Mambo ambayo hutakiwi kufanya ukiwa unaendesha gari la Manual

Nah mkuu si kweli, Hakuna kitu kama icho kusagika kwa selector, haukana any effect unapoegesha mkono, hata ukiweka tofali juu ya gear lever haiwezi kufanya chochote kwasababu mgandamizo wake hauna effect ya kusukuma chini hio lever. mkono usieke kwenye gear kwa sababu ya safety issue tu.

Again Mkuu hii nayo sio sawa na pia more of a safety issue. Unapokanyaga clutch manake una disconnect engine na transmission, huo usago utatokea wap? remember the clutch is always working, and one of its work is to do that. Ukiteremka mlima usikanyage clutch, wacha iteremke ikiwa katika gear, hii inasaidia sana pale unapotaka kubrake

Are you sure?? Kuweka tofali juu ya gear lever hamna kitu?? Hapanaaaa

Na kuhusu kuweka mkono..unajua zile selector za gia zimewekwa kimpangilio..vipi kama mkono uliouegemeza juu ya gear lever ukabadilisha gear pasi na wewe kutaka kwa bahati mbaya?

Na kuhusu kuteremka wapo wanaoweza kubalance clutch na accelerator na gari likaenda as long as anaenda kwa makadirio ya mwendo wa chini
 
1st- try to push down the gear and tell me what you hearing kwanza. The setting ya hio gear lever doesnt allow to push down kwa sababu hakuna space ya kuruhusu ivo ndio maana nkasema no effect. The only effect labda ikatike hio lever, lakini haiharibu gears

2nd- Than that is a safety issue i am talking about, but resting your hands on the lever doesn't cause msuguano. kwenye gari you can do alot of things bila kukusudia, mfano unaweza ukapush accelerator to the limit kwa lengo la kutaka kupiga brake za hafla, that is safety issue, sio kwamba kukanyaga accelerator full time kunafanya msuguano, just safety issues tu.

3rd- mkuu ushawahi endesha manual lakini? katika kilima UNASHUKA, why you need to balance accelerator na clutch? Gari ya manual ikiwa katika mwendo you dont need to use the clutch anymore labda kuwe na mambo ya kusimama simama, na inavotakiwa gari ikianza kuondoka huo mguu wako usiwe nanga, unauondoa katika clutch completely na kuutumia kwa kubadili gear, huku nlipo kisiwani unapoenda kupasishwa driving schol, jamaa mwanzo wa safari mpaka mwisho anautizama huo mguu wako kama umeutia nanga katika clutch. kuna sehemu ya kuweka mguu ukarest once ukichange gear au hujaona? Nyie ndo mnaunguza clutch faster.
 
Pale unapoendesha gari ya manual ile gear lever inawezekana ikawa kama kitu kigumu kwako, lakini unapoizoea ni kitu cha kufurahisha na starehe kucheza nacho hasa unapokuwa barabarani. Kuna baadhi ya mambo ya kuzingitia kabla au hata baada ya kujua kuendesha gari ya manual ili kujiweka salama barabarani na kukilinda chombo chako.

1. Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako

Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.

2. Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo

Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.

3. Usiweke mguu wako muda wote juu ya pedeli ya Clutch

Kuweka mguu wako muda wote kwenye pedeli ya clutch kutaifanya clutch yako kuengage partially na kusababisha kutereza kwa clutch kila mara. Hii inapelekea kusagika kwa clutch na muda mwingine kunapelekea kupoteza kiasi kikubwa cha mafuta kwa sababu ya kupoteza transimission energy kubwa.

4. Usikanyage Pedeli ya Accelerator mpaka mwisho pale unapokuwa kwenye gear ndogo

Kukanyaga pedeli ya Accelerator (mafuta) mpaka mwisho pale gari lako linapokuwa katika mwendo mdogo sio vizuri kwa sababu kutapelekea kutumia kiasi kikubwa cha mafuta bila sababu. Unashauriwa kukanyaga pedeli yako ya mafuta mpaka mwisho pale tu unapokuwa katika gear za kasi ili kulifanya gari lako litembee katika mwendokasi mkubwa.

5. Usibadili Gear bila kukanyaga clutch

Clutch inasaidia kutenganisha injini na gear box kila muda inapokanyagwa. Ni muhimu kukanyaga clutch kwanza kabla ya kujaribu kubadili gear yoyote ili kuipa maisha marefu gear box yako. Clutch Unit hutumika kusafirisha mzunguko wa injini kutoka kwenye injini kwenda kwenye transmission.

6. Usibane brake wakati wa kusimama bila ya kukanyaga Clutch

Wakati unapotaka kusimama ni muhimu sana kukanyaga clutch. Cha kuzingatia hapa ni muda wa kubana clutch, jaribu kupunguza mwendo mpaka pale unapoona sasa unahitaji kusimama na hapo unaruhisiwa kukanyaga clutch na kulifanya gari lako kusimama.

Kumbuka Clutch ni kila kitu linapokuja suala la gari za manual, hakikisha umepata mafunzo ya kutosha kabla ya kuanza kutumia gari la manual katika barabara kuu.

Credits: swahilitech.com
mkuu kuendesha manual siwezi
 
We mtoa post inaonekana ujawaienesha gari umbali mrefu pia umeendesha hizi gari auto hyo Namba (1 ) gari kama Faw na Howo au lori za kichina n pasua kichwa mda wote mkono upo kwenye gear Lever ahaaaaaa ahaa hyo namba (5) baba angu hzo gari nimetaja kuna gia inabid tu uskizie RPM unakanyagia tu bila clutch ukisema utie gia zote 12 ndugu yangu mguu 1 utakua ka Mua mwingine ka mgomba ingawa walioeleza yote ndo utaratibu ila kiukweli kuna mambo inabidi uachane nayo safari ufike. Imargin safari ya 2000+ KMs

Mkuu kuna utofauti wa kuendesha gari kubwa na dogo. Hizi ni tips za gari dogo.
 
1st- try to push down the gear and tell me what you hearing kwanza. The setting ya hio gear lever doesnt allow to push down kwa sababu hakuna space ya kuruhusu ivo ndio maana nkasema no effect.

2nd- Than that is a safety issue i am talking about, but resting your hands on the lever doesn't cause msuguano. kwenye gari you can do alot of things bila kukusudia, mfano unaweza ukapush accelerator to the limit kwa lengo la kutaka kupiga brake za hafla, that is safety issue, sio kwamba kukanyaga accelerator full time kunafanya msuguano, just safety issues tu.

3rd- mkuu ushawahi endesha manual lakini? katika kilima UNASHUKA, why you need to balance accelerator na clutch? Gari ya manual ikiwa katika mwendo you dont need to use the clutch anymore labda kuwe na mambo ya kusimama simama, na inavotakiwa gari ikianza kuondoka huo mguu wako usiwe nanga, unauondoa katika clutch completely na kuutumia kwa kubadili gear, huku nlipo kisiwani unapoenda kupasishwa driving schol, jamaa mwanzo wa safari mpaka mwisho anautizama huo mguu wako kama umeutia nanga katika clutch. kuna sehemu ya kuweka mguu ukarest once ukichange gear au hujaona? Nyie ndo mnaunguza clutch faster.
Mkuu ifahamike kuwa hizi ishu ni kwa ajili ya usalama wa chombo na wakwako binafsi...

BTW sijawahi kukanyaga clutch mwendo wote wa safari eti mguu ukae pale juu ya plate..noo... Hiyo ya kubalance mimi niliona siku moja tu..Also, sijawahi kuendesha gari la manual kwa muda mrefu sana..

Thanks for the challenge.
 
Mkuu kuna utofauti wa kuendesha gari kubwa na dogo. Hizi ni tips za gari dogo.

Kwani kuna mahali kaandika kua ni gari ndogo au kubwa na wewe hujui lolote juu ya mechanism ya engine za magari na hujui zote ziko sawa tu na hujui kua kuna gari kubwa pia ni automatic tena ile auto yake hzo unazosema ndogo n ngumu sana na kama manouver ya gari ndogo hata kubwa unaweza fanya kama kupiga stop engine au kuvua gia toka 16 mpka 2 na gar ikasimama umbal wa mita 100.Chukua hii baba tumecheza na kila aina ya gari ndio mana nikampa maujuz mwenzio.
 
Andika vizuri.
 
True true lakini inategemea na gari.

Ahsante kwa ukumbusho

Gari zote kama ulivosema za manual mfumo ni 1 wa uendeshaji utofauti unakuja sie gari kubwa unahitaji kubalance tela na kua makini usiunguze mabusta ya break kma selection ya gia na RPM uwiano n mbaya hasa kushuka au kupanda.
 
Mkuu ifahamike kuwa hizi ishu ni kwa ajili ya usalama wa chombo na wakwako binafsi...

BTW sijawahi kukanyaga clutch mwendo wote wa safari eti mguu ukae pale juu ya plate..noo... Hiyo ya kubalance mimi niliona siku moja tu..Also, sijawahi kuendesha gari la manual kwa muda mrefu sana..

Thanks for the challenge.

Clutch utie nanga ahaha dk 5 tu unaskia lishaanza kunuka haswa.... na linaungua n shida
 
Pale unapoendesha gari ya manual ile gear lever inawezekana ikawa kama kitu kigumu kwako, lakini unapoizoea ni kitu cha kufurahisha na starehe kucheza nacho hasa unapokuwa barabarani. Kuna baadhi ya mambo ya kuzingitia kabla au hata baada ya kujua kuendesha gari ya manual ili kujiweka salama barabarani na kukilinda chombo chako.

1. Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako

Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.

2. Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo

Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.

3. Usiweke mguu wako muda wote juu ya pedeli ya Clutch

Kuweka mguu wako muda wote kwenye pedeli ya clutch kutaifanya clutch yako kuengage partially na kusababisha kutereza kwa clutch kila mara. Hii inapelekea kusagika kwa clutch na muda mwingine kunapelekea kupoteza kiasi kikubwa cha mafuta kwa sababu ya kupoteza transimission energy kubwa.

4. Usikanyage Pedeli ya Accelerator mpaka mwisho pale unapokuwa kwenye gear ndogo

Kukanyaga pedeli ya Accelerator (mafuta) mpaka mwisho pale gari lako linapokuwa katika mwendo mdogo sio vizuri kwa sababu kutapelekea kutumia kiasi kikubwa cha mafuta bila sababu. Unashauriwa kukanyaga pedeli yako ya mafuta mpaka mwisho pale tu unapokuwa katika gear za kasi ili kulifanya gari lako litembee katika mwendokasi mkubwa.

5. Usibadili Gear bila kukanyaga clutch

Clutch inasaidia kutenganisha injini na gear box kila muda inapokanyagwa. Ni muhimu kukanyaga clutch kwanza kabla ya kujaribu kubadili gear yoyote ili kuipa maisha marefu gear box yako. Clutch Unit hutumika kusafirisha mzunguko wa injini kutoka kwenye injini kwenda kwenye transmission.

6. Usibane brake wakati wa kusimama bila ya kukanyaga Clutch

Wakati unapotaka kusimama ni muhimu sana kukanyaga clutch. Cha kuzingatia hapa ni muda wa kubana clutch, jaribu kupunguza mwendo mpaka pale unapoona sasa unahitaji kusimama na hapo unaruhisiwa kukanyaga clutch na kulifanya gari lako kusimama.

Kumbuka Clutch ni kila kitu linapokuja suala la gari za manual, hakikisha umepata mafunzo ya kutosha kabla ya kuanza kutumia gari la manual katika barabara kuu.

Credits: swahilitech.com
Gea ndogo ni namba 4, 5 na 6. Na gea kubwa ni 1, 2 na 3
 
Back
Top Bottom