mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 11,005
- 20,805
Ngoja niongeze nyama mkuu..VITU 4 AMBAVYO HUFUNDISHWI SHULENI LAKINI NI MUHIMU MAISHANI MWAKO
Shuleni watu hufundishwa kufanikiwa tu ila hakuna somo la kumuelekeza mtu afanye nini anapokuwa katika nyakati ngumu sana
Kila mtu amekaririshwa kuwa soma sana,faulu utapata kazi nzuri kisha utakuwa na maisha mazuri
Hivyo kila mtu husoma na kufanya kazi kwa bidii sana ili afanikiwe kuwa na maisha mazuri
Endapo hatapata maisha mazuri ataona hakuna thamani ya kwenda shule hivyo kwake shule haina maana
Unatakiwa utambue kuwa kama hutojifunza kwenye historia unakwenda kurudia makosa ya watangulizi wako
Unaweza kukumbuka mwaka ambao maisha yalikuwa mazuri nchi nzima kwamba kila mtu ni mwenye afya,hana kesi,hana madeni,kila mtu maisha mazuri sherehe kila nyumba ?
Haijawahi kutokea na haiwezi kutokea hivyo tuache kujidanganya bali tuangalie maisha katika uhalisia sio kuwapa watu matumaini ya uongo
Ukweli ni kuwa maisha bila matatizo hayana maana hivyo kwa sababu watu wengi hawataki matatizo hivyo huteseka kwa kila tatizo
Madaktari wasome ili iweje kama hakuna wagonjwa ?
Watu waende jeshini ili iweje kama upo usalama kila kona
Watu watafute walinzi wa mageti ili iweje kama hakuna uhalifu?
Maana yake ujiandae na matatizo au usijiandae lazima utapata matatizo tu
Matatizo ni kama mvua hivyo itanyesha kwa watu wote ila kila mmoja ataona uzuri wa mvua au ubaya wa mvua ila mvua ipo palepale
Ndiyo sawa na matatizo kwako utaona sio tatizo kwa mwengine ataona ni tatizo maana yake maisha hayawezi kuwa fair kwa kila mtu.
Mambo 4 shule huwezi kufundishwa ni
1.KUKABILIANA NA NYAKATI NGUMU
Watu wengi hufanya vizuri shuleni lakini hawana elimu ya kuibuka baada ya kuanguka
Wengi wanajua fanya kazi kwa bidii kisha utapanda vyeo na kuwa na mshahara mzuri hivyo utakuwa na maisha mazuri sana
Tatizo ni kwamba hakuna anaewafundisha kuwa ukifanya kazi kwa bidii sana na usipopanda vyeo ufanye nini?
Wengi huambiwa wakiwa na bidii kazini ndio watadumu kazini lakini hakuna mwenye kuwaambia kuwa kampuni inaweza kupunguza wafanyakazi wake kama haipati faida bila kujali juhudi za wafanyakazi
Endapo utapata matatizo na hukujiandaa kuyapokea lazima utapata msongo wa mawazo
Wafanyakazi wengi maofisini huwezi kuwaona wanatabasamu muda wote wamenuna mpaka unaogopa kuwauliza chochote wengi huona ni jambo la kawaida
Hakuna mtu ambaye yupo kawaida muda wote amenuna
Ukiona mtu amenuna kuna kitu hakipo sawa
2.KUKATALIWA NI KAWAIDA
Haijalishi umesoma kwa kiwango gani lazima utakataliwa tu
Hakuna mtu mzuri kwa 100% au mbaya kwaa 100%
Wapo hujiua tu kisa marafiki zao wamepata kazi yeye amekosa
Wapo huamua kuwa walevi kisa tu wamekosa ajira
Wapo huamua kuishi kwa kulalamika kisa ajira hamna
Wapo hujidhuri kisa talaka
Wapo husomesha wachumba zao kisha wakiambiwa hakuna ndoa huamua kuwaua wachumba zao kisa kukataliwa
Lazima utambue kuwa utakataliwa sana labda usiombe chochote kwa mtu yeyote
Kwenye kukataliwa hakuna msomi,tajiri, maskini, Handsome, beautiful,mzuri wa sura au mbaya
Mwenye muonekano mzuri au mbaya
Hakuna cha rangi,urefu,ucheshi,upole wala kipaji bila kujali upoje lazima utakataliwa sana katika maisha yako kuliko kukubaliwa
Sehemu kubwa ya maisha ni maumivu na sehemu ndogo tu ndio sherehe
Ndio maana unasoma miaka 4 sekondari lakini graduation ni siku moja tu
Kama hukujiandaa kupokea taarifa mbaya lazima utateseka sana
3.NAMNA YA KUPOKEA TAARIFA MBAYA
Hakuna somo la kukuelewesha namna ya kupokea taarifa mbaya kama kifo,ajali,talaka,ugomvi,namna ya kuishi na watu wenye tabia tofauti na zako
Hakuna mwenye kukufahamisha kuwa maishani mwako utapata matatizo bali utaambiwa ukisoma sana ndio unakuwa na maisha mazuri
Ukweli ni kuwa huwezi kuepuka matatizo na endapo huwezi kutatua matatizo katika maisha yako ni wewe tu unaekwenda kuteseka
4.NAMNA YA KUBADILIKA KUENDANA NA MAZINGIRA
Shuleni mnaweza kusoma somo moja baba na mtoto notes zilezile na nyote mkapewa vyeti lakini katika maisha hakuna kitu kama hicho
Mnaweza kuwa na tatizo moja lakini kila mmoja akatumia njia tofauti
Shule ulijibu swali tofauti na mwalimu alivyokuelekeza unakosa hata kama umekesha unasoma
Katika maisha ni kuwa hakuna maelekezo ya namna ya kuishi bali unaishi kuendana na wakati uliopo
Huku unakosea kwanza ndio unajifunza ila shule unajifunza kwanza kisha unapewa mtihani na mtihani lazima uwe katika silabasi
Matatizo ya kwenye maisha hayana silabasi
Huku unaweza kuzaliwa katika familia ya kitajiri baba yako akafa na ndugu wakachukua mali zote ukaishi maisha ya kimaskini
Unaweza zaliwa katika maisha mazuri lakini ukapoteza kila kitu na usijue pa kuanzia
Huku hakuna kuanza shule ni miaka 7 huku unaweza kuwa na miaka 23 ukapata matatizo ambayo alitakiwa kupata mzee wa miaka 60 lakini bado unatakiwa uyatatue
Lazima ujue kuwa ahadi kuvunjwa ni kawaida,unaowaamini kukugeuka ni kawaida
Unaowadai kukunyima pesa kawaida
Unaowasaidia kukuacha mpweke wakati mgumu ni kawaida
4.MAISHA SIYO VILE UNAPANGA WEWE
Kukosolewa ni kawaida
Watu kukuchukia ni kawaida
Watu kukushangilia leo na kesho kukuzomea ni kawaida
Kanuni mbili za kukusaidia ukiwa na matatizo
1. Accept Whatever comes to your life
Pokea chochote kinachotokea katika maisha yako bila kukasirika kwa sababu kukasirika sio suluhisho la matatizo yako
"Train your mind to accept disappointment because they will come from people you trusted most"
2.Change what you can and let go what you can't change
Kubali kuwa kile huwezi kukibadilisha sio jukumu lako kujitesa juu yake
Huwezi kupanga fursa gani zije kwako ila unapanga ufanye nini kwa fursa zinazokuja kwako
Huwezi kufuta historia yako bali unaweza kuandika historia mpya
Kujitesa kwa makosa ya zamani ni kupoteza muda
Huwezi kuifanya jana irejee na fursa za jana zirejee bali unaweza kuwekeza nguvu zako kwa fursa mpya
Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
5 -- ukiachwa achika.
By mwandende.