona narudi utotoni
Ngoja nikija Boma nitaruka hapo Chuga, Chap!!!Ok pouwa kijana Karibu chuga!
41. Ukipewa zawadi za kumpelekea mtu, hata gunia la mkaa hulifikishi ! Sanasana waweza lipeleka smolo hausi !........inaendelea
31. Raha unaipata kucheza na wajukuu na sio wanao
32. Ukimwita mwanao Ynnah unasikia 'ah huyu baba nae'
33. Ushamaliza ujenzi,bajeti yako kubwa sasa ni ada za shule
34. Unasahau hata kondomu zinakouzwa maana ukizivaa tu mtambo unalala doro (hii aione Kongosho)
35. Unazaa nje na kuleta mtoto mkeo wala hajali,mshakuwa kama kaka na dada
36. We na ma mkwe mshakuwa paka na panya,una miaka kumi hujamwona
37. Outing yako kubwa na mkeo/mmeo ni kanisani,msikitini,harusini na vilio.
38. Mtu akikwambia ataku 'tweet' unaona kakutukana,facebook unadhania ni uso wa kitabu
39. Mechi za yanga na simba huendi tena kisa unakumbukia enzi za sembuli
40. Kila baya litendwalo na serikali we kazi yako ni kusema 'angekuwepo Nyerere'.
...........itaendelea
1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi
2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani
3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe
4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini
5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala
6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa
7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club
8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei
9. Idadi ya tisheti na jinsi inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo
10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua
11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako
12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi
13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu
14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwapa mabaki uliyotoka nayo Subway ama Steers
15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana
16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala
17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulima lima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura (Kufuga kuku)
18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh' ngapi?"
19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba
20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Express, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani
21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati
22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"
23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati
24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa
25. Ukimwona rafiki yako yu mjamzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"
26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja
27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako
28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei na mfumo mbovu wa utawala
29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi
30. Ukimaliza kusoma kanuni hizo 29 hapo juu unaanza kuhesabu ambazo unaingia wewe.
Ukiona una nusu ya sifa hizi 30 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma
My wife tuu'bi YNNAH , hii mimatirio yote siku zote ulikua umeichimbia wapi? Haya namie niongezee moja, lakini hii ina wahusu wanawake tu, kwa wadada kama Madame B, Preta, Mamndenyi, King'asti , Kipipi Kongosho Usishangae katikati ya game akakuuliza "Maudoudou imeshaanza?" au akakwambia "fanya haraka salon watafunga nataka nikaritachi hujui kesho J'3" anakukata stimu lote!
Za siku nyingi Kongosho.....nakumisi kichizi ujue,jioni njoo protea basi nikupige wine.Ha ha ha ha, hivi wewe una nini? Hapo pekundu hapo, haya tu
Ila hili limenihusu kabisa, 29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi
Mi naona narudi utotoni