SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Binadamu tumeumbwa kusahau. Ngoja niwakumbushe mambo mawili matatu ambayo yaliibadilisha Simba kutoka katika mkwamo iliokuwa nao.
1. Tunasahau Simba ilikuwa inacheza hadi dakika ya 60 inakata moto. Tukalilia fitness za wachezaji. Sasa hivi hakuna anayeongelea tatizo la fitness. Tatizo lililobaki ni wachezaji kuogopa majeraha maana imeonekana ama kitengo cha utabibu Simba kina mapungufu au wachezaji wamegundua hawathaminiwi tena pale wanapotoka kwenye majeraha. Hili limewaathiri sana kisaikolojia wachezaji wa Simba.
2. Tunasahau kuwa kabla ya ujio wake, Simba ilifika kipindi ilikuwa haiwezi kupiga hata pasi 3 bila kupoteza mpira. Kaangalie mechi ya juzi na Yanga, kaangalie mechi zote mbili za mwisho dhidi ya Al Ahly, sasa hivi timu kiasi fulani inaridhisha kwenye eneo hilo. Inakosa mtu sahihi pale mbele wa kutumia nafasi. Angepatikana huyo mtu hata confidence na ufanisi wa mawinga na viungo ungeongezeka maana wangejua wana mtu wa maana pale mbele. Wachezaji wa Simba bado hawawaheshimu Jobe na Freddy.
3. Benchikha ameipa Simba ujasiri wa kutoka kwenye utegemezi wa wachezaji fulani tukianza kwa Manula ambaye rotation ya makipa ilimu expose akaamua kujivunja, leo hii hakuna mwenye mashaka na Ayoub tofauti na golini akikaa Manula au Salum. Tukaja kwa Bocco, huyu alikuwa anaachwa kwenye safari nyingi za nje hadi akasoma alama za nyakati, naye alipoona vipi akajivunja. Muda ungeruhusu na angekuwa na kikosi kipana naamini wote wangefikiwa.
4. Hili siliweki kama ni fanikio ila anaweza kuwa ametufumbua macho na likifanyiwa kazi linaweza kuzaa matunda kuliko wengi wanavyotegemea. Wanasema "Changamoto ni mama wa uvumbuzi". Hapa naongelea kitendo cha kumtumia Kanoute kama striker. Huyu jamaa ana urefu sahihi na anajua kupiga mashuti. Simba ikifanyia kazi wazo la kumhamishia pale mbele naye akajizoeza kucheza hapo hasa kukaa sehemu sahihi anaweza kuwa chaguo la 1 au la 2 kwenye nafasi hiyo na hawezi kushindwa kuipa Simba magoli 10-12 kwa msimu.
NINAPOMLAUMU:
1. Kutomtumia ipasavyo Miquissone hata pale anapoonyesha msaada kwa timu.
2. Kuacha kuwatumia madogo kama Karabaka na Chasambi. Nadhani baada ya kuwa disappointed na kuletewa kina Jobe, alifanya makusudi kuwafunika hata wale alioletewa wenye uafadhali ili aonyeshwe kutoridishwa kwake kwa wale ambao hakuwataka hasa kwenye position muhimu kama striker (ili anaowalaumu kwa kuwaleta kina Jobe wasije sema mbona yule na yule pia tumewaleta na wanakusaidia) hadi akaanza kuwaweka mastriker wote wawili nje. Hapa alitufanyia uhuni mkubwa.