Mambo ambayo yananiumiza na yaliyowahi niumiza sana

Imenigusa iyo story ya wewe na mshua wako, wazee wetu wanabeba mengi sana moyoni ndio vile tu dunia ipo corrupted na ferminism kwaiyo wazee wanaonekana wabaya.

Mimi mzee wangu walitemana na bi mkubwa nikiwa mtoto mchanga kabisa, hatukuonana wala kuwasiliana na mzee, ningefanya maamuzi ya kuchagua upande ingekua rahisi kuchagua upande mama na kumchukia mzee kwa kuona kanitelekeza lakini pamoja na kwamba nilikua mtoto sikua na hard feelings na mzee

Nimekuja kuonana na mzee kwa mara ya kwanza alikuja kijijini kwenye msiba wa bi mkubwa wakati huo ni form 1, ilikua kipindi cha likizo kwaiyo msiba ulivyoisha tu nikaenda nae nyumbani kwake niliishi vizuri sana na mzee mpaka anafiriki Momi nipo form 5, naweza kusema mzee ni mtu mwema zaidi niliyewahi kuishi nae maishani mwangu, mpaka kwenye wosia wake kaniandika kama mmoja wa warithi.

Sijui kilichowatenganisha wazazi wangu kwaiyo nitabaki kuwaenzi wote wawili kama wazazi wangu. Wanaume tunatakiwa kujua tunaishi kwenye ferminism world kwaiyo tunatakiwa kuwa wamoja maana hatuna mkombozi mwingine zaidi ya sisi wenyewe tu.
 
Kuna msemo unasema "Do not let your failures define your failures"..Changamoto tunazopitia wanadamu ni nyiiingi yatupasa tumkabidhi Mungu atuongoze katika maisha yetu maana mawazo anayotuwazia ni mema Sana maishani mwetu .

Pole kwa yote yalitokusibu
 
Hauwezi kitenga na ndugu kwakuwa haujawa well established lakini nimejaribu kupitia maelezo yako kuna mambo ya kiroho (yaweza kuwa ushirikina) umefanyiwa ndio maana kila uchao likitoka hili linakuja lile utasumbuka na kuona watu au ndugu hawafai jitafute kwenye yataisha kiroho safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…