Mambo gani umeyafanya au kuyapitia maishani mwako ambayo hutamani mwanao/mtu mwingine kuyapitia?

Mambo gani umeyafanya au kuyapitia maishani mwako ambayo hutamani mwanao/mtu mwingine kuyapitia?

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Ahlan wa sahlan

Ukiwa kama mwanadamu lazima kuna mambo mabaya umeyapitia katika maisha yako ambayo hutamani mwanadamu mwingine (mwanao,ndugu n.k) aje kuyajua na kuyapitia.

Binafsi sitapenda mtu yeyote hususani wanangu aje kujua kuhusu Kamari (kubeti).

Why? Ni ulevi ambao mtu akishauonja ni ngumu sana kuuacha.

Je wewe ni mambo gani hutapenda mwanao au ndugu yako ayapitie maishani mwake?

Karibu
 
Sitapenda Mtu yoyote wa kizazi changu akatae Shule.

Avute sigara au Bangi.

Anywe Pombe.

Akose utiifu kwa Wazazi,hasa Mama yake.

Alale na Wanawake watu wazima.

Nimechora mstari mwekundu kwa hayo.

Sitaki Wanangu warudie makosa yangu.
 
Kubeti na pombe.

Pombe nakunywa hadharani ila kubeti najificha na huwa nawasema vibaya sana wanaobeti kukiwa na hiyo mada.

Sema kuna siku nabahatisha nambutua kanjibai lakini na kipigo hakiepukiki.

Sitaki kabisa mwanangu aige au ajue kuwa mimi baba yake nabeti.
 
Wakwangu wapitie humu humu nilipopitia mimi Nb: Kwa uzembe wao lakini.
 
Ahlan wa sahlan

Ukiwa kama mwanadamu lazima kuna mambo mabaya umeyapitia katika maisha yako ambayo hutamani mwanadamu mwingine (mwanao,ndugu n.k) aje kuyajua na kuyapitia.

Binafsi sitapenda mtu yeyote hususani wanangu aje kujua kuhusu Kamari (kubeti).

Why? Ni ulevi ambao mtu akishauonja ni ngumu sana kuuacha.

Je wewe ni mambo gani hutapenda mwanao au ndugu yako ayapitie maishani mwake?

Karibu
Sitaki mwanangu awe polisi kwani walishanifanyia vitendo vibaya tena mbele ya watoto wangu,nilipigwa vibao mbele yao wakawa wanalia,nilijikakamua na kuleta noma ambayo hao PT hawatasahau maishani mwao kwani si mwenye jicho, jino,uso kilichotoka salama,ilinigharamu sana baada ya hapo but nilirudisha heshima kwa wanangu.

Toka siku hiyo niliwaambia siku niko hai au nimekufa nikisikia mmojawenu amekuwa polisi namlaani.Sumu ambayo nimewalisha sidhan kuna mwanangu anaweza kuwa PT

NYINGINE :Sitaki wanangu wanywe pombe hata kwa kuonja hili ni somo ambalo nawambia kila nikiwa nao,mie bado nakunywa na wameshuhudia madhara ya pombe kupitia kwangu,sidhani km wanaweza kunywa maishani mwao,pombe imenipotezea kazi za maana kama mara 3 nikawa takakata,nina kazi sasa naitunza km yai wanangu wameona ni jinsi kipindi cha pombe kupita kiasi kilivokuwa na kipindi cha sasa pombe za wastani kilivo
 
Sitaki mwanangu awe polisi kwani walishanifanyia vitendo vibaya tena mbele ya watoto wangu,nilipigwa vibao mbele yao wakawa wanalia,nilijikakamua na kuleta noma ambayo hao PT hawatasahau maishani mwao kwani si mwenye jicho, jino,uso kilichotoka salama,ilinigharamu sana baada ya hapo but nilirudisha heshima kwa wanangu.Toka siku hiyo niliwaambia siku niko hai au nimekufa nikisikia mmojawenu amekuwa polisi namlaani.Sumu ambayo nimewalisha sidhan kuna mwanangu anaweza kuwa PT
NYINGINE :Sitaki wanangu wanywe pombe hata kwa kuonja hili ni somo ambalo nawambia kila nikiwa nao,mie bado nakunywa na wameshuhudia madhara ya pombe kupitia kwangu,sidhani km wanaweza kunywa maishani mwao,pombe imenipotezea kazi za maana kama mara 3 nikawa takakata,nina kazi sasa naitunza km yai wanangu wameona ni jinsi kipindi cha pombe kupita kiasi kilivokuwa na kipindi cha sasa pombe za wastani kilivo
Dunia hii Mama lukumba lukumba, dunia ina mwendo kama wa ngamia × 2.
 
Kuchemsha dodoki changa na kulila, si taki hiyo fedhea tena Dunia ya sasa sio Ile ya Jana, njaa kitu Cha mwisho ku fikiri kupita kwenye uzazi wangu isipokuwa kwa uzembe wao!
 
Kuchemsha dodoki changa na kulila, si taki hiyo fedhea tena Dunia ya sasa sio Ile ya Jana, njaa kitu Cha mwisho ku fikiri kupita kwenye uzazi wangu isipokuwa kwa uzembe wao!
Mkuu hebu fafanua, dodoki ni kitu gani?
 
Sitampangia mwanangu cha kufanya, atafanya anachopenda mradi havunji sheria. Ninaposema cha kufanya namaanisha shughuli ya kumuingizia kipato
 
Back
Top Bottom