Mambo 8 Ambayo Huenda Hukuyajua Kuhusu Mila na Desturi za Jamii ya Wamaasai

Kuna ile Mila ya mwanaume kuchomeka mkuki kwenye nyumba ya mwanaume mwenzako wakati unamlia mke wake,naomba ufafanuzi.
Na jirani yangu mmasai ana bonge la mke.
Nimeshanunua mkuki tayari.
ucjaribu watakupdidy.
 
Kuna ile Mila ya mwanaume kuchomeka mkuki kwenye nyumba ya mwanaume mwenzako wakati unamlia mke wake,naomba ufafanuzi.
Na jirani yangu mmasai ana bonge la mke.
Nimeshanunua mkuki tayari.
Mkuu; hiyo mila ilikuwepo zamani sana. Utaratibu wa hicho kitendo ilikuwa ;
1. Mkuu wa boma(nyumba/mji) lazima awe ni rafiki yako wa karibu sana.
2. Mwanamke (Yeyoo) wa boma lazima awe alikwisha kukuona na anatambua urafiki wako na mme wake.
3. Mwanamke mlengwa shart awe ameridhia jambo hilo.Vinginevyo atakuumbua i.e. atamweleza mme wake.
Tofauti na hapo 1-3,mnzehe ukikutwa utacharangwa sime kama nyama ya buchani.
Siku hizi hiyo mila haipo kabisa na wala usije ukathubutu kujaribu - ukipona bahati yako.
Halafu ujue kuna maambukizi ya VVU na hatimaye UKIMWI; Gonorrhea, Syphilis, UTI, etc. etc.
NB: Nakushauri ww endelea kutunza mkuki wako kwani utakufaa sana siku wakija wale wasiojulikana.
 
Nilienda Parakuyo, huko Kilosa, nikakaa mwezi mzima Wamasai ni wabaguzi sana, hawataki mtu asiye Maasai ajenge kijijini hapo
Sawa. Unajua ni kwa nini mkuu?
Majibu haya hapa:
1. Mtu asiye maasai; wenyewe wanamwita mswahili (Olumeek') ni msumbufu, mjanja-mjanja, muongo-muongo hv, haaminiki, ni mjeuri, mshari-mshari na kigeugeu (imbelekenya naaleng') sana n.k.
2. Wamaasai wengi ni wafugaji au wanapenda mifugo zaidi na kwa mtindo wa Ufugaji Huria. Mifugo inahitaji nafasi/eneo kubwa lisiloingiliwa na shughuli nyingine pinzani za kiuchumi e.g. kilimo cha mazao.
3. Mfumo wa maisha umasaini ni mfumo dume. Wanawake, kwa utaratibu hawawezi kuchanganyikana na wanaume kirahisi na ni watu wa kupewa maelekezo na amri tu.(Siku hizi kuna ka-unafuu kidogo). Katika mfumo huo, mtu asiye maasai ni vigumu kuufuata na mara nyingi ataonekana ni mvurugaji - Mleta fujo.
4. Familia za maasai ni extended family na huishi wengi kwa pamoja ndani ya nyumba moja kwa mahusiano ya undugu. Watoto huweza kuingia nyumba yoyote miongoni mwa nyumba zilizopo hapo kwenye boma na kupata huduma sawa na watoto wengine eneo hilo. Kwa mtu asiye maasai, hiyo ni ngumu sana. e.g. Umasaini viboko hutumika kuadabisha watoto na akina mama rika zote.. Je, asiye maasai atavumilia na kukubaliana na hilo?e.g. Unarudi kutoka kwenye mihangaiko yako huko halafu ukifika nyumbani unamkuta mkeo kalambwa bakora za kutosha; kisa hakusalimia wazee au alikuwa anaongea-ongea wakati wazee wanatafakari jambo fulani au mwanao amechapwa sana kwa kisa cha kufukuza mbuzi kwenye shamba la mswahili.
 
Hivi Kuna wachawi wa kimasai?
 
Hivi Kuna wachawi wa kimasai?
Hapana. Wapo wale wanaoaminika ni wenye kijicho au jicho baya (Eeta engang'u). Kwa mfano akiwatazama ndama wako, hao ndama au ng'ombe wataanza kudhurika, kukonda na hatimaye hufa. Kinga au ili kuzuia madhara hayo wanatumia njia ya kuwapaka ng'ombe matope (mavi na mkojo wa ng'ombe hao) yaliyochanganyika na udongo wa humo zizini wanakolala.
NB: Usisahau kutofautisha kati ya Wamaasai na Waarusha japo lugha zao zinafanana kwa kiasi kikubwa sana.
 
Wàarusha ndio wachawi?
 
Back
Top Bottom