Mambo Haya Kumi (10) Usiyojua Kuhusu Fedha Ndiyo Yanakufanya Uendelee Kuwa Masikini.

Hongera sana ndugu! kwa hatua uliyoifikia,
Nakupa pongezi kubwa sana, ila pia nina ushauri kwako,

Kwa ambao huwa wanasoma vitabu kwa hayo uliyoyaandika hapo juu nikwamba tumesoma tayari kitabu kizima,
Bado hatujakutana na wazo jipya, hata kama hakuna mawazo mapya basi sijapata ushawishi sababu naona mbona sina kipya cha kujifunza?
Ushauri wangu tumia lugha zaidi ya uandishi kuliko lugha ya maelezo,
Hata kama nikiwa na majibu yakwamba yai litachemsha ila bado nahitaji kujiuliza litachemshwaje? hii ndio point yangu

Zingatia lugha ya uandishi zaidi ongeza na sanaa yako basi utafanya makubwa zaidi, ila hongera sana kwa ulilolifanya
 
Asante kwa ushauri,
Kitu kikubwa ambacho naamini ni kwamba kila mtu ana kitu cha kujifunza kwenye kila kitu.
Hivyo kama umesoma maelezo hayo na ukaona hakuna cha kipya cha kujifunza, maana yake wewe siyo mtu wa kujifunza na hilo linaweza kuwa kikwazo kwako kupiga hatua zaidi ya pale ulipo sasa.
Mimi binafsi huwa nasoma vitabu nilivyoandika mwenyewe, na kila ninaposoma kuna kitu kipya najifunza, kuna mawazo mapya yanaunganika na siwezi kumaliza kusoma na nikabaki kama nilivyokuwa.
Na pia kuna baadhi ya vitabu ambavyo huwa nimechagua kusoma kwa kuvirudia rudia, vingine nimeshasoma zaidi ya mara kumi, lakini kila nikirudia kusoma kuna kitu kipya naondoka nacho, ambacho awali sikukipata au kukielewa vizuri.
Hivyo nikukaribishe ujipatie kitabu na ujifunze na kwa hakika kuna mapya utaondoka nayo, ambayo kama utakwend akuyafanyia kazi basi hutabaki pale ulipo sasa.
Karibu sana.
 
Uncle Sam system
uncle Sam system
 
Ukisikia kuna fursa unakaribishwa ujue wewe ndio fursa
Mkuu achana na mitazamo hasi, itakukwamisha wewe mwenyewe kufanikiwa.
Pata maarifa na yatumie kupiga hatua zaidi.
Maarifa ndiyo uwekezaji pekee ambao hakuna anayeweza kukuibia.
Karibu sana.
 
Uncle SAM SYSTEM
 
Karibu Kwenye Uzinduzi Wa Vitabu; Elimu Ya Msingi Ya Fedha Na Tano Za Juma.

Rafiki yangu mpendwa,

Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye uzinduzi wa vitabu vipya ambavyo nimevitoa.

Vitabu hivyo ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, ambapo ndani yake utajifunza mambo yote muhimu sana kuhusu fedha, ambayo hujawahi kupata nafasi ya kujifunza sehemu nyingine yoyote kwenye jamii.

Kitabu cha pili ni TANO ZA MAJUMA 5O YA MWAKA, hiki ni kitabu kikubwa ambacho utakisoma kwa mwaka mzima. Ndani yake kuna uchambuzi wa kina wa vitabu 50 vya mafanikio, siri 50 za mafanikio na mafunzo mengine mazuri kwako kuweza kuchukua hatua na kufanikiwa zaidi.

Uzinduzi wa vitabu hivi viwili utafanyika jumamosi ya tarehe 03/08/2019 kuanzia saa 8 kamili mchana mpaka saa 12 kamili jioni.

Uzinduzi utafanyika jijini dar es salaam, kwenye ukumbi wa hoteli ya GOLDEN PARK iliyopo Sinza Kumekucha, Dar es salaam.

Ada ya kushiriki uzinduzi huu ni tsh elfu 10 (10,000/=).

Ili kushiriki uzinduzi huu unapaswa kuweka nafasi yako mapema kwa sababu nafasi za ushiriki ni chache. Kuweka nafasi ya kushiriki semina, tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu, pamoja na maelezo kwamba nitashiriki uzinduzi wa vitabu kwenda namba 0717396253 au 0755953887.

Ada ya kushiriki uzinduzi huu unapaswa kulipa kabla ya tarehe 01/08/2019.

Karibu sana kwenye uzinduzi wa vitabu hivi viwili muhimu ambavyo vitakuwezesha kupiga hatua sana kwenye maisha yako.

Kwenye uzinduzi huu, pamoja na kupitia yale muhimu kutoka kwenye vitabu hivi viwili, utajifunza yafuatayo;

1. Kwa nini uwekezaji kwenye maarifa ndiyo uwekezaji pekee unaolipa sana.

2. Sababu 10 kwa nini unapaswa kusoma kitabu kila siku na kutembea na kitabu popote unapokuwa.

3. Jinsi ya kupata muda wa kusoma kila siku hata kama umebanwa na majukumu yako mengine.

4. Jinsi unavyoweza kusoma kitabu kimoja kila mwezi.

5. Jinsi ya kutoa kitabu kilichopo ndani yako na ukaacha alama hapa duniani.

Uzinduzi huu wa vitabu siyo wa kukosa, karibu tujifunze kwa pamoja na uweze kupata maarifa sahihi pamoja na hamasa ya kuchukua hatua ili kufanikiwa zaidi.

Tuma sasa majina yako na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki uzinduzi kwenda namba 0717396253 au 0755953887 na nafasi yako itahifadhiwa.

Rafiki na kocha wako,

Dr. Makirita Amani.
 
Hongera sana doctor nitanunua nakala yangu! Nimehisi nasoma "the richest man in Babylon" na akina Kiyosaki

Hii itafungua watu akili

Kudos doctor.......
 
Kwingine kote tumeenda sawa. ..hapo kwenye Maisha ya kitajiri siyo rahisi umenichanganya kabisa.
 
Kwingine kote tumeenda sawa. ..hapo kwenye Maisha ya kitajiri siyo rahisi umenichanganya kabisa.
Jipatie kitabu usome, utaelewa kwa kina na kama kuna mahali utakwama au kutokuelewa tunaweza kuwasiliana nikakupa ufafanuzi.
Karibu sana.
 
Hakika nimeipenda sana makala yako naiona wazi ina funzo kubwa sana ndani yake! Ngoja nikomae nipate kitabu hicho naona kina kitu cha kujikwamua! Hongera sana mkuu kwa kazi nzuri
 
Ili kurahisisha na kuondoa hofu ya watu kuhisi kutapeliwa ungetafuta mawakala kila mkoa ili mtu akihitaji anaenda moja kwa moja analipa anaondoka na kitabu. Ni mawazo yangu lakini mkuu.
 
Ili kurahisisha na kuondoa hofu ya watu kuhisi kutapeliwa ungetafuta mawakala kila mkoa ili mtu akihitaji anaenda moja kwa moja analipa anaondoka na kitabu. Ni mawazo yangu lakini mkuu.
Asante kwa mawazo mazuri,
Hii inayofanyika sasa ni pre order ndiyo maana unaona kinauzwa kwa ofa.
Baada ya kuzinduliwa kitauzwa kwa bei kamili na kitapatikana kupitia mawakala mbalimbali nchi nzima.
 
Mara ya kwanza nilipokisoma kitabu Rich daddy poor daddy nilihisi utajiri na financial freedom vikimiminika ndani ya roho yangu, nikaona kabisa nguvu ya maandishi kwenye maisha yangu, but in the long run ndipo nilikuja kuujua upande wa pili wa kile nilichokiona kuwa ukweli wa kimuujiza, sasa nipo huru, na hata sikumbuki nilichokisoma huko miaka hiyo, thanks for sharing
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…