Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hebu fafanua hapo kwenye kulala na wanawake watu wazimaSitapenda Mtu yoyote wa kizazi changu akatae Shule.
Avute sigara au Bangi.
Anywe Pombe.
Akose utiifu kwa Wazazi,hasa Mama yake.
Alale na Wanawake watu wazima.
Nimechora mstari mwekundu kwa hayo.
Sitaki Wanangu warudie makosa yangu.
Kamari ni ulevi wa siri sana, yaani hata mkeo hawezi kujua kama unabeti.Huwezi amini hadi mapadri na masheikh wanabeti. Ni ulevi uliorahisishwa kiganjani.Kubeti na pombe.
Pombe nakunywa hadharani ila kubeti najificha na huwa nawasema vibaya sana wanaobeti kukiwa na hiyo mada.
Sema kuna siku nabahatisha nambutua kanjibai lakini na kipigo hakiepukiki.
Sitaki kabisa mwanangu aige au ajue kuwa mimi baba yake nabeti.
Kuwausia watoto ni jambo jema sanaSitaki mwanangu awe polisi kwani walishanifanyia vitendo vibaya tena mbele ya watoto wangu,nilipigwa vibao mbele yao wakawa wanalia,nilijikakamua na kuleta noma ambayo hao PT hawatasahau maishani mwao kwani si mwenye jicho, jino,uso kilichotoka salama,ilinigharamu sana baada ya hapo but nilirudisha heshima kwa wanangu.Toka siku hiyo niliwaambia siku niko hai au nimekufa nikisikia mmojawenu amekuwa polisi namlaani.Sumu ambayo nimewalisha sidhan kuna mwanangu anaweza kuwa PT
NYINGINE :Sitaki wanangu wanywe pombe hata kwa kuonja hili ni somo ambalo nawambia kila nikiwa nao,mie bado nakunywa na wameshuhudia madhara ya pombe kupitia kwangu,sidhani km wanaweza kunywa maishani mwao,pombe imenipotezea kazi za maana kama mara 3 nikawa takakata,nina kazi sasa naitunza km yai wanangu wameona ni jinsi kipindi cha pombe kupita kiasi kilivokuwa na kipindi cha sasa pombe za wastani kilivo
Hatuzungumzii kuhusu kumpangia bali kumuhusia mambo ambayo yamekugharimu wewe katika maisha yako hivyo hutaki kuona mwanao nae anayapitiaSitampangia mwanangu cha kufanya, atafanya anachopenda mradi havunji sheria. Ninaposema cha kufanya namaanisha shughuli ya kumuingizia kipato
Funguka mkuu huenda wengine tukapata maonyoHata nakosa la kusema maana...
Wahindi walikufanyaje mkuu?Kufanya kazi kwa wahindi. Aki nitapambana at least wafanye kazi kokote lakini sio kwa hao.
Zilikufanya nini hizo links?kusambaza link za tala
Naamini ivo.Thank youSafi sana... Utatoboa soon...
Yani kuna watu wanabeti hadi wanakondaBinafsi sitapenda mtu yeyote hususani wanangu aje kujua kuhusu Kamari (kubeti).
Acha tu mzee.....hili ni janga. Hakuna ulevi mzuri, kubeti ni ugonjwa wa akili ambapo mbetiji hujawa na false hopes daily kuwa atafanikiwa kupitia kamari.Yani kuna watu wanabeti hadi wanakonda
Ndio sitampangia kwa sababu sitaki apitie niliyopitia mimi kwa sababu ya kupangiwaHatuzungumzii kuhusu kumpangia bali kumuhusia mambo ambayo yamekugharimu wewe katika maisha yako hivyo hutaki kuona mwanao nae anayapitia
Ndio sitampangia kwa sababu sitaki apitie niliyopitia mimi kwa sababu ya kupangiwa
Una Watoto Wangapi?Kuishi maisha magumu...sitoacha kupambana juu ya wanangu.
WawiliUna Watoto Wangapi?
Mkuu hebu fafanua hapo kwenye kulala na wanawake watu wazima