Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Manung'uniko yamezidi. Lawama zimejaa. Kelele zimeongezeka. Eti kwanini Mungu anatuacha tunateseka? Eti kwanini anatuacha tunaumia, tunaugua, tunakufa..?
Ulisoma kitabu gani wewe kwamba Mungu aliumba bunduki, mabomu na virungu? Wanadamu wenyewe ndio wanaotengeneza silaha hizo kisha wanazitumia kupigana. Halafu wanaopigwa na kuachwa na majeraha wanamwangushia lawama Mungu eti kwanini anawaacha wanaumia?!
Ulisikiliza redio gani wewe ikakuambia kwamba Mungu ndiye aliyeweka mipaka ya nchi na kubuni majina ya nchi zilizopo leo? Majina ya nchi na mipaka mliiweka wenyewe. Baada ya kuigawanya dunia mpendavyo, kila nchi ikaanza kujivuna: Eti "sisi tuna akili kuliko nyinyi." "Eti sisi tuna nguvu kuliko nyinyi." Matokeo yake mmesababisha machafuko, magomvi na vita. Ndege zisizo na rubani zinapiga, miji mizuri inageuzwa magofu. Watoto wanabaki yatima, halafu mnamlaumu Mungu eti kwanini anaruhusu mabaya yanawapata?!
Ulisoma gazeti gani wewe kwamba Mungu aliumba sukari? Mungu aliumba vyakula vyenye "natural sugar" nyie mkaamua kujitengenezea sukari yenu kisha mnaiweka kwenye juice, kwenye maziwa, kwenye keki... halafu mkipata kisukari mnamnung'unikia Mungu, eti kwanini anaacha magonjwa yanawatesa?! Ulisikia wapi wewe kwamba Mungu ndiye aliyeumba hizo dawa mnazokunywa kisha zinawaletea "side effects" kibao?
Uliambiwa na nani wewe kwamba Mungu ndiye aliyetunga katiba na sheria zinazotumika katika nchi mbalimbali? Sheria mlizitunga wenyewe. Sheria hizo sasa zinawabana halafu mnamlalamikia Mungu eti kwanini haingilii kati. Aingilie kati mambo mliyoyapitisha wenyewe? Mambo yote hayo mabaya mmeyasababisha wenyewe, acheni kumnung'unikia Mungu.
Please, acheni kabisa kumlaumu na kumnung'unikia Mungu. Mungu aliiumba dunia isiyo na mabaya tunayoyaona leo. Hapo mwanzo kila kitu kilikuwa chema. Mabaya yaliyopo leo duniani ni sisi wenyewe tumeyasababisha kwa sababu ya dhambi zetu na tamaa zetu. Tukiendelea kumnung'unikia Mungu, yatatupata madhara makubwa. Soma Biblia uone yaliyowapata wana wa Israeli walipomnung'unikia Mungu baada ya kutolewa utumwani, Misri.