Mambo 5 yanayoweza kudhuru Ubongo wako.

Mambo 5 yanayoweza kudhuru Ubongo wako.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mambo 5 yanayoweza ku Dhuru Ubongo wako.

Kukosa Kifungua Kinywa asubuhi

attachment.php

Watu wanaokosa kifungua kinywa asubuhi wanapata upungufu wa kiwango cha sukari kwenye damu. Hii husababisha upungufu wa madini (nutrients) kwenye ubongo na hatimaye ubongo hudhoofika.
Kula kupita kiasi:
Inasababisha kukaza kwa misuli au mishipa ya Ubongo na hatimaye hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa

fahamu.

Kuvuta Sigara:

Kwenye sigara kuna kitu kinaitwa Nikotini ambayo ndani yake kuna chembechembe ambazo zina sababisha makunyanzi kwenye ubongo na kisha kudhoofu.

Kutumia Sukari nyingi:

Matumizi ya sukari nyingi husababisha matatizo katika mfumo wa unyonyaji wa Protini na Madini joto mwilini na kusababisha ugonjwa wa Utapiamlo ambao pia huingilia mfumo wa fahamu

Kuvuta Hewa chafu:

Ubongo ndio mtumiaji mkubwa wa Oxijeni tunayo ivuta. Unapovuta hewa chafu unapunguza mgawo wa Oxijeni kwenye Ubongo na hatimaye kupunguza ufanisi wake
 
sasa hiyo kifungua kichwa kuna mtanzania anapona hapo?maana wengi hubreak fast saa nne!jamani!
 
Kifungua kinywa cha aina gani manake kama mimi huwa sipendi chai wala sijui mara ya nimekunywa lini? Nimezoea kunywa juice au matunda then nasubiri lunch
 
Kifungua kinywa cha aina gani manake kama mimi huwa sipendi chai wala sijui mara ya nimekunywa lini? Nimezoea kunywa juice au matunda then nasubiri lunch

Safi sana, kifungua kinywa kikiwa ni matunda freshi zaidi, kama unakunywa na juisi ambayo umetengeneza mwenyewe nyumbani freshi zaidi.
 
Kifungua kinywa cha aina gani manake kama mimi huwa sipendi chai wala sijui mara ya nimekunywa lini? Nimezoea kunywa juice au matunda then nasubiri lunch

Mhh we ndo km mimi....hatutofautiani hapo
 
na wale wanaofungulia viroba asuhuhi na mapema je?
 
mkuu matunda na juice ya matunda si kitu kimoja?

Hapana mkuu, kwenye juisi tunaongeza maji au maziwa, sukari na chumvi kidogo wakati matunda tunayala yenyewe kama yenyewe, kwahiyo tofauti ipo. Ukipata vyote viwili i.e juisi + matunda sawa, ukipata kimojawapo pia sawa.
 
Dah sijawai kuchangia hata mara moja kwenye hili jamvi lkn kiukweli post yako imeniacha hoi sana.

Mkuu kipi kilichokufurahisha sana ?
mie nimeongea ukweli mtupu maana hii kitu inatumika sana nshindwa namna ya kuacha
 
Hapana mkuu, kwenye juisi tunaongeza maji au maziwa, sukari na chumvi kidogo wakati matunda tunayala yenyewe kama yenyewe, kwahiyo tofauti ipo. Ukipata vyote viwili i.e juisi + matunda sawa, ukipata kimojawapo pia sawa.

ahsante mkuu..

lakini watu wa economics wanasema kwamba hivyo vitu ni sawa.
 
Hapana mkuu, kwenye juisi tunaongeza maji au maziwa, sukari na chumvi kidogo wakati matunda tunayala yenyewe kama yenyewe, kwahiyo tofauti ipo. Ukipata vyote viwili i.e juisi + matunda sawa, ukipata kimojawapo pia sawa.
Hapana mkuu, kwenye juisi tunaongeza maji au maziwa, sukari na chumvi kidogo wakati matunda tunayala yenyewe kama yenyewe, kwahiyo tofauti ipo. Ukipata vyote viwili i.e juisi + matunda sawa, ukipata kimojawapo pia sawa.
ushauri: usipende kuweka sukari kwenye matunda..kwanini usiache sukari ya matunda yenyewe mfano nanasi lina sukari..tikiti..papai..embe..n.k
 
Ooh kumbe itabidi nihakikishe di miss breakfast masna wengine tumezoea kula branch.
 
mbona wengine nasikiaga wanashauri protein zaidi kwa asubuhi??

Inategemea na afya yako kwa ujumla ipoje na ni kazi gani hasa unaenda kufanya siku hiyo, lakini matunda ni safi zaidi ili kuondoa sumu, kuupa mwili nguvu upya n.k
 
ushauri: usipende kuweka sukari kwenye matunda..kwanini usiache sukari ya matunda yenyewe mfano nanasi lina sukari..tikiti..papai..embe..n.k

Ni kweli hasa kwa matunda yenye sukari nyingi ila kuna matunda bila sukari huwezi kunywa juisi yake. Usisahau pia kuongeza chumvi kwenye juisi yako.
 
Back
Top Bottom