Mambo 5 ya thamani kuliko mwili wa mwanamke

Mambo 5 ya thamani kuliko mwili wa mwanamke

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mpendwa Bachelor, Ikiwa sababu kuu ya kuwa mwanamke ni kwa sababu ana kifurushi kikubwa cha mbele aka Manchester united na kifurushi cha nyuma aka Arsenal, basi hauko kwenye MAPENZI. Haijalishi unafikiria nini, ikiwa unaona tu mali yake ya mwili basi UMEPOTEA katika TAMAA. ****************************

Hapa kuna mambo 5 ambayo yatakuwa muhimu zaidi kwa Mwanaume yeyote baada ya Ndoa kuliko yale mambo ambayo kwa asili huwavuta Wanaume kwa Wanawake.

1) AMANI YA AKILI Kabla ya kuoa mwanamke yeyote, kwanza kabisa, anakupa amani ya akili? Je, ana uwezo wa kukupa amani ya akili? Baadhi ya Wanaume hawabaki nyumbani kwa sababu ya mwanamke waliyemuoa. Afadhali walale ofisini au kwa rafiki kwa sababu walioa wababe nyumbani. Nyumba zao ni eneo la vita, mwanamke anakuja na kuweka uadui kati ya mwanamume na watu wa familia yake. Vita kila mahali. Kwamba ana KIFUA KIKUBWA hakuhakikishii atakupa RAHA KUBWA. Ukioa mwanamke kwa mambo hayo, na akageuka kuwa mwanamke msumbufu, hata hutajisikia kuvutiwa naye. Utamchukia na vile vitu vilivyokuvutia kwake. Kwa hivyo tafuta kwanza.

2) MSAADA: Kuna wakati unaweza ukakabiliwa na majaribu na vita kama Mwanaume na utahitaji kuungwa mkono na mke wako, Utahitaji aina ya usaidizi usiotolewa na mwili wake. Bali utahitaji aina ya usaidizi unaotolewa na ubongo wake, kwa mikono yake, kwa roho yake, kwa usawa wa Maarifa yake, kwa ujuzi wake na yatokanayo.
ASS (Kalio kubwa) sio ASSET (MALI).
Mali bora za mwanamke sio za Kimwili ni za kiroho .
Je, anaweza kukusaidia katika maombi?
Je, anaweza kukusaidia kifedha?
Je, anaweza kukusaidia kimwili?
Je, anaweza kukusaidia kwa mawazo, ushauri?
Je, anaweza kujenga na wewe?

3) MTUNZAJI BORA WA NYUMBANI
Mwanamke ambaye hawezi kutunza nyumba yake. Ambaye hawezi kuwa bosi nyumbani na kusimamia rasilimali za mumewe na zake na za watoto kuifanya nyumba kuwa sehemu salama,

Mwanamke ambaye anatoka Ijumaa kwenda Sherehe na anarudi nyumbani akiwa amelewa.

Mwanamke ambaye nyumba yake ni chafu kama dampo.
Huyo hafai ni inapaswa kuwa muangalifu zaidi.

4) USHIRIKIANO
Ikiwa kuna jambo lolote Mwanaume yeyote hapaswi kulifanyia mizaha nalo, ni jinsi mwanamke anavyoshirikiana naye, Hiyo itaamua mengi ya yeye kufanikiwa au la. Jinsi anavyokumbatia maono yake, Jinsi anavyoonyesha uwezo wa KUNYENYEKEA, KUTII na MWAMINIFU. Kuna wanawake (hata Sehemu za Ibada) wanachukia Mamlaka, neno “submission” linawachukiza. Wao kwasababu kwa asili ni wakaidi, waasi, na wanaojitawala. Muoe mwanamke wa namna hii hata kifua chake kikiwa kikubwa kuliko daraja la Mfugale, kiuno chake kimepinda kama mdudu nyigu na mgongo wake mkubwa kama bonde la ufa. Haiwezi chukua hata mwaka mmoja (ukiweza kuvumilia kwa muda huo) utajuta kwa nini uli muoa.
Mwonekano wa Mwanamke wa mwili wake usikuingize katika mtego.

5) ANAYEJALI /ANAYEPENDA
Mwanaume siku zote atahitaji mke wake acheze nafasi ya MPENZI na siku nyingine MAMA Kumjali. Kumwangalia kama mtoto mchanga. Na unapogundua kuwa Mwanamke uliyemuoa hana asili ya kimama, Utaelewa kwa nini watu wetu wanasema kwamba "kakhi no be leather." Kwa hivyo angalia sasa, Anawachukuliaje watoto, anawachukuliaje wazee. Anakuangalia vipi ****************************
Si mimi ninayejaribu kumhukumu Mwanamke yeyote kwa sababu yeye ni mkubwa katika baadhi ya maeneo kuliko Wanawake wengine.

KUWA MAKINI

Angalia ZAIDI ya Mwili na Urembo wa Mwanamke"
 
usiombe mwanamke mchoyo na kiburi , utanyimwa mpaka mapenzi na kila kitu asichokubaliana ni vita na revenge tuu, kwake Ushindi kwa gharama yeyote na kukukomoa ndio anajisikia vizuri
 
Back
Top Bottom