Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji119]Mi nilivoona inahusu namba namba, nikaachana nayo. Sijawahi kumsifu Mwl wangu wa Maths.
Same to me [emoji38]Duh hiyo ya hao ndugu waliogongwa na Taxi moja derava huyo huyo sehemu na abiria yule yule imenishangaza zaidi
Hizo Kanuni unazijua unitajie !? Maana nikifa sitaki kurudi tena ktk huu ulimwengu uliojaa matesoNi imani ya baadhi ya madhehebu ya dini za kiasia, nadhani hata za kiafrika pia. Kwamba ukifa hapa duniani, utazaliwa kiumbe kingine au mtu mwingine hapahapa duniani. Ubora wa kiumbe kijacho hutegemeana na maisha unayoyaishi leo.
Mfano, simba mwema akifa anaweza akazaliwa binadamu mkatili kidogo kama simba, akijitaidi nae akifa anaweza kuzaliwa mtu mwema. Imani hii inaonesha kwamba maisha ni mzunguko tu wa shida duniani.
Kwa imani hii, peponi au paradiso ni kutoweka kwenye huu mzunguko. Kuna kanuni nne zmezaa nane ukizifuata, ukifa mwili wako unatoweka nje ya mzunguko huu wa shida, na kuishi tena kunakoma.
Kuna risasi Alipigwa kichwani kichwa kikafunuka ubongo ukamwagika video zipo YouTube. Mpaka mkewe alikuwa ana hangaika kuokota fuvu la kichwa [emoji22][emoji22][emoji22]Kennedy alipigwa risasi ya shingo, siyo kichwa. Soma vizuri upelelezi wa kufo chake.
Huyu makamo wa Raisi Ina maana alikuwa na power kubwa inayo zuia mpaka agencies za usalama wa taifa kufanya uchunguzi wa kifo Cha Raisi !?Alipigwa Risasi Mbili, moja shingoni ya Kwanza, Na ya pili kichwani. Wanaosema alipigwa Risasi moja ni wale waliotaka kusema Muuaji alikuwa ni mmoja. Ukweli ni Kuwa Makamo wa Rais Lindon Johnson ndiye aliyepanga yale mauaji. Maana J F. Kennedy, Boby F. Kennedy na Martin Luther King Jr wote alikuwa na beaf nao, na wote wafe, tena wote wafe kwa kupigwa Risasi, na kwa kupigwa Risasi na Lone assassin? Probability ya hiyo kuwa ni coincidence, ni ndogo kuliko kupigwa na Radi ukiwa ndani ya Ukumbi wa Senem!
Tazama Zapruder Film, anapigwa Risasi, anajishika shingo, Mkewe anamwatamia, na Kisha anapigwa nyingine Ubongo unasambaza na Mkewessafari hii anapanic anaruka kuokota kipande cha fuvu kilichofumuliwa kutoka kichwa cha Kennedy!
Shikamoo nature [emoji16][emoji16][emoji119][emoji119]Hawa mapacha wa kiume wanaofanana (identical Twins), waliasiliwa (adopted) na familia mbili tofauti mara tu baada ya kuzaliwa
Hizo familia zilizowaAdopt hao watoto zilikuwa hazifahamiani kabisa ila kila Familia ilimpa jina la JIM kwa mtoto waliyemuadopt, Hivyo hao mapacha wote walikuwa na jina la Jim
Baada ya hao wakina Jim kukua, kila mmoja akaamza maisha yake, lakini walikuwa na ufanano huu
1: Wote walijiunga na Law-Enforcement Training
2: Wote walikuwa na uwezo wa Mechanical Drawing na Capentry
3: Wote walioa wake wanaoitwa Linda
4: Wote walipata mtoto wa kiume na kila mtu kwa upande wake walimuita mtoto huyo James Allain
5: Hao mapqcha waliwataliki wake zao wa kwanza (Linda) na kila mtu alioa mke mwingine na huyo mke aliitwa Betty
6: Wote walikuwa wanamiliki mbwa aliyekuwa anaitwa Toy
7: Mapacha hao (Jim Lewis na Jim Springer) walikutana kwa mara ya kwanza mwezi Feb, 9- 1979, ikiwa ni miaka 39 ya kutengana
View attachment 464263
Inatisha na kuhuzunisha clip zipo YouTube [emoji22][emoji22][emoji22] mkewe anaruka kwenda kufuata ubongo uliopo ktk fuvu lililo fumuliwa Kwa risasi [emoji22][emoji22]Daaaaah Mkuu nimeogopa sana pale Kennedy alipopigwa risasi ya kichwa.
Kwa maana hiyo alifumuliwa kichwa chote?
Mungu wangu sikuwa nikijua hili [emoji87]
Kuna kitu kingine cha ajabu mnara qa babeli ulipoangushwa sasa mabaki yake yalikuwa yamejichora kama shape ya pembetatu guwa watu wanaenda kutalii sasa kuna mtaalam mmoja wa majengo sijui wa wap nimesahau kajenga jengo sawasawa na mabaki ya mnara wa babeli.wenyewe wanasema coincidense1. Ozil na Ferrari
Enzo Ferrari mwanzilishi wa ferrari ambaye Kisura anafanana na Mchezaji wa mpira Mesut Ozil alifariki Mwaka ambao Ozil alizaliwa.
![]()
2. Lincoln na Kennedy.
Maraisi wawili wa Marekani waliowahi kupendwa sana Lincoln na Kennedy wote walikuwa na urefu sawa wa futi sita. Wote waliwahi kwenda vitani kabla ya kuwa Marais. Wote walikufa siku ya ijumaa. Wote kwa kupigwa risasi kichwani. wote wakiwa wamekaa pembeni ya wake zao.
![]()
3. Kutabiriwa kwa Titanic.
Miaka 14 kabla ya kutengenezwa titanic, mwandishi wa vitabu Morgan Robertson alitabiri Kuzama kwa Titanic. Kwenye kitabu chake cha Futility, or the Wreck of the Titan alitumia jina la titan kusimulia meli isiyoweza kuzama. Meli ya kwenye kitabu ilikuwa urefu sawa na meli ya ukweli ya Titanic. Meli ya kwenye kitabu cha Robertson ilizama kwa kugonga mwamba wa barafu kwenye Bahari ya Atlantic ya kaskazini, kitu ambacho kilitokea pia kwenye titanic ya ukweli.
![]()
4. Mfalme Umberto I wa Italy
Mfalme Umberto I wa Italy alifahamiana na mumiliki wa mgahawa baada ya kugundua kuwa wote wamezaliwa siku moja, mji mmoja na wote wameoa wanawake wenye majina yanayofanana. Siku chache baadaye wote wakauliwa siku moja sehemu tofauti kwa kupigwa risasi.
![]()
5. Napoleon na Hitler (129).
Adolf Hitler alizaliwa miaka 129 baada Napoleon Bonaparte. alitawala miaka 129 baada ya utawala wa Napoleon. aliivamia Urusi miaka 129 baada ya Napoleon kuivamia Urusi pia. Na aliondolewa madarakani miaka 129 baada ya Napoleon naye kuondolewa madarakani.
![]()
6. Gari la Archiduke Ferdinand.
Kuuliwa kwa Archduke Franz Ferdinand kulifungua rasmi vita ya kwanza ya dunia. Gari alilokuwa amepanda wakati anauliwa lilikuwa na plate number A11-11-18. Vita vya kwanza vikaisha rasimi November 11, 1918 - 11-11-18.
![]()
Three Updates
7. Ujenzi wa Bwawa la Hoover
Ujenzi wa bwawa hili liligharimu maisha ya watu wengi, lakini mtu wa kwanza kufa ni bwana J.G. Tierny, ambaye alifariki December 20, 1922. Mfanyakazi wa Mwisho kufa kwenye huu ujenzi alikuwa Mtoto wa Tierny alikufa siku sawa na siku aliyokufa baba ake miaka 13 baadaye, December 20, 1935.
![]()
8. Video game Iliyotabiri semptember eleven (Twin tower iliyopigwa na Osama)
Video game ya Deus Ex ambayo ilikuwa officially released June 2000. Game hili lilitengenezwa kuakisi maisha ya New york city, lakini katika hatua za mwisho kabisa wakagundua kwamba wamesahau kuyaweka majengo pacha ya biashara (Twin Towers). Ili kukwepa gharama na muda wa kuanza kutengeneza upya ikabidi waandike tu mwanzo wa game kwamba yale majengo yamelipuliwa na magaidi.
![]()
9. Ndugu wawili wa Hamilton
Dereva wa baiskeli yenye injini (Moped) mji wa Hamilton, Bermuda alifariki mwaka 1974 kwa kugongwa na taxi. mwaka ulifuta 1975 eneo lile lile, mdogo wake naye aligongwa akiwa anaendesha baiskeli ya injini, gari iliyomgonga ni ile ile iliyomgonga kaka ake, na cha ajabu kabisa dereva yule yule, na pia alikuwa amebeba abiria yule yule aliyekuwa amemubeba siku anamugonga kaka mtu.
![]()