Mambo ambayo yananiumiza na yaliyowahi niumiza sana

Mambo ambayo yananiumiza na yaliyowahi niumiza sana

Choosen85

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
1,143
Reaction score
2,475
Wakuu kwema.
Ni jpil njema sana na ya neema kubwa.
Mambo haya yamenitokea na kuniumiza sana.
1. Niligombanishwa na baba yangu mpaka leo hatuelewan na alisema alishani delete mbaya zaidi walioleta yote hayo ni shangazi zangu na mama wa kufikia na baadhi ya ndugu kikubwa ni wivu maana kidogo mzee alikuwa anakauwezo kuliko ndugu zake wote.
Ajabu nina mdogo wng naye ni wa kiume naye hivyohivyo wakamgombanisha na mzee ila wadogo zangu wa kike hawajaletewa kadhia hiyo.
Nipo naendelea na maisha yangu kama vile sina wazazi niliamua kuachana na ndugu wote na kusonga mbele wengi hawajui maisha yangu kwa undani wala kujua nipo wapi.
Mzee nilimuomba msamaha mbele ya ndugu wote kama kuna mahali nilikosea anisamehe akadai mbona hana tatzo na mimi ajabu nilipomtembelea ndo akafunguka alishani delete so niliamua kutemana naye nina zaidi ya miaka 4 sjakanyaga home.

2. Nina mradi wangu wa mbuzi niliajiri kijana wa kuchunga sasa siku ya mshahara ilipofika nikamlipa pesa yake ajabu zilipita kama siku 3 toka nimemlipa sjaonana naye siku 1 akanipigia simu ananiambia hela niliyomlipa aliweka ndani karudi kuchunga hakuikuta na akadai mimi ndo nilienda nikaingia ndani na kweli nilipomlipa kama leo kesho yake nilienda kumpelekea mahitaji yake key ninazo so nilifungua nikamuwekea hapo nikasepa sa akanituhumu nilipoingia nilichukua na hela niliyomlipa wakati skufanya hivyo na wala siwezi inaniumiza sana.
3. Ndugu yangu mmoja ambaye ndiye tumeshibana sana kidogo ndiye anajua mambo yangu siku 1 akanambia ana jambo anataka niambia tukapata muda tukameet aisee alinishushia tuhuma nzito sn mpaka leo najiuliza sjui aliyapata wapi hayo akadai eti mimi namsema kwa watu eti atakufa na ukimwi kama mama yake ambaye naye alishafariki alikuwa aunt yangu aisee iliniumiza sana nilipomshinikiza aniambie aliyesema hzo hbr ni nani alikataa kuniambia bt nilibaki nahisia uwenda ni mkewe ndiye alimpanga maana huwa sielewani na mkewe sababu ya maujinga yake nikahisi taarifa hii anaijua so aliamua kumpanga mumewe mimi nimesema jambo hilo kwa watu ili anigombanishe na ndugu yangu naumia mpk leo.

Ni hayo machache tu japo yapo mengi hebu tushirikishe na ww ni lipi linakuumiza mpk leo au unanishauri nini mkuu......
 
Chief kwa kifupi hakuna mtu perfect duniani hata hao mitume unao sikiaga hawakuwa watu wa kawaida kama sisi mungu aliwafanya special ndo maana na utume wao ukalithishwa kwa vizazi vyao tofauti na hapo chief fanya yako unayoona yanakupa hamani na kutomkosea mungu wako bas inatosha binadamu wengine wote waone kama kima vile hakuna zuri kwenye dunia ukitaka kujifanya et upo perfect kama mitume utafeli mzee
 
😂😂😂😂.una roho nyepesi sana.
Kun mwamba sielewani na ndugu wa mama upande wa mama yake wala baba yake,
Sielewani na ndugu wa baba upande wa mama yake wala baba yake.yaani kiufupi koo zangu zote.naishi kama mnyama.na SIJALI NA MUNGU ANANILINDA.mimi siamini katika NDUGU.baba mwenyewe ana miaka zaidi ya 10 hajaniona.anakaa hapo kimara.mimi nipo bagamoyo.
 
Uko kijijini wapi?. Kwa namna unavyoishi ni ngumu kupata maendeleo,hata ulime,ufuge vipi ni ngumu sana kupata maendeleo kwa tabia zako na za mahala ulipo.

Ushauri wangu kama unaweza kuhamq huko kijijini,hamia walau mjini uchangamane na watu wengine,ujue na uone namna nyingine ya maisha. Muhimu ukifika mjini usichunguze wengine kabisa. Piga kazi zako,bila kuangalia kushoto kulia.

Mwisho sahau maswala ya ndugu. Kama mzee aliku-delete,uwe una uhakika wewe kweli hukumkosea. (Maana ktk maelezo yako kuna kauongo fulani kuna mambo yako umeyaficha). Pia inaonekana wewe ni mtu wa fitina fitina hivi. Sasa kama wewe una uhakika hujamkosea msahau achana nae,piga kazi kwa akili zako zote. Ukitoboa ukiwa alone,mdogo mdogo wataanza kujisogeza kwako. Kwa sasa unatengwa ksbb huna kitu. Pia jitathimini wewe pia
 
Kwamba nipo kijijini au siyo kwa taarifa yako Dar nimezaliwa nimesoma hapo mpk udsm na mzee huko ndo kwake kbs ameshastaafu ana makazi yake dsm.
Nipo Mwanza usagara tu hapa jirani na kivuko
Mambo ya kwamba kuna kitu ninaficha sjui nn hzo ni hisia zako tu na ujuaji wako. Swala la kumkosea mzee kama umesoma kwa umakini nilichoandika bs usingekurupuka hivi huoni mpk niliomba msamaha tena mbele ya ndugu zake wa damu mbele ya ndugu wengne maana tulikutana msibani.
Otherwise thanks kwa ushauri wako pia na ujuaji wako.
 
😂😂😂😂.una roho nyepesi sana.
Kun mwamba sielewani na ndugu wa mama upande wa mama yake wala baba yake,
Sielewani na ndugu wa baba upande wa mama yake wala baba yake.yaani kiufupi koo zangu zote.naishi kama mnyama.na SIJALI NA MUNGU ANANILINDA.mimi siamini katika NDUGU.baba mwenyewe ana miaka zaidi ya 10 hajaniona.anakaa hapo kimara.mimi nipo bagamoyo.
Kudadeki!
 
Back
Top Bottom