Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
1.
Moja ya Katiba bora duniani ikilinganishwa na Katiba za nchi mbalimbali duniani kama vile Kenya, Uganda, Uingereza, Marekani
Imejielekeza katika kutatua changamoto za makundi yote katika jamii. Mfano haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu, watoto, wanawake, vijana, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo na wasanii.
2.
Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa ulikuwa wa uwazi na shirikishi
Uteuzi wa wajumbe walioshiriki katika uandaaji ulizingatia uwakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wabunge, wawakilishi kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, watu wenye ulemavu, wanawake, vijana, viongozi wa dini, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo, wasanii, wafanyakazi, waajiri, wafanyabiashara, wasomi n.k.
3.
Katiba Inayopendekezwa inalenga kuimarisha Muungano
Imezungumzia namna itakavyotatua kero za Muungano kupitia uanzishwaji wa Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Sura ya 9, ibara 127 na 128).
Katiba ya mwaka 1977 haikubainisha namna ya kushughulikia kero za Muungano na hivyo Kero nyingi kuchelewa kutatuliwa kwani hakukuwa na mfumo mahsusi wa kutatua kero za Muungano.
4.
Katiba Inayopendekezwa imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira
Sura ya 3 imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira kwa kuzingatia mgawanyo na matumizi bora ya ardhi, fidia, mipaka, na umiliki ili kuondoa changamoto za mapigano na migogoro ya ardhi, maliasili na mazingira. Hii ni fursa ya Katiba Inayopendekezwa kutatua migogoro mingi ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya Sekta hizo.
5.
Katiba Inayopendekezwa imezungumzia misingi ya Utawala Bora.
Ibara ya 6 ya Katiba inaeleza wajibu wa kila mmoja katika uadilifu, demokrasia, uwajibikaji na utawala wa sheria. Jambo hili ni muhimu kwa Utawala wa Nchi na uwajibikaji wa Viongozi katika maendeleo ya nchi.
6.
Katiba Inayopendekezwa imeweka miiko kwa viongozi wa umma na watumishi wa Serikali
Ibara ya 30 na 31 inaelezea namna ya kuwawajibisha viongozi na watumishi wa umma wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Kupitia katiba mpya, vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma vitakomeshwa.
7.
Utashi wa kisiasa wa viongozi kufanikisha upatikanaji wa Katiba mpya
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa, Vyama vya Hiari na Viongozi wa Makundi mbalimbali kama Wanawake, Wazee, Vijana na hata viongozi wa Walemavu kwa pamoja wamedhamiria kupatikana kwa Katiba mpya kwa kusimamia michakato yote kwa mujibu wa sheria. Aidha vyama vya siasa vyenye wabunge na visivyo na wabunge vilishiriki katika mchakato wa Bunge Maaluma la Katiba.