Mambo aliyoyafanya Rais Samia Suluhu yanayomgusa moja kwa moja Mtanzania

Mambo aliyoyafanya Rais Samia Suluhu yanayomgusa moja kwa moja Mtanzania

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Haya ni baadhi ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan;

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi sana likiwemo lile la elimu bure kutoka primary mpaka advance pia amesema kwa wanafunzi wa kidato cha sita watakao faulu vizuri masomo ya sayansi watapata ufadhili wa masomo ya chuo kikuu (scholarship) kwaiyo tunaona mtoto akiweka bidii anaweza kusoma from primary to university bure tumuombee Rais Samia suluhu Hassan maisha marefu zaidi.

Rais Samia amewezesha suala la kupunguzwa tozo katika miamala ya simu katika kutuma na kupokea fedha kwa zaidi ya 40%. (Tozo ya juu kabisa itapungua kutoka 7000 hadi 4000).

Kwa kutambua ukuaji wa sekta ya Sanaa na kujiajiri kwa vijana, Rais amewezesha kupunguzwa kodi(with holding tax) katika Tasnia ya Filamu kutoka 15% hadi 10%.

Kwa kutambua kupanda kwa bidhaa katika Soko la Dunia, Rais amewezesha kuondolewa kwa kodi (Zero rating) kwa bidhaa za mafuta ya kula (edible oils).

Kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Kilimo, Rais amewezesha kuondolewa kwa kodi (Zero rating) kwa mbolea inayozalishwa hapa nchini na mahitaji mengine muhimu ya wakulima, Wafugaji na Wavuvi.

Asante sana mama kwa kutujari watanzania
 
Pia la Traffic usumbufu wa Traffic lililotatuliwa ongeza
Ilitakiwa uliweke namba moja ndio uweke hayo mengine
 
--Hizo tozo za Miamala ziliwekwa na Nani?
Na aliyezipunguza ni Nani?

--Kuhusu elimu bure tangu enzi za mwendazake zilikuwapo.

Weka hoja zingine mpya.
 
Kaleta nyongeza ya shilingi 8000/= kwa watumishi
Lakini kawainua watumishi waliokua na mishahara midogo sasa mtu anapokea 5m anataka aongezewe sawa na wa 300k Lengo la Rais Samia Suluhu ni kuwainua wale wenye mishahara ya chini
 
--Hizo tozo za Miamala ziliwekwa na Nani?
Na aliyezipunguza ni Nani?

--Kuhusu elimu bure tangu enzi za mwendazake zilikuwapo.

Weka hoja zingine mpya.
Kupitia izo tozo Rais Samia Suluhu amekamilisha maboma 560 ya vyumba vya madarasa katika shule za sekondari ambapo shilingi bilioni 7.0 zilitolewa.
 
Alipewa maelekezo aanzishe mchakato wa katiba mpya Ili UCHAGUZI wa serikali mitaa uwe chini ya katiba mpya hapo 2024 na hilo Ndio takwa la wananchi Wenye NCHI!!

Cha ajabu akalopoka eti katiba Sio kipaumbele kwake bali maendeleo!wakati katiba Ndio maendeleo YENYEWE,Akatangaza rasmi kuwa 2025 atagombea na akaanza kuwashughulikia wapinzani wake KWA kuwaondoa kwenye uwaziri eti wajiandae VIZURI KWA mapambano!!!


Je ana uhakika gani 2025 itafika yeye akiwa BADO ni Rais!?Ameweka makubaliano na Mungu!?Mtangulizi wake alishinda lakini Mungu akamuita je yeye ana uhakika gani!!?


Kama mnampenda kama Mimi nimpendavyo mwambieni amrudishe Warioba mchakato uanze Rasmi na apige chini kikosi kazi cha mchongo cha walamba asali!Mwambieni NCHI ina wenyewe hii sio yake ya kujifanyia atakavyo!!Mwambieni walamba asali wanampoteza kabisa na kufanya too late yake isiwe beyond Muda wa makubaliano na waliompa MAAGIZO!!

Refference; Operation Imesitishwa the state wamesema apewe Muda! Uzi wa Tumia akili!

Ndio màana Mimi KWA upendo kabisa NIMEKUWA nikiimba na Koo langu halitokauka kamwe kwamba;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe katiba mpya"!

Na kama anaona hawezi kufata maagizo ni simple tu achukue hii Hapa;-

"Samiah jiuzulu Sasa nchi imeshakushinda ulambaji asali umekuponza"!

Kiroho safi KABISA!!
 
Mama Samia kitu ambacho hawezi sahaulika uongozi wake ni kumaliza Kero za Traffic hizo Kero Nyerere, Mwinyi ,Mkapa,Kikwete na Magufuli wote walishindwa kutatua hiyo Kero.Mama Samia kaweza.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni .Mama Samia kaweza
 
Mama Samia kitu ambacho hawezi sahaulika uongozi wake ni kumaliza Kero za Traffic hizo Kero Nyerere, Mwinyi ,Mkapa,Kikwete na Magufuli wote walishindwa kutatua hiyo Kero.Mama Samia kaweza.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni .Mama Samia kaweza
Rais Samia amefanya mambo mengi mazuri anastahili pongezi
 
Pia la Traffic usumbufu wa Traffic lililotatuliwa ongeza
Ilitakiwa uliweke namba moja ndio uweke hayo mengine
Mama kazi yake ni kutekeleza ni msikivu anatusikiliza zaidi wananchi na ametekeleza kelo yetu ya matraffic vizuri kama umejua ilo
 
Usisahau na kututangazia 23%. Tangazo lilimguza kila Mtanzania. Nimesema tangazo lakini
Lakini wenye mishahara midogo wamenufaika lengo ilikua ni kuwainua wenye mishahara midogo
 
Lakini kawainua watumishi waliokua na mishahara midogo sasa mtu anapokea 5m anataka aongezewe sawa na wa 300k Lengo la Rais Samia Suluhu ni kuwainua wale wenye mishahara ya chini
Angeondoa marupurupu ya wabunge kwanza, ndio uzalendo
 
🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom