Mambo ambayo hutakiwi kuchelewa kwenye maisha kama tayari una mpango wa kufanya jambo husika

Mambo ambayo hutakiwi kuchelewa kwenye maisha kama tayari una mpango wa kufanya jambo husika

Kwakwel kuna time nikiwa na wadau maeneo flan huwa kabisa naona nawakata stimu kwakua sigongi vyombo. Sema ndio hivyo na wao wameshanikubali tu kuwa mwamba tulishamkosa so wananichukulia vile nilivyo tu

Sasa hiyo unatakiwa uwe mtu muongeaji na mwenye stori ukiwa mkimya alafu hunywi Hali inazidi kuwa ngumu kwa marafiki
 
MAMBO AMBAYO HUTAKIWI KUCHELEWA KWENYE MAISHA KAMA TAYARI UNAMPANGO WA KUFANYA JAMBO HUSIKA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Leo sitawachosha ndugu zangu. Nitashusha vitu kisha nitawaacha mkitatafakari kwenye weekend hii.

Kwenye akili yako kuna mambo yanaendelea, kuna mambo unayawaza kuhusu maisha yako. Hiyo ni kawaida Sana. Kuwaza Sana wakati mwingine huondoa Ari na shauku ya kutekeleza. Kuwaza Sana wakati mwingine huondoa uthubutu.

Basi wakati unawaza, yafuatayo ni mambo ambayo hupaswi kuchelewa kuyafanya ikiwa tayari yapo Katika mawazo yako;

1. Usichelewa kuamua shughuli ya kukuingizia kipato.
Ukishafikisha miaka ishirini tayari akili yako itaanza kukosa utulivu ikifikiria kipi ufanye.
Hapa kuna njiapanda mbili, mosi, shughuli unayoipenda Versus shughuli iliyopo mbele yako.
Usichelewa kufanya maamuzi ya nini chakufanya kwenye maisha kitakachokuingizia kipato.
Ukifikisha miaka 25 uwe ushafanya maamuzi ya nini utafanya, kisha miaka mitano jifunze na pata ujuzi wa kufanya kitu hicho. Miaka 30 uwe na uzoefu na kitu ambacho unafanya. Usichelewe.

2. Usichelewe kuanzisha familia na kuwa na watoto.
Hapa sizungumzii kuzaa kama mbwa na kutelekeza watoto kwa watu wengine kanakwamba wewe umefariki.
Nazungumzia kuanzisha familia ambayo utakuwa nayo bega kwa bega, unaiangalia, na inakutazamia wewe.

Ukifikisha miaka 25 Hakikisha ushaseti mitambo yako ya ku- launch familia yako. Miaka 30 angalau uwe na mtoto Mmoja kama kijana wa kiume. Wakati kwa Binti miaka 30 angalau uwe na watoto wawili.

Hakikisha watoto wako wakukute ukiwa kijana mwenye nguvu, ukivaa nguo zinakukaa, ukisuka nywele na kufumua ni nyeusi tii. Hiko ni Kipindi sahihi kwako kulea watoto na malezi hayatakusumbua Sana kwa sababu utakuwa na nguvu na shauku.
Labda uwe na shida ya uzazi lakini kama hauna usichelewe kuanzisha Familia.

Miaka 20-40 ni umri wa kujitafuta kwa maeneo Mengi sio tuu kujitafuta kiuchumi Bali hata kwenye mambo ya familia. Ndio wakati sahihi wa kuitafuta familia yako.

Ndio wakati pekee ambao wewe na Mkeo/Mumeo mtaweza kufanya mambo yote ya ujana pamoja ikiwezekana na watoto wenu kwa pamoja mkiwa na furaha.

Unapochelewa kuanzisha familia hata ukiwa na pesa kuna mambo utayajutia na hayatakupa furaha Ile ya ndani kabisa.

Kila Jambo na wakati wake.
Kuna wakati wa kusoma, kuna wakati wa kujitafuta na kuanzisha familia, kuna wakati wa kulea watoto wadogo, kuna wakati wa kusomesha.
Hata hivyo kuna wakati itakupasa ufanye mambo mawili Mpaka matatu kwa pamoja.

Ukifikisha miaka 50+ angalau watoto wanatakiwa wawe wamefika mbali. Yaani kwa Lugha nyepesi ni kuwa upara au wakati mvi zinaanza kukutoka inatakiwa baadhi ya kete ziwe zimefika mbali.
Sio unazaa mtoto wakati mvi na upara umekujaa kichwani. Labda kama ulikuwa unaumwa au unamatatizo ya uzazi.
Mtoto akizaliwa akikukuta na mvi au upara hawezi kukuchukulia kama Baba isipokuwa Babu. Na hiyo Sio HEKIMA.

Hautaifurahia familia yako kama utavunja protocols za kifamilia na kimahusiano. Na familia yako haitakufurahia.
Kwa sababu mambo yasipofanyika kwa wakati heshima na uzuri wake hupungua.

Najua vijana watasema hakuna Pesa. Maisha hayaendeshwi na Pesa. Maisha yanaendeshwa na imani na uthubutu hila kukata tamaa. Maisha mazuri na yaheshima ni kufanya vitu kwa wakati na kwa usahihi.

Fikiria uhangaike Kutafuta pesa Muda uende ndipo uanzishe familia alafu unapata pesa unajikuta nguvu za ujana za kumfurahisha Mkeo hauna.
Au meno ya kula nyama huna. Hapo ndipo utayaona maisha hayana maana kabisa.

Najaribu kusema, kila Jambo linamuda wake. Kuanzisha familia hakukuzuii wewe kutafuta pesa ikiwa utapata mtu sahihi. Nasisitiza, mtu sahihi.

3. Usichelewe kuingia kwenye siasa kama unandoto za kuwa kiongozi.
Unajua kabisa unataka siku Moja uwe diwani, au Mwenyekiti au mbunge lakini mpaka unafikisha miaka 25 hujajiunga na chama chochote. Maifurendi hauko sahihi.

Jiunge kwenye siasa. Jenga mtandao, pata uzoefu. Hii itakusaidia mbeleni kutimiza malengo yako.

4. Usichelewe kufanya Drama, Sanaa na michezo Mitandaoni.
Usiishi maisha ya watu wengine. Maisha ni yako.
Wakati tunasoma, tukiwa vijana kuna wanafunzi walikuwa wanaona haya kufanya Sanaa na drama shuleni. Sio kwamba walikuwa hawapendi, Bali wengine aibu, wengine bendera fuata upepo, wengine umaskini wa akili n fikra.

Sisi wengine kina Taikon mambo yote ya shule tulifanya, midahalo tumefanya, talent show tumefanya, kwenda kwenye mipira na trips za shule tumeenda, madisko ya shule tumecheza, showoffs za kutembea na warembo wa shule tumefanya Sana.

Graduation za shule zote tulicheza, yaani lazima tushiriki hasa kwenye matukio ya muziki na kubang.
Yaani kiufupi maisha ya shule yalikuwa matamu Sana na tuliishia.
Chuo nako hivyohivyo.
Hayo ndio maisha.

Maisha ni Sanaa. Hayawezi kuwa matamu bila Sanaa na burudani. Kuwa kwako serious hakuongezi chochote kwenye furaha yako.

Kama wewe sio mtu wa showoff na Mitandaoni kama Sisi. Haimaanishi usiende Clubs, Casino, nenda ukaenjoy maisha huko mbuzi wewe. Muda ni mchache ndugu yangu.

Sio Muda utaona ujana ulipita haukuufurahia alafu ukiambiwa nini ulikuwa unafanya utabaki umeduwaa.

Fanya Drama, igiza maisha ambayo unayatamani ukichoka Rudi kwenye maisha yako. Acha ubwege. Fanya Kazi
Pata pesa ya kutosha
Nenda Dubai ukatumikishe Waarabu na wazungu wakutumikie. Pesa ikiisha Rudi nyumbani uendelee kula Dagaa zako.
Hayo ndio maisha. Sio ujifanye uko serious Sana.

Maisha hayahitaji uwe serious Sana. Maisha yanahitaji uishi uenjoy. Ufanye michezo ya hapa na pale.

Ukifika miaka 40 huko unapumzika zako. Unapiga mashambulizi ya kushtukiza.

Sio unakufa hata haujawahi kumtumikisha mzungu au muarabu alafu umlipe. Alaaah!

Acha nipumzike sasa

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kweli lleo umeshusha nondo.

Zaa watoto ukiwa chini ya miaka 40, ili unapofikisha miaka 60, last born wako awe anaingia chuo kikuu na siyo una mtoto yuko shule ya msingi.
 
Back
Top Bottom