Mambo 7 yanayodhihirisha ubora wa katiba inayopendekezwa.

Mambo 7 yanayodhihirisha ubora wa katiba inayopendekezwa.

aaaa.jpg

hatuzungumzii mambo ya vyama hapa huko ni kuishiwa hoja, tunaangalia mustakabali wa taifa letu tanzania. Uwe mzalendo acha ushabiki usio na manufaa.
 
ukimbiwe wewe simba au chui? Toa hoja ujibiwe.

Katiba pendekezwa ina harufu ya rushwa; Ubabe, na uchakachuaji.
Imekiuka cardinal principal: Muundo wa serikali umekaa vibaya ulilazimishiwa;
muungano na ZNZ sio msitari kutoka kwenye maandiko matakatifu kwamba hauwezi kubadilishwa kulingana na mahitaji ya wakati
Katiba inatufanya watu wa tanzania bara hatuna asili kwa kuikana Tanganyika
Ilipitishwa kwa kura ya wazi na siri; je kura ya maoni itapigwa vipi?
 
MKUU ,HIZI NI id MAALUM KWA KAZI MAALUM..WATETEZI WA KATIBA YA CHENGE WOTE WAMEJIUNGA MWEZI MARCH MWAKA HUU..(SO FAR KATIKA UZI HUU..WHAT A COINCIDENCE)
USISAHAU KUNICHUKIA -Join Date : 15th March 2015
claudiaeliakimu-Join Date : 13th March 2015
UFO_ALIEN- Join Date : 10th March 2015
B-2 STEALTH BOMBER- Join Date : 15th March 2015
USIEMPENDA KAJA- Join Date : 14th March 2015
MWASI MWAKENDA- Join Date : 9th March 2015

MWENDELEZO WA WACHUMIA TUMBO....
CC:kapongoliso, MTK,share ,mwakaboko ,
business-men-green-team-word-23111392.jpg
letter-b-icon.png
green-doll-number-7.gif

Yeah niliusoma mchezo mapema, kinachonishangazaga hawa ni watanzania wenzetu wana watoto, hata kama hawana basi kuna watoto wa ndugu zao na hata wao watajaaliwa watoto siku moja, sasa haiyumkiniki mtu kutetea huu ufedhuli ilhali akijua kabisa wanae au wajukuu watakuja umia siku zijazo..

Very stupid!!
 
Watanzania ni watu waelewa sana Bw. mwakaboko, Jiulize kwa nini wewe ndio unajifanya unawasemea? Unaweza kuwa na document za Katiba Inayopendekezwa au Rasimu lakini uelewa wako ukawa ni mdogo na hivyo kuwapotossha Watanzania. Acha udanganyifu, uwe muungwana na Taifa lako.
Muungwana ni yule anayetetea maslahi ya nchi na sio tumbo lake. Usitake kunidanganya hapa wakati ukweli naujua. Mimi nafahamu kuwa jiwe sio mkate, wewe unataka kuniaminisha kuwa jiwe ni mkate watoto wangu wale tu hakuna shida. Acheni kupotosha. Hebu niambie katika hayo niliyoya post hapo juu lipi halina maslahi kwa Taifa.

Yaani kama wasomi wote tungekuwa kama wewe, basi tungeonekana wote ni wajinga katika mambo yote ila ni wasomi. Nimekwambia kuwa ninazo hizo docs ili usije ukaja na ngonjera za alinacha kuwa sijaisoma. Nimeisoma na kuirudia tena na tena. Kuna vihaki fulani kwa vijana, wanawake na hata wazee vimewekwa, ila mwishowe vikapigwa pini visidaiwe mahakamani hata haki ya elimu haiwezi daiwa mahakamani. Au mwenzangu umekaririshwa!!!!! kitu chenyewe huna na hujakisoma?
 
nawe unahangaika sana na hao waliokutuma wakati nyote mnajua ukweli wa uzuri wa hii katiba. Pole sanan ujumbe umekufikia, ndo basi tenaaaaaa
Yaani umeonesha namna gani ulivyo na uelewa mdogo wa mambo, read between the lines, you will understand my ujumbe. Kwa sababu wewe unatumwa unadhani kila aliyepo hapa jukwaani katumwa kama wewe. Can't we learn from the past!!!!
 
yeah niliusoma mchezo mapema, kinachonishangazaga hawa ni watanzania wenzetu wana watoto, hata kama hawana basi kuna watoto wa ndugu zao na hata wao watajaaliwa watoto siku moja, sasa haiyumkiniki mtu kutetea huu ufedhuli ilhali akijua kabisa wanae au wajukuu watakuja umia siku zijazo..

Very stupid!!

hawa watu ni wanufaikaji na mfumo uliopo..haiwezekani ''mastermind'' adraft katiba....baada ya miezi kadhaa anaitwa kwenye kamati ya maadili ...upuuzi mtupu...
 
Yeah niliusoma mchezo mapema, kinachonishangazaga hawa ni watanzania wenzetu wana watoto, hata kama hawana basi kuna watoto wa ndugu zao na hata wao watajaaliwa watoto siku moja, sasa haiyumkiniki mtu kutetea huu ufedhuli ilhali akijua kabisa wanae au wajukuu watakuja umia siku zijazo..

Very stupid!!

kama wao si jamii ya mafisadi basi ni wale watanzania wachache wenye funza kwenye ubongo
 
ha ha ha ha ha katiba ya chenge imetulia kwa wapiga dili. Nchi imeshakwisha hii na hiyo katiba inayopendekezwa ni ya kugawana mbao. Mamlaka yote ya wananchi imenyofolewa na fisi wala watu bila huruma. Maadili hamna, uwajibishaji hamna, madaraka ya rais mfalme yameongezwa, tume ya uchaguzi ni ya chama kimoja, maslahi mapana ya wakulima hayajazingatiwa, wopora ardhi ndio wamepewa kipaumbele, hamsini kwa hamsini si ya mwanamke wa kitanzania kule kijiji bali ni ya wake za mafisadi, binti zao, michepulo yao, endelea kutaja uchfu wa katiba inayopendekezwa na joka makengeza chenge na binamu yake sita.
Umesema ukweli ambao unauma kwa wazalendo wa Kitanzania. Maana wengine ni viongozi wetu lakini uzalendo hakuna kabisa. Watu wote waelewa wanajua ile iko pale kulinda makundi fulani katika nchi hasa watu aina ya Chenge
 
kama unavyo sasa unabisha vitu gani kuhusu katiba inayopendekezwa? Ukweli unauma eeenh??? Message sent katiba hii ni ndiyooo tu coz imecover kila kitu, huna jipya la kuniconvince nkakuelewa, kaisome katiba uielewe then ndo uje na hoja zenye mantiki.

Alafu unatakiwa uelewe kwamba tatizo sio hayo yaliyomo tu ndio utuambie eti katiba ninzuri,tatizo niyale yaliyoondolewa hasa yanayowagusa viongozi na badala yake wanatuletea mambo eti ya usawa wa kijinsia kupata nafasi asilimia sawa.Hatupo kwenye mashindano ya urembo au komborela mkuu tunatafuta Muarobaini wa Ujenzi wa Taifa letu linalohusu vizazi vyote bila kujari itikadi,rangi,umri,jinsia nk.
 
hivi wewe mwakaboko mbona umekuwa mbogo? Kitu gani hujakielewa katika katiba inayopendekezwa ili ujibiwe? Naona unajibu kwa hasira hasira tu, katiba imaetulia naamini majibu unayo ila unaona aibu kukubali ukweli wa haya mambo, kuwa muwazi tukuelewe bhana.
Read betwen the lines in my post, you will understand my message. Ila kama unaisoma ukiwa na mihemko unaondoka na sifuri
 
wewe kijana uwage muelewa, toa hoja mbona hueleweki? toa 7bu zako ambazo zinakufanya uipinge hiyo Katiba then ujibiwe hizo hoja sio kulalamika lalamika tu bila msingi.
Pole pole ndg yangu, mimi sio kijana kama unavyofikiri. Mwenzako alisema nimejeli/ nimetukana nikamwambia ahighlight hayo matusi/kejeli kimya mpaka sasa. Nimeandika mapungufu ya hiyo katiba pendekezwa hapo, na hiyo ni sehemu tu, I think you have your own agenda and a not national agenda. Read between the lines or else keep quiet . Can't we learn even from the past!!!
 
kaka kasome katiba inayopendekezwa upate majibu ya hoja zako zisizo na mantiki ulizoziweka hapo juu, sasa kumbe katiba zote unazo, unachokaidi kitu gani? Kila majibu ya maswali yako yapo au umetumwa na ukawa au? Soma uelewe kama huna kazi pumzika ulale, huku hapakufai maanake kazi yako ni kuzungumza mabaya tu inamana hakuna mazuri ndani ya hiyo katiba?
TENA hufahamu, fahamu sasa kuwa wewe sio mzalendo wa kweli. Mzalendo wa kweli hawezi shabikia Taifa lake kuangamizwa na watu wachache ambao anawafahamu kuwa ni wezi ila kwa kuwa wamempa shekeli anaona hakuna shida. Yaliyoondolewa ni mihimili katika Taifa lolote la waungwana. Bila hata haya unasema eti nikalale ratiba yangu ya kulala unaijua wewe. Mwenye mamlaka ya kuniambia nikalale ni Mungu, maana Yeye ndiye ajuaye nitalala lini, sio wewe. Acheni kupotosha wananchi na kushabikia nchi kuibiwa au nawe ni ukoo mmoja na wazee wa escrow kwa hiyo unaona tunakuzibia ulaji mchana kweupe peeeeeeeeeeeee!!!
 
1.
Moja ya Katiba bora duniani ikilinganishwa na Katiba za nchi mbalimbali duniani kama vile Kenya, Uganda, Uingereza, Marekani
Imejielekeza katika kutatua changamoto za makundi yote katika jamii. Mfano haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu, watoto, wanawake, vijana, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo na wasanii.
2.
Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa ulikuwa wa uwazi na shirikishi
Uteuzi wa wajumbe walioshiriki katika uandaaji ulizingatia uwakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wabunge, wawakilishi kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, watu wenye ulemavu, wanawake, vijana, viongozi wa dini, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo, wasanii, wafanyakazi, waajiri, wafanyabiashara, wasomi n.k.
3.
Katiba Inayopendekezwa inalenga kuimarisha Muungano
Imezungumzia namna itakavyotatua kero za Muungano kupitia uanzishwaji wa Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Sura ya 9, ibara 127 na 128).
Katiba ya mwaka 1977 haikubainisha namna ya kushughulikia kero za Muungano na hivyo Kero nyingi kuchelewa kutatuliwa kwani hakukuwa na mfumo mahsusi wa kutatua kero za Muungano.
4.
Katiba Inayopendekezwa imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira

Sura ya 3 imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira kwa kuzingatia mgawanyo na matumizi bora ya ardhi, fidia, mipaka, na umiliki ili kuondoa changamoto za mapigano na migogoro ya ardhi, maliasili na mazingira. Hii ni fursa ya Katiba Inayopendekezwa kutatua migogoro mingi ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya Sekta hizo.
5.
Katiba Inayopendekezwa imezungumzia misingi ya Utawala Bora.
Ibara ya 6 ya Katiba inaeleza wajibu wa kila mmoja katika uadilifu, demokrasia, uwajibikaji na utawala wa sheria. Jambo hili ni muhimu kwa Utawala wa Nchi na uwajibikaji wa Viongozi katika maendeleo ya nchi.
6.
Katiba Inayopendekezwa imeweka miiko kwa viongozi wa umma na watumishi wa Serikali
Ibara ya 30 na 31 inaelezea namna ya kuwawajibisha viongozi na watumishi wa umma wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Kupitia katiba mpya, vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma vitakomeshwa.
7.
Utashi wa kisiasa wa viongozi kufanikisha upatikanaji wa Katiba mpya
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa, Vyama vya Hiari na Viongozi wa Makundi mbalimbali kama Wanawake, Wazee, Vijana na hata viongozi wa Walemavu kwa pamoja wamedhamiria kupatikana kwa Katiba mpya kwa kusimamia michakato yote kwa mujibu wa sheria. Aidha vyama vya siasa vyenye wabunge na visivyo na wabunge vilishiriki katika mchakato wa Bunge Maaluma la Katiba.

katiba ya nchi haipaswi kuwa na vipengele 7 tu ambavyo ni bora bali inabidi kila kitu kilichomo kiwe bora na itoke kwa wananchi kweli
 
Katiba pendekezwa ina harufu ya rushwa; Ubabe, na uchakachuaji.
Imekiuka cardinal principal: Muundo wa serikali umekaa vibaya ulilazimishiwa;
muungano na ZNZ sio msitari kutoka kwenye maandiko matakatifu kwamba hauwezi kubadilishwa kulingana na mahitaji ya wakati
Katiba inatufanya watu wa tanzania bara hatuna asili kwa kuikana Tanganyika
Ilipitishwa kwa kura ya wazi na siri; je kura ya maoni itapigwa vipi?

Kama huna hoja kaka pumzika tuu ndugu yangu, hayo maneno tu hata kwenye khanga yamo! Katiba ni nzuri, isome uielewe.
 
1.
Moja ya Katiba bora duniani ikilinganishwa na Katiba za nchi mbalimbali duniani kama vile Kenya, Uganda, Uingereza, Marekani
Imejielekeza katika kutatua changamoto za makundi yote katika jamii. Mfano haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu, watoto, wanawake, vijana, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo na wasanii.
2.
Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa ulikuwa wa uwazi na shirikishi
Uteuzi wa wajumbe walioshiriki katika uandaaji ulizingatia uwakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wabunge, wawakilishi kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, watu wenye ulemavu, wanawake, vijana, viongozi wa dini, wazee, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo, wasanii, wafanyakazi, waajiri, wafanyabiashara, wasomi n.k.
3.
Katiba Inayopendekezwa inalenga kuimarisha Muungano
Imezungumzia namna itakavyotatua kero za Muungano kupitia uanzishwaji wa Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Sura ya 9, ibara 127 na 128).
Katiba ya mwaka 1977 haikubainisha namna ya kushughulikia kero za Muungano na hivyo Kero nyingi kuchelewa kutatuliwa kwani hakukuwa na mfumo mahsusi wa kutatua kero za Muungano.
4.
Katiba Inayopendekezwa imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira

Sura ya 3 imebainisha suala la ardhi, maliasili na mazingira kwa kuzingatia mgawanyo na matumizi bora ya ardhi, fidia, mipaka, na umiliki ili kuondoa changamoto za mapigano na migogoro ya ardhi, maliasili na mazingira. Hii ni fursa ya Katiba Inayopendekezwa kutatua migogoro mingi ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya Sekta hizo.
5.
Katiba Inayopendekezwa imezungumzia misingi ya Utawala Bora.
Ibara ya 6 ya Katiba inaeleza wajibu wa kila mmoja katika uadilifu, demokrasia, uwajibikaji na utawala wa sheria. Jambo hili ni muhimu kwa Utawala wa Nchi na uwajibikaji wa Viongozi katika maendeleo ya nchi.
6.
Katiba Inayopendekezwa imeweka miiko kwa viongozi wa umma na watumishi wa Serikali
Ibara ya 30 na 31 inaelezea namna ya kuwawajibisha viongozi na watumishi wa umma wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Kupitia katiba mpya, vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma vitakomeshwa.
7.
Utashi wa kisiasa wa viongozi kufanikisha upatikanaji wa Katiba mpya
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa, Vyama vya Hiari na Viongozi wa Makundi mbalimbali kama Wanawake, Wazee, Vijana na hata viongozi wa Walemavu kwa pamoja wamedhamiria kupatikana kwa Katiba mpya kwa kusimamia michakato yote kwa mujibu wa sheria. Aidha vyama vya siasa vyenye wabunge na visivyo na wabunge vilishiriki katika mchakato wa Bunge Maaluma la Katiba.
Hamfrey polepole
Naomba uje huku bro.
 
Last edited by a moderator:
katiba ya nchi haipaswi kuwa na vipengele 7 tu ambavyo ni bora bali inabidi kila kitu kilichomo kiwe bora na itoke kwa wananchi kweli

Kweli wewe hujaisoma na hujaelewa kitu hapo, hizo ni baadhi ya sehemu ama vipengele muhimu vilivyomo kwenye Katiba hiyo, sio kwamba viko hivyo tuuu, dah kusoma kumbe ni shidaaah eenh! duh rudi darasani tena kwanza.
 
Katiba iliyoandikwa na wezi.... .mafisadi......wala rushwa........unategemea iwe safi???........ipo kimasrahi ya mafisadi kuwatanulia mianya yao ya kula fedha za walala hoi...... Am sorry mr. Chenge Vijisenti...
 
Back
Top Bottom