Hivyo kama umesoma maelezo hayo na ukaona hakuna cha kipya cha kujifunza, maana yake wewe siyo mtu wa kujifunza na hilo linaweza kuwa kikwazo kwako kupiga hatua zaidi ya pale ulipo sasa.
Ndugu unasafari ndefu sana kuliko ambavyo nilikuwa nakufikiria,
NIkajua may be ni mtu fulani leaner but kumbe ni walewale wajuaji,
NImekupa ushauri wa mambo mawili ya msingi
1.Lugha
2.Sanaa
Sasa nakufafanulia
Lugha Pamoja Na Sanaa
Usipotumia lugha fulani yakumshawishi mtu ama lugha inayomfanya mtu ajisikie ama apende kusoma kitu chako inakuwa ni kazi bure
Msomaji hapaswi akutafute mwandishi ulikuwa unataka kusema nini, unapaswa kumfanya msomaji umtafute anahitaji nini,
lugha unayoitumia na sanaa yako ni yakumfanya msomaji akutafute wewe mwandishi ulilenga nini,
Ndio maana nikakuambia mfumo unaoutumia hata ulivyoeleza kwa ambao tumezoea kusoma vitabu haujanishawishi niweze kununua nakala hata moja maana tayari nikilekile umeeleza kwa lugha ya kawaida isiyokuwa na mvuto.
Umenilazimisha sana kuzungumza haya ila sina budi kukueleza,
Lengo ni hili
Andika lugha itakayomvutia msomaji
kuna waandishi wameandika mambo ya kawaida sana ila walitumia lugha vizuri na sanaa wakaweza kuuza sana nakala zao na walifanikiwa kututeka wasomaji
Mfano soma kitabu "
KISS THAT FROG" Ni mambo ya kawaida sana yaliyoandikwa yaani kwa wanaotafuta maarifa hasa kwa njia ya maandishi wamekutana nayo mara nyingi mno,
Ila yameonekana kama mawazo ya kipekee sababu katumia Lugha ya kutushawishi wasomaji na amefanikiwa.
sasa rudia tena kusoma maoni yangu ya mara ya kwanza kisha acha kuwa mjuaji unapokuja mbele za watu kuwakilisha mawazo yako
Tumia lugha rafiki